MZOZO wa Barcelona na LaLiga kuhusu Gavi umeongezeka huku tovuti ya ligi hiyo ikimwondoa kiungo huyo kwenye kikosi cha Barcelona.
Inakuja siku chache baada ya mzozo wa usajili kupigwa mahakamani huku klabu hiyo ya Catalan ikipoteza azma ya kumsajili nyota huyo.
Inahofiwa kwamba Gavi anaweza kuwa mchezaji huru ikiwa Barcelona hawatashughulikia masuala yao ya kifedha.
LaLiga wamekataa kusajili mkataba mpya wa kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 baada ya Barca kuonekana kuwa wamevuka kiwango cha matumizi yao hadi mwisho wa msimu.
Klabu hiyo imejaribu mara kadhaa kutengua hukumu hii.
Sasa ligi hiyo imemuondoa Gavi kwenye orodha ya kikosi cha Barca kwenye tovuti yao katika ishara nyingine ya mzozo unaozidi kuwa mkubwa.
Gavi bado anaweza kuichezea Barcelona lakini yuko chini ya kandarasi ya vijana hadi suala hilo litatuliwe
Inafungua uwezekano wa klabu ya Uhispania uwezekano wa kulazimika kumsajili chipukizi huyo na kufungua mlango kwa vilabu vingine vinavyojaribu kumnunua kama mchezaji huru.
Klabu ya Nou Camp ilifikiri kuondoka kwa Memphis Depay na Gerard Pique kungewaruhusu kumsajili Gavi.
Lakini sasa wanatakiwa kuchunguza chaguo la kuruhusu nyota zaidi kuondoka ili kusawazisha vitabu.