Tarehe 23 ya mwezi wa 7 mwaka 2018 majira ya saa 2 za aubuhi yaani mapema kabisa mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji Mo kupitia mtandao wa X ambao kipindi hiko ulikua ukifahamika kama Twitter aliweza kuchapisha ujumbe wake ambao kwa namna moja au nyingine ulichukuliwa kitofauti na mashabiki wa soka wa Tanzania kumbuka ni miaka sasa imepita tangu andiko hilo.
Aliandika “Tunahitaji Yanga imara ambayo inaweza kushindana na Simba.Tunahitaji Yanga imara kwa ajili ya timu bora ya Taifa Stars.Ninawaombea Yanga waweze kupita katika kipindi hiki kigumu kwao, wanapaswa watulie na waungane upya” baada ya miaka hiyo ni wazi tunawaona Yanga wakifuzu hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Afrika.
Naweza kusema kauli aliyoitoa Meneja Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba ni sahihi kabisa lakini ameshindwa kujua ni wakati gani wa kuitoa kauli hiyo kama ulikua hujui tu nimnukuu kile ambacho ametoa na anasema kufuzu kwa Yanga katika hatua ya robo fainali anaepaswa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba Mohammed Dewji na wa pili Club ya Simba.
“Wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika, wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua”
“Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri, kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi, huu ndio ukweli ambao utadumu milele”
Kila mmoja atakua na lake na kuzungumza vile ambavyo anajiskia lakini alichosema Ahmed ni sawa kabisa kwani kupitia kauli ya Mo Dewji miaka 6 baadae tumekuja kuiona yanga ambayo imekua bora sana na ikiwa na wachezaji ambao ni hatari lakini kubwa zaidi ni kuondoka katika kipindi kigumu ambacho walikua wakikipitia na kupata mfadhili ambaye ameipeleka mbali klabu hiyo.
SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Wa Simba Kwenda Kwa Yanga
1 Comment
Pingback: Yanga Sc Kutinga Robo Fainali Imekuwa Nongwa? - Kijiweni