Kama kuna mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga msimu huu basi ni Khalid Aucho hasa katika safu ya kiungo wa ulinzi au namba 6 mara nyingi akicheza mbele ya mabeki wanne na nyuma ya namba nane wawili wa yanga (Mudathir na Max).

Majukumu yake yamekuwa kuamua kasi ya mchezo lakini pia kuwapa yanga uhai wakiwa hawana mpira hata wakiwa na mpira ameamua mashambulizi mengi kwa kutumia uwezo wake wakupiga pasi ndefu za hatari wachezaji wanaoweza kucheza namba kama yake Yanga ni Jonas Mkude pamoja na zawadi mauya ambao wameonekana kutokuaminiwa sana na kocha Miguel Gamondi.

Kwa sifa hizo ni wazi kuwa mchezaji wa aina hii anatumika katika michezo mingi sana katika michuano yote hivo kuna mda atahitaji mbadala je mbadala wake ni upi? kutokana na tetesi ni kuwa yanga wameonesha kuitaka saini ya Yusuph Kagoma kuziba pengo hilo swali kuu sasa.

Je Yusuph Kagoma ni mbadala sahihi wa Khalid Aucho Yanga?

Kwanza tukiri kuwa kumpata kiungo mkabaji wa asili sio vyepesi simba tangu waachane na thadeo lwanga hawajapata tena wa vile Yusuph Kagoma anasifika kuwa mzuri katika ukabaji lakini pia timu inapohitaji kwenda mbele anatumika kama kiungo wa chini mchezeshaji amekuwa na mfululizo mzuri sana wa kiwango ndio maana yupo kwenye list ya tetesi

Swali ni ataimudu presha ya Yanga? nakupa jibu kwa upande wangu ni ngumu mno kumuamini kagoma moja kwa moja aichukue nafasi ya aucho kama ataondoka labda kama Miguel Gamondi ataamua kutumia viungo wa chini wawili yani namba sita wawili mmoja acheze katika mabox mawili yani (box to box ) box la timu yake na timu pinzani kwanini hivi ?

Endapo kuna makosa yatajitokeza katika uchezaji basi mpinzani atabidi akabiliane na viungo wawili wakabaji ili kuwaona mabeki wanne wa nyuma hivyo itamlazimu Gamondi atumie mfumo mmoja wapo kati ya hii hapa (4-2-3-1) (4-2-2-2) (5-2-3) tutaongelea siku nyingine michanganuo ya mifumo hiyo timu ikiwa na ikiwa haina mpira yapi ni majukumu ya viungo wawili wakabaji.

Kwakumalizia kama kuna uwezo yanga wamshikilie aucho sio vyepesi kupata mbadala wa kiungo mkabaji wa asili mwenye uwezo wa kushambulia na kuwa kiungo wa chini mchezeshaji aucho ahitaji mtu yoyote pembeni yake ili uone uwezo wake ila yanga wanamuhitaji aucho ili uone uwezo wao hasa wakiwa hawana mpira.

SOMA ZAIDI: Pamba Jiji FC Ni Mkombozi Wa Soka Na Maisha Mwanza?

Comments are closed.

Exit mobile version