Kuelekea michuano ya Ulaya, Euro 2024 ngazi ya timu za taifa, Shirikisho la mpira wa miguu bara la Ulaya (UEFA) limetangaza kuja na mpira utakaotumika katika michuano hiyo ambao utakua na uwezo wa kugundua mchezaji atakaekua amezidi (offside) au alieshika mpira haraka zaidi kuliko VAR.
Mpira huo utakaojulikana kama Fussballiebe umetengenezwa na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Adidas na utakua na teknolojia ya kisasa zaidi ya ugunduzi wa offside hivyo kuwarahisishia waamuzi wa mchezo kwa haraka zaidi.
Adidas ni shirika la kimataifa la Ujerumani, lililoanzishwa na lenye makao yake makuu huko Herzogenaurach, Bavaria, ambalo husanifu na kutengeneza viatu, nguo na vifaa. Ni mtengenezaji mkubwa zaidi wa nguo za michezo huko Uropa, kampuni ya Adidas ni ya pili kwa ukubwa ulimwenguni, baada ya Nike
Teknolojia hiyo itasaidia kuonesha kuwa endapo mpira umeshikwa lakini waamuzi watajiridhisha zaidi kwa kuangalia katika kamera za marudio (VAR) ili kujiridhisha kama mpira umeshikwa.
Kumekua na changamoto kubwa sana kutoka kwa mameneja wa vilabu mbalimbali katika ligi kuu ya Uingereza ambao wamekua wakilalamika kuhusu video za usaidizi kwa waamuzi (VAR) na kudai kuwa zinawaumiza katika baadhi ya maamuzi yake hali iliyopelekea kufikiria mfumo mpya wa mpira utakaogundua kuzidi katika mchezo (offside) kwa msimu ujao wa ligi.
Michuano ya Euro kwa mwaka 2024 itafanyika nchini Ujerumani kuanzia tarehe 14 ya mwezi wa 6 mpaka tarehe 14 ya mwezi wa saba.
Kwa taarifa zetu zaidi, soma hapa.