Ilipoishiaย “Fuata maelekezo yangu, kuwa makini hao Watu wana akili yaย ziada sana wakati mwingine Watu hawaamini kama Huyo Mzungu niย Binadamu, wana akili iliyozidi…unaweza kuwa umetegwa, kablaย ya kutoka Msibani hakuna ishara tata?” Alimpa wakati waย kufikria, Zola akasemaย
“Nilikuwa makini kuliko kawaida, hakuna aliyeniona ila wakatiย natoka…” Ukimya ukatawala, Mzee Dawson akamuuliza Zolaย
“Enhee ilikuwaje?” Zola akafikiria alipokuwa akitoka paleย aliparamiana na Mwanamke mmoja mzuri sana, hakutaka kulisemaย hilo akiamini sio ishara ya kumueleza Mzee Dawsonย
“Sio ishara!”ย Endeleaย ย
“Sawa endelea kuwa makini na gari hilo” Gari hiyo ndogoย nyeusi iligota katika moja ya hoteli maarufu sana Mjini hapoย iliyoitwa Sarafina Hotel, Muda huu jamaa mwenye upara alikuwaย akishuka bila kuonesha wasiwasi wowote huku Zola akiwaย anatafuta sehemu rahisi ya kupaki Gari yake, Jamaa wa uparaย akaingia kwenye lifti wakati Zola akiwa amejibanza mahaliย anamchungulia, haraka akapandisha ngazi kuelekea juu kwaย spidi ambayo kila mmoja alishangaa kwa Mzee kama Zolaย kupandisha zile ngazi kwa spidi kubwa kama umeme, Naamย ilikuwa ni kawaida kwake kutokana na mafunzo aliyoyapataย zamani nchini Mexico na Cuba.ย
Alipofika Floo ya pili alipokelewa na ukimya, akili yakeย ikamwambia kuwa Jamaa wa upara atakuwa Floo ya juu yake yaaniย ya tatu, basi Zola kwa spidi ile ile alizidi kupandisha ngaziย na kuendelea kustaajabisha Watu aliopishana nao, mwisho waย Floo ya pili alimuona jamaa wa Upara akikata kona upande waย kushoto, Zola hakutaka kupoteza muda alizidi kumfuatilia iliย ajuwe Jamaa yule alikuwa akienda wapi, huku akili yakeย ikimwambia kuwa ni miongoni mwa wale waliousuka ule mpango waย vifo vya Robert na Bosco na hatimae kumtumia Anastanzia kamaย mchezo wa kuigiza ili kuficha jambo ambalo kwa asilimia kubwaย lilifanikiwa. Alipokata kushoto alianza kuhisi hali yaย tofauti, achilia mbali ukimya bali kulikuwa na milango miwiliย ambayo ilikuwa wazi tena ikiwa inacheza kuashilia kuwaย ilikuwa imeguswa sekunde chache zilizopita.ย
Zola akakunja mkono wake wa kushoto ambao alipendelea kuuitaย Mkono Wa Mungu, kisha akachomoka na Bastola yake yenyeย kiwambo maalum cha kuzuia mlio wa risasi kutoka, tayariย alikuwa na hisia kuwa alikuwa ameingizwa mtegoni, akachomoaย Ear phone masikioni baada ya kuhisi mawasiliano kati yake naย Mzee Dawson yalikuwa yanasuasua na hakutaka kuzungumza kwaย sauti kubwa, Kitendo cha Zola kuchomoa zile Ear Phoneย masikioni kilimpa ishara Mzee Dawson, akahisi pengine Zolaย yupo kwenye mtego wa kifo, haraka akachukua gari kuitafutaย Sarafina Hoteli ilipo, Naam! Zola alikuwa akinyata kama pakaย aliyekuwa akimvizia panya ili aweze kumla, alipiganisha akiliย yake huku macho akiwa anayaelekeza kwenye ile milango miwiliย iliyo waziย
Akauchagua mlango mmoja akaingia taratibu kisha akafungaย mlango bila kuruhusu sauti ya kufungwa kwa mlango huoย kusikika, mbele aliona kuna korido iliyo kimya sana, akawaย anaifuata. Alikuwa amejikunja kama duma vile huku akijuwaย kuwa kosa lolote atakalo lifanya linaweza kuondoa uhai wake,ย akaupita mlango wa kwanza na wa pili, akili ikamwambiaย aufungue mlango wa tatu, alikuwa ni mwenye hisia kali kamaย Mbwa wa polisi vile, alihema taratibu sana, alifundishwa kuwaย kuhema kwa nguvu kunaweza kusababisha shabaha kwenda tofautiย jambo ambalo hakutaka litokee pale, akiwa ameshikilia kitasaย hicho huku akivuta taratibu Zola alikutana na teke kaliย lililomnyumbisha na kusababisha bastola yake kuanguka chini,ย akiwa anataka kuiokota Bastola hiyo ilipigwa teke naย kuburuzika mita kadhaa, Ndipo Zola akajuwa sasa yupo katikaย hatari mno, kwa umakini akageuka taratibu kumtazamaย aliyempiga teke.ย
Alikutana na sura ya Malaika, ambaye yeye alimtambua kamaย Judith tena alikuwa katika sura bandia ambayo Zola alikuwaย akiijuwa. Mzee Zola akayakumbuka maneno ya polisi aliyempigiaย simu na kumtaarifu juu ya mauwaji ya polisi katika kituo chaย polisi, akautumia muda huo kuyatazama maungio ya Msichanaย huyo mwembamba lakini hatari sana akagundua ana ujuzi mkubwaย wa kareti.ย
Zola hakutaka kupoteza muda wake japo alijuwa Msichana huyoย ni hatari sana kwake, akakunja mguu na kutupa teke lililofikaย hadi kwenye mbavu za msichana huyo ambaye aliudaka mguu waย zola kisha akaukunja na kumsababishia Zola maumivu mkali,ย akapigwa kwenye ngoko ndipo Zola alipotoa sauti ya maumivu,ย akauvuta mguu haraka ili usivunjwe, akawa na maswali mengiย kichwani aliyotaka kumuuliza Msichana huyo lakini aligunduaย kuwa hana muda wa kupoteza hapo.ย
Akaweka mikono yake vizuri ili aweze kutupa shambulio,ย Malaika akajirusha na kutua kwenye mikono ya Mzee Zola ambayoย ilikuwa imekazwa, kisha akavingirika na kumpa teke la usoย Mzee Zola akaangukia pembeni, akamfuata na kuanza kumpigaย sehemu ya tumbo huku akimwambiaย
“Wewe ni mahiri sana kwa upelelezi lakini mwisho wa kuifanyaย kazi hiyo ni leo, nakuuwa Hapa ili kupeleka ujumbe kwaย aliyekutuma” Zola alikuwa akigugumia kwa maumivu, harakaย akauvuta mguu wa Malaika na kumuangusha akapata muda waย kujipanga upya,,, safari hii Zola hakuwa na bahati kabisa,ย Malaika aliutumia ujuzi wake wa mapigano na kumpiga kisawaย sawa Zola hadi akatema Damu, akamuinua na kumkaba shingoniย huku akiwa amemgandamiza ukutani, Zola akaitumia nguvu chacheย iliyobakia akampiga teke sehemu nyeti ikawa auheni kwake,ย Malaika akaanguka chini haraka akajiokota, ni kama vileย alikuwa amemchokoza basi Zola alikutana na Ngumi za usoย mfululizo hadi akachanganikiwaย
Akajikuta muda mchache ameanguka chini na kushindwa kuinuka,ย Malaika alipoona Zola hawezi tena kurudisha majibu yaย mpambano huo uliopigwa kisiri ndani ya Hoteli hiyo, akavuaย sura ya Bandia ndipo Zola akapata kuiona sura halisi yaย Mwanamke huyo.
“Naitwa Malaika! Najua huna uwezo wa kufanya chochote hapoย Zola sababu zimebakia sekunde chache nikupoteze, kamaย ulifikiria kuwa mtaweza kupambana na Mafia Gang basi huu uweย ujumbe kwa wajinga wenzako, Mtakufa wote endapo mtaendeleaย kutufuatilia” Malaika akachomoa kisu chake kutoka katikaย mfuko wa koti alilovaa, akamsogelea Mzee Zola akamwambiaย
“Kwakuwa umefanikiwa kunijuwa basi huna haki ya kuendeleaย kuishi” Malaika akanyanyua kisu ili amchome Zola sehemu yaย moyo, Ghafla alisikia mlango ukifunguliwa huku risasiย zikimiminwa mfululizo, akajirusha na kuanza kukimbia kwaย kuzikwepa hadi akazama kwenye korido, alikuwa ni Mzee Dawsonย ndiye aliyemsaidia Zola pale vinginevyo Zola angeuawa pale.ย
“Pole Zola” alisema huku akiwa amempa mkono Zola awezeย kusimama, akamsaidia akasimama kisha Dawson akaiendea Bastolaย ya Zola ambayo ilikuwa sakafuni akampatiaย
“Mshenzi yule alikuwa anaondoa uhai wangu na kama sio weweย basi mgekuja kuchukua maiti yangu hapa”ย
“Bado siamini kama msichana yule amekukalisha chini Zola!”ย
“Dawson! Niliposikia hadithi ya yule Msichana ya kuuwa polisiย zaidi ya 15 katika kituo cha polisi nilifikiria ni utaniย lakini leo nimeamini kwanini aliwashinda polisi, ana ujuzi waย Kareti kitu ambacho ni hatari zaidi kwetu”ย
“Oooh!! Mungu wangu, hatuna muda wa kupoteza hapa, tuondoke”ย Alisema Mzee Dawson, mara moja wakashuka hadi chini kilaย mmoja akaingia kwenye gari yake na kuelekea alipopafahamu.ย
Zola alikuwa na hasira sana akiwa ndani ya gari, kupigwa naย Malaika kulimuumiza sana lakini alifanikiwa kuijua suraย halisi na jina la huyo Mwanamke ambalo ni Malaika, akili yakeย ikamtuma aelekee kituo cha polisi, Mkono mmoja ulikuwa naย maumivu makali sana lakini alijikaza, alichotaka kujuwa niย mafaili gani yule Malaika aliyaiba ndani ya kituo cha polisi,ย akaambiwa kuwa mafaili hayo yalikuwa ya kesi mojaย iliyoshikiliwa na kitengo cha Ikulu.ย
Kesi hiyo ilimuhusu jamaa mmoja aliyeitwa Jamaal, ambayeย alikamatwa siku moja baada ya tukio la kuuawa kwa Makam waย Rais kutokea, Historia ya jamaa huyo ilimuelezea kuwa ni Mtuย aliyepitia mafunzo maalum ya kijeshi ya ulengaji wa shabahaย ya masafa marefu na upiganaji, alikamatwa katika uwanja waย ndege baada ya msako mkali uliokuwa ukiendelea.
Baada ya kumnasa walikuta Bunduki na risasi ambayo ilitumikaย kumuuwa makam wa Rais, moja kwa moja alishtakiwa kwa kosaย hilo na kufungwa kwa siri katika gereza moja la siri sana,ย Jamaal alikutwa na vitambulisho vilivyomuonesha kuwa anaย Uraia wa Nchi nane ikiwemo Marekani na Ukraine jambo ambaloย liliwashangaza sana lakini Jamaal alizungumza lugha nyingiย vizuri sana japo alikuwa na asili ya Somalia. Pia taarifaย ilienda mbali zaidi na kusema kuwa Jamaal alikutwa naย vitambulisho vya kijeshi vilivyoonesha kuwa aliwahiย kulitumikia jeshi la Israel na Palestina ndani ya miakaย miwili,ย
Zola alikaa chini na kujishika kichwa chake kisha akaulizaย
“Kwasasa Jamaal anashikiliwa gereza gani?” Swali hiliย lilimfanya polisi aliyekuwa akimueleza Zola akae kimya kidogoย kisha akasemaย
“Gereza lipo Ikulu ya Nchi, sisi hatuhusiki tena na kesi hiyoย Zola” Zola akauliza tenaย
“Kwanini mafaili ya kesi bado yalikuwa hapa?”ย
“Kwasababu kesi ilianzia hapa lakini cha kushangaza baada yaย kukamatwa tuliondolewa katika kesi hiyo”ย
“Nani alitoa oda ya Nyie kuacha hii kesi na ikaenda sehemuย nyingine wakati nyie ndio mnakazi hiyo?”ย
“Aliyetoa oda ni Rais wa Nchi” Zola aliondoka baada ya kupataย majibu yaliyochanganya akili yake kisha akawasiliana na Mzeeย Dawson wakapanga kukutana katika makazi ya siri ya Zola,ย Usiku Dawson alienda kuonana na Zola, kama kawaida yaoย waligida pombe ili maongezi yaanzeย
“Enhee umegundua nini Zola?” Aliuliza Dawsonย
“Mafaili yaliyobiwa katika kituo cha polisi yalikuwa ya kesiย ya Mtu anayedaiwa kuwa alihusika kumuuwa Makam wa Rais”ย Alisema Zolaย
“Unasemaje? Ina maana polisi wanajuwa ni nani alihusika?”ย
“Sio polisi pekee hata Mkuu wako wa Nchi ambaye anakupa kaziย ya kulisaka kundi la Mafia Gang anajuwa na kibaya zaidiย ametoa amri ya jeshi la polisi kuiacha kazi hiyo” Mzee Dawsonย alionekana kushangaa sanaย
“Inawezekanaje Zola?”
“Hiyo ndio hali halisi ndio maana nimekuita hapa iliย tuzungumze, nahisia mbaya juu ya Mkuu wa Nchi lakini sitakiย kujiaminisha chochote”ย
“Unataka kusema Mkuu wa Nchi kuna kitu anakificha hapa?” Woteย waliacha kunywa pombe wakazama katika maongezi yaoย
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SITAย USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย
ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx ย Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx
8 Comments
Lit
โ๏ธโ๏ธ
Naona inaelekea ukingoni
Nimekipenda kitabu hiki,
Nikama macho yanafumbuka ๐ค๐ค๐ค
Iko poa sanaaa
Fantastic
Nimekipenda kitabu hiki,
Nikama macho yanafumbuka ๐ค๐ค๐ค
Nimeipenda mno kiongoz ongera na asante ongeza bidii