Moja kati ya mechi kubwa hii leo ligi kuu ya Uingereza ni mchezo utakaowakutanisha Arsenal dhidi ya Liverpool katika dimba la Emirates ambao ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya Arsenal.Washika mitutu wa London wanaingia katika mchezo huu wakiwa nafasi ya 3 na alama zao 46 katika michezo 22 waliyoshinda mpaka sasa wakiwa nyuma kwa alama 5 kutoka kwa vinara wa ligi Liverpool.
Liverpool chini ya Jurgen Klopp wanaingia katika mchezo huu wakiwa na michezo 11 bila kupoteza katika michuano yote waliyoshiriki wakipata ushindi katika michezo 8 na kupata sare 3.
TAKWIMU
Huu ni mchezo muhimu zaidi kwa timu zote 2 kwani Arsenal anataka kupunguza gape la point huku Liverpool yeye akitaka kuongeza alama zaidi aendelee kujikita kileleni.
- Katika michezo takribani 241, Liverpool anaongoza kwa ushindi dhidi ya Arsenal akishinda michezo 95 na kuwa mbabe zaidi kwa Arsenal aliyeshinda michezo 82 huku michezo 64 ikienda sare.
- Mchezo wa mwisho kukutana ulikua mchezo wa FA ambao Liverpool waishinda mabao 2:0 na kumtoa katika michuano hiyo.
- Kati ya michezo 7 ya mwisho katika uwanja wa nyumbani Arsenal kashinda michezo 6 na kupoteza mmoja dhidi ya Westham mwishoni mwa mwaka jana.
- Liverpool wanaingiakatika mchezo huu wakiwa na rekodi ya kushinda michezo 4 mfululizo ya ligi akiwa ugenini huku wakiwa hawajafungwa katika michezo 7 wakishinda 4 na kupata sare 3.
TUNABETIJE?
- Liverpool anashinda
- Kutakua na magoli zaidi ya 3 (Total Goals Over 2.5)
- Kutakua na kufungana (Both Team to Score-YES)
SOMA ZAIDI: Nini maana ya player specials katika betting?