Hakuna raha kubwa sana kama kumfundisha mtu kitu na akakuelewa kwa umakini sana na kufanya kile kilichofundishwa.Umuonapo moyo wako utafurahi nawe utajitanua mwanafunzi wangu yule.Duniani kila mtu huzaliwa na akili zake jambo kubwa ni matumizi tu baada kuwa mkubwa na kile ambacho ataongezewa darasani iwe elimu ya nyumbani ama shuleni.
Miaka kadhaa nyuma nilikuwa mfatiliaji wa kikosi cha Sc Constantine katika michuano ya klabu bingwa ambayo iliwahi kutinga hatua ya robo fainali.
Tangu kuanza kwa michuano klabu hiyo ya nchini Algeria ilitumia asilimia 99% ya wachezaji wa nchini Algeria kwenye kikosi cha kwanza wastani wa wachezaji 10 kati ya 11 walikuwa ni wazawaa wa Algeria.
Kwa mara ya kwanza ilipoteza mechi yake kwenye hatua ya makundi lakini ikiwa tayari imefuzu kuingia robo kwa tafsiri pia unaweza ukasema wao walikuwa wanakamilisha tu mechi.
Haikuwa na wachezaji wengi kutoka mataifa mengine ambao walianza kikosini,hawakutumia nguvu nyingi kujieleza uwanjani lakini kila mmoja mpenda michezo na mfatiliaji mkubwa alishuhudia,labda kizazi cha nataka mechi ya Simba na Young Africans sports club pekee ndio kitakua hakikuona.
Sihitaji kuwasifia wachezaji wao na wala kuwakosoa sana wachezaji wetu lakini ukweli shule sio lazima uingie darasani katika majengo ya kata au private school.
Kikosi hiki cha Constantine ambacho ukitazama wachezaji hawa Houssam Limane (GK) π©πΏπΏ, Houcine Benayada π©πΏ,Nasreddine Zaalani π©πΏ,Islam Chahrour π©πΏ,Yassine Salhi π©πΏ,Fouad Haddad π©πΏ,Mohamed Walid Bencherifa π©πΏ,Nassim Yattou π©πΏ,Dylan Bahamboula π¨π¬,Adil Djabout π©πΏ,Abdenour Belkheir π©πΏ
Kilikuwa ni kikosi ambacho kiliwafikisha hadi robo fainali ya michuano hii ya klabu bingwa Africa. Ukitazama unaona Dylan Bahamboula pekee ndio alikua anapewa nafasi uwanjani na wapizani hawakutoka.
Katika michezo yote walitumia wachezaji kumi wa ndani ya Algeria huku mmoja tu anakuwa wa nje ya taifa lao. Nataka niwakumbushe wachezaji wetu wazawa hili liwe somo kwao wanatakiwa kuonyesha wanaweza kuliko kushuhudia wageni wakitamba katika aridhi yao,wageni wanatamba katika vikosi vyao.
Wanatakiwa kuwa na wivu wa maendele/mafanikio ya kufanya vizuri pale wanapopata nafasi kwenye timu zao.
Dhana potofu ya kuwa wao hawawezi kimataifa wanatakiwa kuachana nayo,dhana potofu waliyokuwa nayo kushindwa kushindana na wageni wanatakiwa kuitupa mbali, wachezaji Dickson Job,Mohamed Hussein, Shomar Kapombe, Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na wengine baadhi wameonyesha uwezo mkubwa mbele ya hawa hawa wageni.
Kalamu za waandishi na midomo ya wachambuzi inawatetea sana kiasi kwamba inaonekana kuweka ubaguzi kwa wageni ambao tunawapata hasa pale wanapopata nafasi lakini swali libaki kwenu kwa nini mnashindwa kuonyesha uwezo ili mpate namba za kudumu kama wengine.?
Kwa nini wageni wanakuja Tanzania lakini ninyi hamuwezi kwenda kwao kwa nini.?, Elimu ianze kwenu wenyewe kuwa na mawakala wenye upeo mkubwa wa kuwa washauri wenu,wenye nguvu ya kuwafanya mtoke nje ya Tanzania, mawakala wenye uwezo wa kuwafanya nyie ubora wenu uzidi hawa wageni ambao tunao.
Tanzania tuna viongozi au watu ambao hawakusoma Private school lakini wanafanya kazi nzuri pasipo kusubiri kazi hiyo ije ifanywe na mgeni sasa kwa nini wachezaji ishindikane kutumia hicho kidogo ambacho mnapata kwa makocha wenu hata kama hamjapitia kwenye misingi ya academy.?, Jiongezeni hapo.
Nihitimishe kwa kusema wachezaji wa kigeni ikibidi waongezeke zaidi ya hawa ambao wanasajiliwa hakuna ambacho kinazuia mzawa kucheza ni nyie kuonyesha uwezo wenu na upeo wenu.
Niwatakie somo jema na hitimisho jema la miguu yenu.
SOMA ZAIDI: Fadlu Davis Na Mtihani Mzito Wa Uvumilivu Na Imani Simba