IlipoishiaΒ “Fuata maelekezo yangu, kuwa makini hao Watu wana akili yaΒ ziada sana wakati mwingine Watu hawaamini kama Huyo Mzungu niΒ Binadamu, wana akili iliyozidi…unaweza kuwa umetegwa, kablaΒ ya kutoka Msibani hakuna ishara tata?” Alimpa wakati waΒ kufikria, Zola akasemaΒ
“Nilikuwa makini kuliko kawaida, hakuna aliyeniona ila wakatiΒ natoka…” Ukimya ukatawala, Mzee Dawson akamuuliza ZolaΒ
“Enhee ilikuwaje?” Zola akafikiria alipokuwa akitoka paleΒ aliparamiana na Mwanamke mmoja mzuri sana, hakutaka kulisemaΒ hilo akiamini sio ishara ya kumueleza Mzee DawsonΒ
“Sio ishara!”Β EndeleaΒ Β
“Sawa endelea kuwa makini na gari hilo” Gari hiyo ndogoΒ nyeusi iligota katika moja ya hoteli maarufu sana Mjini hapoΒ iliyoitwa Sarafina Hotel, Muda huu jamaa mwenye upara alikuwaΒ akishuka bila kuonesha wasiwasi wowote huku Zola akiwaΒ anatafuta sehemu rahisi ya kupaki Gari yake, Jamaa wa uparaΒ akaingia kwenye lifti wakati Zola akiwa amejibanza mahaliΒ anamchungulia, haraka akapandisha ngazi kuelekea juu kwaΒ spidi ambayo kila mmoja alishangaa kwa Mzee kama ZolaΒ kupandisha zile ngazi kwa spidi kubwa kama umeme, NaamΒ ilikuwa ni kawaida kwake kutokana na mafunzo aliyoyapataΒ zamani nchini Mexico na Cuba.Β
Alipofika Floo ya pili alipokelewa na ukimya, akili yakeΒ ikamwambia kuwa Jamaa wa upara atakuwa Floo ya juu yake yaaniΒ ya tatu, basi Zola kwa spidi ile ile alizidi kupandisha ngaziΒ na kuendelea kustaajabisha Watu aliopishana nao, mwisho waΒ Floo ya pili alimuona jamaa wa Upara akikata kona upande waΒ kushoto, Zola hakutaka kupoteza muda alizidi kumfuatilia iliΒ ajuwe Jamaa yule alikuwa akienda wapi, huku akili yakeΒ ikimwambia kuwa ni miongoni mwa wale waliousuka ule mpango waΒ vifo vya Robert na Bosco na hatimae kumtumia Anastanzia kamaΒ mchezo wa kuigiza ili kuficha jambo ambalo kwa asilimia kubwaΒ lilifanikiwa. Alipokata kushoto alianza kuhisi hali yaΒ tofauti, achilia mbali ukimya bali kulikuwa na milango miwiliΒ ambayo ilikuwa wazi tena ikiwa inacheza kuashilia kuwaΒ ilikuwa imeguswa sekunde chache zilizopita.Β
Zola akakunja mkono wake wa kushoto ambao alipendelea kuuitaΒ Mkono Wa Mungu, kisha akachomoka na Bastola yake yenyeΒ kiwambo maalum cha kuzuia mlio wa risasi kutoka, tayariΒ alikuwa na hisia kuwa alikuwa ameingizwa mtegoni, akachomoaΒ Ear phone masikioni baada ya kuhisi mawasiliano kati yake naΒ Mzee Dawson yalikuwa yanasuasua na hakutaka kuzungumza kwaΒ sauti kubwa, Kitendo cha Zola kuchomoa zile Ear PhoneΒ masikioni kilimpa ishara Mzee Dawson, akahisi pengine ZolaΒ yupo kwenye mtego wa kifo, haraka akachukua gari kuitafutaΒ Sarafina Hoteli ilipo, Naam! Zola alikuwa akinyata kama pakaΒ aliyekuwa akimvizia panya ili aweze kumla, alipiganisha akiliΒ yake huku macho akiwa anayaelekeza kwenye ile milango miwiliΒ iliyo waziΒ
Akauchagua mlango mmoja akaingia taratibu kisha akafungaΒ mlango bila kuruhusu sauti ya kufungwa kwa mlango huoΒ kusikika, mbele aliona kuna korido iliyo kimya sana, akawaΒ anaifuata. Alikuwa amejikunja kama duma vile huku akijuwaΒ kuwa kosa lolote atakalo lifanya linaweza kuondoa uhai wake,Β akaupita mlango wa kwanza na wa pili, akili ikamwambiaΒ aufungue mlango wa tatu, alikuwa ni mwenye hisia kali kamaΒ Mbwa wa polisi vile, alihema taratibu sana, alifundishwa kuwaΒ kuhema kwa nguvu kunaweza kusababisha shabaha kwenda tofautiΒ jambo ambalo hakutaka litokee pale, akiwa ameshikilia kitasaΒ hicho huku akivuta taratibu Zola alikutana na teke kaliΒ lililomnyumbisha na kusababisha bastola yake kuanguka chini,Β akiwa anataka kuiokota Bastola hiyo ilipigwa teke naΒ kuburuzika mita kadhaa, Ndipo Zola akajuwa sasa yupo katikaΒ hatari mno, kwa umakini akageuka taratibu kumtazamaΒ aliyempiga teke.Β
Alikutana na sura ya Malaika, ambaye yeye alimtambua kamaΒ Judith tena alikuwa katika sura bandia ambayo Zola alikuwaΒ akiijuwa. Mzee Zola akayakumbuka maneno ya polisi aliyempigiaΒ simu na kumtaarifu juu ya mauwaji ya polisi katika kituo chaΒ polisi, akautumia muda huo kuyatazama maungio ya MsichanaΒ huyo mwembamba lakini hatari sana akagundua ana ujuzi mkubwaΒ wa kareti.Β
Zola hakutaka kupoteza muda wake japo alijuwa Msichana huyoΒ ni hatari sana kwake, akakunja mguu na kutupa teke lililofikaΒ hadi kwenye mbavu za msichana huyo ambaye aliudaka mguu waΒ zola kisha akaukunja na kumsababishia Zola maumivu mkali,Β akapigwa kwenye ngoko ndipo Zola alipotoa sauti ya maumivu,Β akauvuta mguu haraka ili usivunjwe, akawa na maswali mengiΒ kichwani aliyotaka kumuuliza Msichana huyo lakini aligunduaΒ kuwa hana muda wa kupoteza hapo.Β
Akaweka mikono yake vizuri ili aweze kutupa shambulio,Β Malaika akajirusha na kutua kwenye mikono ya Mzee Zola ambayoΒ ilikuwa imekazwa, kisha akavingirika na kumpa teke la usoΒ Mzee Zola akaangukia pembeni, akamfuata na kuanza kumpigaΒ sehemu ya tumbo huku akimwambiaΒ
“Wewe ni mahiri sana kwa upelelezi lakini mwisho wa kuifanyaΒ kazi hiyo ni leo, nakuuwa Hapa ili kupeleka ujumbe kwaΒ aliyekutuma” Zola alikuwa akigugumia kwa maumivu, harakaΒ akauvuta mguu wa Malaika na kumuangusha akapata muda waΒ kujipanga upya,,, safari hii Zola hakuwa na bahati kabisa,Β Malaika aliutumia ujuzi wake wa mapigano na kumpiga kisawaΒ sawa Zola hadi akatema Damu, akamuinua na kumkaba shingoniΒ huku akiwa amemgandamiza ukutani, Zola akaitumia nguvu chacheΒ iliyobakia akampiga teke sehemu nyeti ikawa auheni kwake,Β Malaika akaanguka chini haraka akajiokota, ni kama vileΒ alikuwa amemchokoza basi Zola alikutana na Ngumi za usoΒ mfululizo hadi akachanganikiwaΒ
Akajikuta muda mchache ameanguka chini na kushindwa kuinuka,Β Malaika alipoona Zola hawezi tena kurudisha majibu yaΒ mpambano huo uliopigwa kisiri ndani ya Hoteli hiyo, akavuaΒ sura ya Bandia ndipo Zola akapata kuiona sura halisi yaΒ Mwanamke huyo.
“Naitwa Malaika! Najua huna uwezo wa kufanya chochote hapoΒ Zola sababu zimebakia sekunde chache nikupoteze, kamaΒ ulifikiria kuwa mtaweza kupambana na Mafia Gang basi huu uweΒ ujumbe kwa wajinga wenzako, Mtakufa wote endapo mtaendeleaΒ kutufuatilia” Malaika akachomoa kisu chake kutoka katikaΒ mfuko wa koti alilovaa, akamsogelea Mzee Zola akamwambiaΒ
“Kwakuwa umefanikiwa kunijuwa basi huna haki ya kuendeleaΒ kuishi” Malaika akanyanyua kisu ili amchome Zola sehemu yaΒ moyo, Ghafla alisikia mlango ukifunguliwa huku risasiΒ zikimiminwa mfululizo, akajirusha na kuanza kukimbia kwaΒ kuzikwepa hadi akazama kwenye korido, alikuwa ni Mzee DawsonΒ ndiye aliyemsaidia Zola pale vinginevyo Zola angeuawa pale.Β
“Pole Zola” alisema huku akiwa amempa mkono Zola awezeΒ kusimama, akamsaidia akasimama kisha Dawson akaiendea BastolaΒ ya Zola ambayo ilikuwa sakafuni akampatiaΒ
“Mshenzi yule alikuwa anaondoa uhai wangu na kama sio weweΒ basi mgekuja kuchukua maiti yangu hapa”Β
“Bado siamini kama msichana yule amekukalisha chini Zola!”Β
“Dawson! Niliposikia hadithi ya yule Msichana ya kuuwa polisiΒ zaidi ya 15 katika kituo cha polisi nilifikiria ni utaniΒ lakini leo nimeamini kwanini aliwashinda polisi, ana ujuzi waΒ Kareti kitu ambacho ni hatari zaidi kwetu”Β
“Oooh!! Mungu wangu, hatuna muda wa kupoteza hapa, tuondoke”Β Alisema Mzee Dawson, mara moja wakashuka hadi chini kilaΒ mmoja akaingia kwenye gari yake na kuelekea alipopafahamu.Β
Zola alikuwa na hasira sana akiwa ndani ya gari, kupigwa naΒ Malaika kulimuumiza sana lakini alifanikiwa kuijua suraΒ halisi na jina la huyo Mwanamke ambalo ni Malaika, akili yakeΒ ikamtuma aelekee kituo cha polisi, Mkono mmoja ulikuwa naΒ maumivu makali sana lakini alijikaza, alichotaka kujuwa niΒ mafaili gani yule Malaika aliyaiba ndani ya kituo cha polisi,Β akaambiwa kuwa mafaili hayo yalikuwa ya kesi mojaΒ iliyoshikiliwa na kitengo cha Ikulu.Β
Kesi hiyo ilimuhusu jamaa mmoja aliyeitwa Jamaal, ambayeΒ alikamatwa siku moja baada ya tukio la kuuawa kwa Makam waΒ Rais kutokea, Historia ya jamaa huyo ilimuelezea kuwa ni MtuΒ aliyepitia mafunzo maalum ya kijeshi ya ulengaji wa shabahaΒ ya masafa marefu na upiganaji, alikamatwa katika uwanja waΒ ndege baada ya msako mkali uliokuwa ukiendelea.
Baada ya kumnasa walikuta Bunduki na risasi ambayo ilitumikaΒ kumuuwa makam wa Rais, moja kwa moja alishtakiwa kwa kosaΒ hilo na kufungwa kwa siri katika gereza moja la siri sana,Β Jamaal alikutwa na vitambulisho vilivyomuonesha kuwa anaΒ Uraia wa Nchi nane ikiwemo Marekani na Ukraine jambo ambaloΒ liliwashangaza sana lakini Jamaal alizungumza lugha nyingiΒ vizuri sana japo alikuwa na asili ya Somalia. Pia taarifaΒ ilienda mbali zaidi na kusema kuwa Jamaal alikutwa naΒ vitambulisho vya kijeshi vilivyoonesha kuwa aliwahiΒ kulitumikia jeshi la Israel na Palestina ndani ya miakaΒ miwili,Β
Zola alikaa chini na kujishika kichwa chake kisha akaulizaΒ
“Kwasasa Jamaal anashikiliwa gereza gani?” Swali hiliΒ lilimfanya polisi aliyekuwa akimueleza Zola akae kimya kidogoΒ kisha akasemaΒ
“Gereza lipo Ikulu ya Nchi, sisi hatuhusiki tena na kesi hiyoΒ Zola” Zola akauliza tenaΒ
“Kwanini mafaili ya kesi bado yalikuwa hapa?”Β
“Kwasababu kesi ilianzia hapa lakini cha kushangaza baada yaΒ kukamatwa tuliondolewa katika kesi hiyo”Β
“Nani alitoa oda ya Nyie kuacha hii kesi na ikaenda sehemuΒ nyingine wakati nyie ndio mnakazi hiyo?”Β
“Aliyetoa oda ni Rais wa Nchi” Zola aliondoka baada ya kupataΒ majibu yaliyochanganya akili yake kisha akawasiliana na MzeeΒ Dawson wakapanga kukutana katika makazi ya siri ya Zola,Β Usiku Dawson alienda kuonana na Zola, kama kawaida yaoΒ waligida pombe ili maongezi yaanzeΒ
“Enhee umegundua nini Zola?” Aliuliza DawsonΒ
“Mafaili yaliyobiwa katika kituo cha polisi yalikuwa ya kesiΒ ya Mtu anayedaiwa kuwa alihusika kumuuwa Makam wa Rais”Β Alisema ZolaΒ
“Unasemaje? Ina maana polisi wanajuwa ni nani alihusika?”Β
“Sio polisi pekee hata Mkuu wako wa Nchi ambaye anakupa kaziΒ ya kulisaka kundi la Mafia Gang anajuwa na kibaya zaidiΒ ametoa amri ya jeshi la polisi kuiacha kazi hiyo” Mzee DawsonΒ alionekana kushangaa sanaΒ
“Inawezekanaje Zola?”
“Hiyo ndio hali halisi ndio maana nimekuita hapa iliΒ tuzungumze, nahisia mbaya juu ya Mkuu wa Nchi lakini sitakiΒ kujiaminisha chochote”Β
“Unataka kusema Mkuu wa Nchi kuna kitu anakificha hapa?” WoteΒ waliacha kunywa pombe wakazama katika maongezi yaoΒ
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SITAΒ USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza HapaΒ
Β Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Β Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx
8 Comments
Lit
βοΈβοΈ
Naona inaelekea ukingoni
Nimekipenda kitabu hiki,
Nikama macho yanafumbuka π€π€π€
Iko poa sanaaa
Fantastic
Nimekipenda kitabu hiki,
Nikama macho yanafumbuka π€π€π€
Nimeipenda mno kiongoz ongera na asante ongeza bidii