Unaweza ukawa ni miongoni mwa wale ambao wanakua wanajiuliza ni kiasi gani ambacho thamani ya mashindano haya ya CAF iko nayo haswa kwa nafasi ambayo utakua umefikia katika kila hatua ambayo utakua umeingia kwenye michuano hii ya klabu bingwa Afrika ambapo kwa Tanzania tunawakilishwa na klabu za Simba na Yanga.
Wakati huu ambao wananchi wakiwa katika kilele cha furaha baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi ni wazi kuwa mashabiki wao watakua wanajiuliza kuhusu kiasi gani watakuwa wamevuna mpaka sasa.
Bila kusahau wekundu wa msimbazi ambao wana kazi nzito ya kuhakikisha kuwa wanafuzu katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy katika uwanja wa Mkapa moja kati ya mechi ambayo itakua ya kufa na kupona kwa klabu ya Simba.
Muhimu zaidi unachopaswa kufahamu ni kuwa kila timu inapewa pesa ya nafasi iliyofikia na sio kila hatua, ikiwa timu itaomba pesa za usafiri, malazi, vyakula, n.k. Mashindano yakiisha watalipwa kiasi kilichobakia baada ya kutoa fedha walizopewa.
US$ 1 = shilingi 2,545 Tshs
BINGWA:
US$ 4 million
Shilingi bilioni 10 na milioni 180
MSHINDI WA PILI:
US$ 2 million
Shilingi bilioni 5 na milioni 90
KILA TIMU ITAYOISHIA NUSU FAINALI:
US$ 1.2 million
Shilingi bilioni 3 na milioni 54
KILA TIMU ITAYOISHIA ROBO FAINALI:
US$ 900,000
Shilingi bilioni 2 na milioni 290
KILA TIMU ITAYOISHIA HATUA YA MAKUNDI:
US$ 700,000
Shilingi bilioni 1 na milioni 781
Bila shaka umeona kiasi hicho cha pesa kwa kila hatua kilivyo na ndio wakati ambao viongozi wat imu nao huandaa posho za uhakika ili kuwapa nguvu wachezaji wapambane na kufuzu hatua za mbele yake ili kuendelea kuvuna pesa hizo kutoka katika Shirikisho la soka Afrika katika michuano yao ya ngazi hii ya vilabu kwa ligi ya mabingwa Afrika.
SOMA ZAIDI: Yanga Mmeniziba Mdomo, Mpira Ni Uwekezaji Sio Uchawi
2 Comments
Pingback: Kwenye Dua Zenu Msiombee Kukutana Na Petro Atletico - Kijiweni
Pingback: Droo Ya Robo Fainali Ligi Ya Mabingwa Afrika Itavyofanyika - Kijiweni