Najua mnafahamu namna ambavyo mchezo dhidi ya Jwaneng ulivyo na umuhimu mkubwa zaidi kwenu na klabu ya simba kwa ujumla bila kusahau kwa soka la Tanzania ambalo tumeshuhudia tayari ndugu zenu Yanga wakiwa wamefuzu hatua ya robo fainali.
Kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Jwaneng Galaxy mnapaswa kukumbuka katika yale maumivu yaliyoachwa ndani ya mioyo ya wana Simba kwenye dimba la Benjami Mkapa ambapo klabu ya Simba ilikuwa ikihitaji ushindi wowote ama sare ili iweze kusogea hatua inayofuata ila kwa bahati mbaya Jwaneng walitibua sherehe zile.
Jina la mchezaji Gape Edwin Mohutsiwa litakumbukwa zaidi pale LUPASO alipozamisha jahazi la Simba kwa kupachika bao la 3 na kuufanya mchezo ule kumalizika kwa jumla ya mabao 3-1 na kulevo Aggregate ya mabao 3-3.
Mimi naikumbuka kabisa ilikuwa dakika ya 86′ ambapo Mohutsiwa alipopiga mpira wa kichwa uliojaa kambani na kumshinda mlinda mlango Aishi Salum Manula kisha game kumalizika kwa Jwaneng Galaxy kuibuka na ushindi ule.
Naomba niwaambie kuwa siku ya Jumamosi kwenye dimba la Mkapa mnatakiwa kuonsha namna gani nyie ni Wenye Nchi kama ambavyo mmekua mkijinasabaisha katika mambo yenu na nategemea kuwaona mkiwa tofauti na ari kubwa zaidi ya kuitaka kuimaliza mechi mapema.
Wako katika ujenzi wa tasnia ya michezo
Mwanamichezo.
SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Wa Simba Kwenda Kwa Yanga
1 Comment
Pingback: Karabaka Ni Dhahabu Iliyopo Simba Isiyotumika Vyema - Kijiweni