Mabingwa Manchester City wataanza msimu wa ligi kuu ya Premier League siku ya Ijumaa, Agosti 11, dhidi ya Burnley ya Vicent Kompany, ambao wamepanda daraja – ambao ni waliongozwa na nahodha wao wa zamani Vincent Kompany.
Luton Town itacheza mechi yao ya kwanza katika ligi kuu tangu mwaka 1992 dhidi ya Brighton siku moja baadaye, huku klabu nyingine iliyopanda daraja Sheffield United wakiwakaribisha Crystal Palace.
Utawala wa Mauricio Pochettino kama meneja wa Chelsea utaanza nyumbani dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili, Agosti 13.
Manchester United wataanza msimu dhidi ya Wolves huko Old Trafford siku ya Jumatatu, Agosti 14.
Manchester City, ambao wanasherehekea kufanikiwa kushinda Kombe la Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA katika msimu wa 2022-23, sasa wanatafuta kuwa timu ya kwanza ya England kushinda mataji manne mfululizo.
Kikosi cha Pep Guardiola kimefanikiwa kushinda Ligi Kuu mara tano katika misimu mitano iliyopita.
Meneja wa Burnley, Vicent Kompany, alitumikia miaka 11 katika Manchester City na kushinda mataji manne ya ligi.
Msimu wa ligi kuu ya Premier League wa 2023-24 utamalizika siku ya Jumapili, Mei 19, 2024.
Katika taarifa yao siku ya Alhamisi, Premier League ilisema ilikuwa “ina dhamira ya kuwapa wapenzi wa soka taarifa ya angalau wiki sita kuhusu matangazo ya televisheni hadi Desemba 2023, na wiki tano kutoka Januari 24, 2024”.
Taarifa zaidi kuhusu ligi kuu Uingereza tufuatilie hapa.