Ndugu Mhariri leo naomba kuandika kuhusu jambo ambalo wengi hawalizungumzi haswa kuhusu beki wetu Inonga.
Nimefuatilia sana barua zako ambazo umekua ukizichapisha hapa Kijiweni na nimeona nishiriki kwa kuandika kuhusu jambo hili ambalo lipo ndani ya uongozi wa klabu yangu pendwa yenye mitaa yake ya Msimbazi.
Kumekua na taarifa mbalimbali kuhusu maamuzi magumu ambayo viongozi wanafikiria kuyafanya katika kuhakikisha kuwa kunakua na maboresho ndani ya klabu ya Simba haswa katika nafasi ya uongozi pamoja na katika kikosi chetu yaani nikiamaanisha wachezaji na niseme tu kuwa katika yale maamuzi magumu ambayo viongozi wanapaswa kuyafanya wakati huu bila kufikiria mara mbili mbili ni pamoja na kumuuza Henock Inonga.
Mhariri, sio kwamba namchukia beki huyu walaa ila tu ni kwa manufa yetu kwani nimemtazama katika mechi kadhaa ambazo amekua akicheza toka atoke katika michuano ya mataifa barani Afrika ambapo walishika nafasi ya 4.
Inonga wa sasa hivi akiwa uwanjani sio yule wa misimu miwili ya nyuma, huioni seriousness yake wala kujutia makosa yanayojirudia rudia. Kuna namna kama moyo wake haupo tena kuipambania Simba na ni kama anafikiria kuondoka klabuni.
Inawezekana yupo kimwili, lakini sio kiakili, hata uchezaji wake hajitumia kama zamani, mara nyingi anaonekana anatembea na hata hakabi kwa nguvu ile aliyokuja nayo Simba. Kwenye mitandao yake ya kijamii, Inonga ameweka emoji za kulia na kuaga huku akiandika ‘bye’ (kwa heri/kwa herini) bila kufafanua.
Kwa taswira hiyo hakuna nafasi ya kumshawishi kubaki bali kumfungulia milango atafute changamoto mpya. Klabu itapoteza beki mkubwa, lakini itaingiza pesa ndefu ya kutafuta Inonga mwingine wa daraja la juu. Wapo wengi sokoni.
Nakutakia majukumu mema na ahsante kwa kuisoma barua hii.
SOMA ZAIDI: Barua Kwako Mo Dewji Rais Wa Heshima Simba Sc
14 Comments
Wamuuze inonga af watuletee wachezaj kama kina Freddie na jobe wengine tena🚮🚮
Tuungane tuupinge uongozi uliopo kwanz tuache kuwaandama wachezaji wetu😑👍
Wamuuze tu maana ,n dhahiri roho na akili yake havipo kuipambania ssc bali n mwili tu ndyo upo, ni vyema viongozi wabargain vzury kuweza kutengeneza fedha nzury ya kuboreshea kikosi chetu kwa sasa.
Simba kaikuta na hata akiondoka simba itabaki kuwa ni simba walikuwepo mabeki zidi yake nahawpo yeye nani?????
Namuelewa sana muandishi wa barua hii na ana hoja yamsingi asikilizwe NB: naunga mkono hoja 📌
Me naona nivizuri viongozi walione hili kwani kuwa na mchezaji ambayehana uchungu wa timu huyo hawezi kuwa chachu ya maendeleo kwa timu yetu ya Simba
Abakii tuu maan hata akiondka bado simbaa ni mbovuuu
Siyo kwamba inonga hana moyo na timu yake. Huwenda kuna changamoto zinaendelea kwenye klabu ya simba ndo mana inakuwa hivyo. Kama mtaona hawafai wamlete hata yanga tu
Mwache aondoke
Mi nadhani pia ni wakati wa kufikiria kupata wachezaji wapya ikiwemo washambuliaji pamoja na mabeki
Sisi kilio chetu hasa ni wafungaji inonga asiuzwe auzwe jobe na pacha wake tuletewe qualified striker
Tunaweza kusema hivyo,lakini tatizo kubwa lipo katika uongozi especially scouting,,hivi unadhani wachezaji wakiwa wazuri na mahiri utayaona makosa au mapungufu ya viongozi? Jibu ni hapana,
Umaridadi unaficha umasikini,kikubwa viongozi wafanye usajili mzuri,mambo yataenda sawa ikiwa team inafny vzr na hakuna mtu atapeleka lawama kwa viongozi hata ikiwa kwa namna Moja wanakosea pahala,Bali itakuwa kuwashauri tu na team itaendelea mbele.
Pingback: Njia Ipi Bora Kwa Mzize? Aende AZAM au Abakie Yanga Au Ulaya? - Kijiweni
Pingback: Barua Kwako Mwamuzi Arajiga Kuelekea Yanga vs Simba - Kijiweni
Pingback: Aheri Ya Inonga Mgonjwa Kuliko Mabeki Wengine Simba Wazima - Kijiweni