KWA SASA Yanga inahitaji pointi zote sita dhidi ya TP Mazembe katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuondoka na wachezaji wote wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo huo wa Jumapili.
Yanga inaifuata TP Mazembe kifua mbele baada ya kupata matokeo mazuri nyumbani ikiifunga mabao 3-1, huku ikiongoza kundi na tayari imefuzu kushiriki hatua ya robo fainali kwenye mashindano hayo.
Mratibu wa Yanga, Hafidh Salehe alisema ni wachezaji wanne tu ambao watakosekana kwenye msafara huo kutokana na matatizo mbalimbali, huku akithibitisha kuwa wengine wote watasafiri leo.
Saleh alisema nyota watakaokosekana kwenye msafara wa leo ni Denis Nkane, Abuutwalib Msheri, Dickson Ambundo na Bernard Morrison, huku wachezaji wengine wote wakiondoka asubuhi ya leo.
“Wachezaji wote isipokuwa wanne ndiyo watakosekana, huku wengine wa kimataifa walioitwa kwenye timu zao za taifa tukiungana nao nchini DR Congo, ambao ni Stephen Aziz Ki, Fiston Mayele, Kennedy Musonda na Djigui Diarra,” alisema mratibu huyo.
Wachezaji walioondoka leo ni makipa Eric Johora, Metacha Mnata mabeki Djuma Shaban, Kibwana Shomari, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, David Bryson.
Viungo Salum Abubakar, Khalid Aucho ambaye amejiunga na timu jana akitokea timu ya taifa ya Uganda, Zawadi Mauya, Farid Musa,Yanick Bangala, Jesus Moloko na Jesus Moloko huku washambuliaji Mayele na Musonda wakiungana nao nchini Congo.