Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza ongezeko la asilimia 40 la pesa kwa mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies (Afcon) Ivory Coast 2023.
Kufuatia ongezeko hilo la 40% ni wazi kuwa Mshindi wa TotalEnergies Afcon Ivory Coast 2023 atapokea USD 7, 000 000 huku mshindi wa Pili wa TotalEnergies Afcon Ivory Coast 2023 sasa atapata USD 4, 000 000.
Kila mmoja wa Washindi wawili wa Nusu Fainali atapata USD 2, 500, 000 na kila mmoja kati ya washindi wanne wa Robo Fainali, USD 1,300 000.
Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe alisema: “CAF imepata maendeleo makubwa katika miaka miwili iliyopita katika kuongeza pesa za Afcon na mashindano yake mengine yote makubwa.
” Tumeongeza Pesa ya mshindi wa Afcon hadi USD 7 ,000, 000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 kutoka Pesa ya awali ya Afcon,”
“Nina imani kuwa sehemu ya pesa ya Tuzo itachangia katika kuendeleza soka na pia kuwanufaisha wadau wote wa soka, pamoja na kusaidia vyama vyetu vya wanachama katika tawala zao.”, amesema.
Michuano hiyo itafanyika kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 nchini Cote d’Ivoire. Ambapo timu ya Taifa ya Tanzania ,Taifa Stars imepangwa kundi F na timu za DR Congo, Morocco na Zambia.
Endelea kufuatilia zaidi kuhusu taarifa mbalimbali za AFCON kwa kugusa hapa.