Ukiachilia mbali matokeo na utamu wa ligi kuu Tanzania Bara lakini kumekua na purukushani za aina yake kati ya Azam Fc na mshambulaiji wao Prince Dube ambaye amekua akizungumziwa sana katika mitandao ya kijamii na hili ni baada ya kuandika barua ya kuomba kuondoka katika kikosi cha Azam.
Kama ni kweli, kitu cha kwanza anachotakiwa kujiuliza Dube ni Je, ni kitu gani ambacho uongozi wa Azam FC haujamtimizia au haujakitimiza kwa timu nzima, hadi ashindwe kupambana na kutimiza hiko kitu anachokitaka.
Yeye binafsi ni kwa asilimia ngapi ametimiza majukumu yake uwanjani, kwa ajili ya kuisaidia Azam FC kutwaa mataji? Ameondoka ghafla katikati ya msimu, wakati wachezaji wenzake wakiendelea kuvuja jasho uwanjani, kwa ajili ya kutimiza malengo ya klabu, Je, haoni hii ni kuwavunjia heshima na kuwadharau wachezaji wenzake kuwa hawawezi kupata taji lolote!?
Akiwa kama mshambuliaji kinara kwa misimu minne hii, ameshajiuliza ni kwa kiasi gani ameiathiri Azam FC kwa kutokuwepo kwake uwanjani kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo amekuwa akiyapata!? Azam ilivyokuwa klabu ya mfano na yenye uungwana, imekuwa ikizingatia afya za wachezaji na kutoa kipaumbele cha kutibiwa popote pale tatizo linaposhindwa kutatuliwa hapa nchini, kitu ambacho Dube amefanyiwa na mabosi wake ambao hivi sasa anadaiwa kuwaponda.
Mbali na mchezaji kutibiwa nje ya nchi, pia hupewa stahiki zake za kila za mwezi (full Salary) na bonasi (full bonus) pale timu inapopata ushindi! hivi ndio namna Azam FC imekuwa ikiwajali wachezaji wake. Ndio Dube anataka kuondoka Azam FC! Lakini akumbuke fadhila na namna Azam ilivyomvumilia kwa kipindi chote kizuri na kibaya, kuliko kuanza kutoa shutuma hewa kwa uongozi ambao ulikuwa ukimpigania kupata atakacho kwa kipindi chote.
Uongozi wa Azam FC umeshamuwashia taa ya kijani kuondoka kama anavyotaka, ila anatakiwa kutimiza masharti ya mkataba aliousaini msimu huu, kuwa ili aweze kuwa huru kujiunga na klabu yoyote basi atatakiwa kulipa au kulipiwa na klabu inayomtaka USD 300,000 (release clause). Namalizia kwa kusema, mabosi wa Azam FC wanafanya kazi kubwa sana ya kujenga timu na soka la Tanzania kwa ujumla, muda si mrefu mtakula matunda yaliyotokana na jitihada zenu.
Kupitia sauti yake ambayo inazagaa mtandaoni anapata shaka juu ya majeraha yake tangu afike Azam FC anadhani kuna kitu kimejificha nyuma yake pale anaposema “Kitu kingine unayoweza kuiona ani ninayoiona ni sula la majeraha yangu, ukiangalia majeraha yangu nikiwa Afrika Kusini au Zimbabwe utaona nilikuwa nacheza mechi zote za msimu mzima, nilipokuja hapa sina muendelezo nacheza mechi chache nakuwa nje nacheza tena mambo yanapoanza kuwa vizuri narudi tena nje, wakati napojaribu kukaa chini nakufikiria naona kuna kitu nyuma ambacho siwezi kukiona kwahiyo nafikiri nikipata changamoto nyingine, mazingira tofauti huwezi kujua labda mambo yatabadilika, kwakuwa mimi ni mchezaji ambaye anataka kucheza kila mechi, kuwa tayari kwajili ya timu, sasa vitu kama hivyo vikiendelea kutokea unaona hapana hapana hapa sio mahali pakuendelea kuwepo, hivyoo”
SOMA ZAIDI: Kuondoka Kwa Benchikha Tuitegemee Simba Hii Yenye Matola
2 Comments
Pingback: Soka La Wanawake Ndio Ukombozi Wa Maisha Kwa Mabinti - Kijiweni
Pingback: Sitegemei Mapya Kwa Benchikha Kama Wachezaji Ni Hawa - Kijiweni