Ilipoishia “Joshua naomba tuonane kwenye mgahawa muda huu” Alisema NoelaΒ kisha alikata simu, Desmond alishusha pumzi zake baada yaΒ kujiridhisha kuwa Noela hajagundua lolote maana kamaΒ angedungua asingemuita jina la Joshua bali angemuita Desmond,Β kumbe Noela alishajuwa kila kitu, alikuwa katika upeleleziΒ wake binafsiΒ
Desmond alipotoka pale Hotelini moja kwa moja alienda kuonanaΒ na Mchumba wake Noela kama alivyoambiwa, alimkuta Noela akiwaΒ amejawa na tabasamu na bashasha kitu ambacho kilimfanyaΒ Desmond azidi kujiamini kuwa Noela hajafahamu lolote lile,Β waliagiza chakula huku Noela akizidi kumsoma Desmond, akiliΒ ya Desmond haikutulia kabisa sababu alihitaji kufahamu kamaΒ Joel alikuwa amefanikiwa kupeleka Hundi ile kwa Mtu wa Tatu. Endelea
SEHEMU YA KUMIΒ
“Nimetoka Hospitali, unamkumbuka yule rafiki yangu uliyewahiΒ kuniona naye hapa?” aliuliza Noela makusudi ili kuzidiΒ kumsoma DesmondΒ
“Eeeh nakumbuka, anaumwa?” alihoji DesmondΒ
“Hapana amekutwa ameuawa huko porini, inasikitisha mno alafuΒ kaacha Mama anayeumwa sana” Alisema Noela huku akiwa makiniΒ sana na jicho lake la uchunguzi, Desmond alishtuka mno hukuΒ macho yake yakiwa yamemtoka pima kama Mjusi aliyebanwa naΒ mlangoΒ
“Ameuawa…..Nani aliyemuuwa?” alihoji Desmond akiwa katikaΒ hali ya kuchanganikiwa sana, Noela akagundua kuwa alichokuwaΒ ametumiwa na marehemu Lucia kilikuwa na ukweli mtupuΒ
“Haijajulikana, polisi wanafanya uchunguzi. Inasemekana piaΒ ameacha mgonjwa ambaye yupo mahututi na huyo mgonjwaΒ inawezekana kuwa chanzo cha kifo cha Lucia” Alisema NoelaΒ huku jicho lake likiongeza umakini wa kumtambua DesmondΒ
“Mgonjwa!! aaah Noela, naomba tuachane na hizo stori,Β tumekuja hapa kula Mpenzi” Alisema Desmond kisha alimwambiaΒ NoelaΒ
“Naenda chooni mara moja” Desmond alinyanyuka akaelekeaΒ Chooni bila kujuwa kuwa Noela alikuwa tayari amegundua kuwaΒ yeye ni MuuuwajiΒ
Japo moyo ulimuuma sana Noela ila kilichompata Lucia alijionaΒ ana kila sababu ya kuleta haki, Desmond alipofika chooniΒ alijiinamia kwenye sinki la kunawia maji akiwa amechoka sana,Β alianza kuhisi ugumu mkubwa sana kwenye Maisha yake,Β alimpigia simu Joel akamuuliza kama amekutana na huyo Mtu waΒ Tatu.Β
Joel akiwa ndani ya gari hilo aliloelekezwa alipokea simu,Β alionekana kuzungumza kwa kutulia sana huku pembeni yakeΒ kukiwa na mwanaume mmojaΒ
“Nimeshampatia” Alisema JoelΒ
“Haya basi tukutane mara moja pale tunapokutanaga….naonaΒ mambo magumu, Kifo cha Lucia kimekuja kuharibu kila kitu”Β Alisema Desmond, baada ya simu ya Desmond kukatwa JoelΒ alimgeukia Mwanaume ambaye yupo ndani ya hiyo gani akamwambiaΒ
“Ngoma imeanza kuchezwa, Hii Hundi hakikisha unachukua pesaΒ na kuziweka kwenye akaunti nyeusi, ni lazima tumtumie DesmondΒ kuvuna pesa alafu kila kitu kitamuangukia mwenyewe” AliagizaΒ Mwanasheria Joel, kumbe mwanasheria Joel ambaye niΒ mwanasheria wa Mandy ndiye Mtu wa tatu ambaye alikuwaΒ akijifanya kuzunguka kwenye suala lililojificha ili apateΒ pesa kutoka kwa Desmond kwa kujifanya anajuwa siri zaΒ Desmond, Mwanaume aliye pembeni yake ndiye yule ambayeΒ Desmond alikuwa akimtilia shaka na ndiye aliyekuwa akifanyaΒ michezo mingi michafu na ndiye aliyelitoa lile gari kuleΒ Baharini kisha akaliweka gari lingine kisha akawapigia simuΒ polisiΒ
Basi, Baada ya kumaliza kuongea na Joel akifikiria ni MtuΒ mzuri anayeshirikiana naye alirudi kwa Noela ambayeΒ alijifanya yupo bize akipata chakula, angalau baada ya kutokaΒ Chooni alionekana kuwa sawa japo Noela alikuwa ameshamgunduaΒ muda mrefu, walipata chakula ndipo Noela alipomchomekeaΒ DesmondΒ
“Nasikia Mgonjwa wa Marehemu Lucia ameamka leo, ingekuwaΒ faraja sana kwa Lucia kumuona mgonjwa aliyemhudumia kwa mudaΒ mrefu akiamka” Alisema kwa mtego Mkubwa sana na DesmondΒ akaingia mtegoni, alishtuka akaulizaΒ
“Unamaanisha Mandy?” alihoji akiwa ameamka kutoka kitini,Β ndipo sasa akawa amemdhihirishia wazi Noela kuwa ana Mke piaΒ ni MuuwajiΒ
Noela naye akaamka akijifanya kushangaaΒ
“Heee kumbe unamjuwa?” Alihoji NoelaΒ
“Hapana….Hapana simjui, Noela tutaonana baadaye” AlisemaΒ Desmond kisha aliondoka mbio kuelelekea Hospitalini bilaΒ kujuwa kuwa alikuwa ametegwa, Haraka Noela alimfuata kwaΒ nyuma kisha naye aliingia kwenye gari yake akawa anamfuatiliaΒ Desmond kwa nyuma, Safari hii ilifika hadi kwenye HospitaliΒ aliyolazwa MandyΒ
Akiwa amepaki gari eneo lingine la Hospitali tofauti naΒ alipopaki Desmond, Noela alipokea ujumbe kuwa Mgonjwa MandyΒ amerudisha fahamu, huu ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa DaktariΒ Mkuu wa Hospitali sababu alimuachia maagizo kuwa akiamkaΒ Mandy apewe taarifa na pia alipewa agizo moja kubwa sana,Β Noela akakumbuka alichomwambia DaktariΒ
Alimwambia kuwa anafanya uchunguzi wa kifo cha Lucia naΒ huwenda mgonjwa huyo akawa ndiyo chanzo cha kifo cha LuciaΒ hivyo atakapoamka pengine kuna siri anaifahamu hivyo kitu chaΒ kwanza ahakikishe anamuweka sawa kiakili ili DesmondΒ asishtuke mapema hadi pale watakapopata ushahidi wa kutosha
Akiwa mbio mbio, Desmond alifunga breki miguuni mwa DaktariΒ Mkuu aliyekuwa akitoka wodini kwa MandyΒ
“Dokta nimesikia Mke wangu ameamka” Alisema Desmond akiwaΒ katika hali ya haraka na hofu mnoΒ
“Ndiyo Mkeo ameamka ila bado hana nguvu, unaweza ukamuona ilaΒ usimkumbushe chochote” Alisema Dokta, Basi Desmond aliufunguaΒ mlango wa wodi hiyo, kweli alimuona Mandy akiangaza huku naΒ kule kama Mtu aliyekuwa akijiuliza yupo wapiΒ
Hofu ilimjaa sana Desmond kisha alimsogelea Mandy taratibuΒ huku akiwa mwenye maswali mazito sana ya kuwa Mandy amemjuwaΒ Desmond kuwa ni Muuwaji wa Mama ake, Mandy alipomuona DesmondΒ alionekana wazi kuwa na maumivu makali moyoni, alimtazamaΒ Desmond huku chozi likimbubujika, yule Daktari Mkuu alisimamaΒ mlangoni akichungulia tuΒ
Mandy alikumbuka siku ya tukio la yeye kupigizwa ukutani naΒ Desmond, siku hiyo ilikuwa hivi, aliiyona cheni ya Mama yakeΒ kwenye koti la suti la Desmond, cheni ambayo Desmond aliivuaΒ kwenye shingo ya Mama Mandy baada ya kumuuwa kisha akaiwekaΒ kwenye koti lake, Mandy alipoiyona ile cheni ndipoΒ alipogundua kuwa Desmond ni Muuwaji, wakati anapiga SimuΒ Desmond alitokea ndipo vurugu za kufukuzana zilipoanzaΒ
Tuendelee, Basi Desmond alisogea na kumshika mikono MandyΒ akamwambiaΒ
“Umeamka Mama?” alihoji DesmondΒ
“Wewe ni Nani?” aliuliza Mandy, Desmond alishtuka sana kishaΒ akajiuliza ina maana Mandy amepoteza kumbukumbu zake,Β alijikuta akitabasamu maana kama amepoteza kumbukumbuΒ hatoweza kumtaja kama Muuwaji wa Mama yake.Β
“Pole kwa maumivu sawa Eeh!! Mimi ni Mume wako Desmond”Β Desmond alijitambulisha pale, Daktari alielekea moja kwa mojaΒ kwenye maegesho ya Magari akamwambia Noela kuwa MandyΒ amefanya kama alivyoagizwa yaani kujifanya amepotezaΒ kumbukumbu.Β
“Safi sana, Desmond ni mchumba wangu na hii pete amenivishaΒ jana tu” Alisema Noela kisha aliivua pete hiyoΒ
“Sistahili kuwa na pete yake sababu ni Mume wa Mtu piaΒ Muuwaji, kwakuwa ameshajulikana ndiye Muuwaji basi kaziΒ iliyobakia niachie Mimi”Β
“Sawa!!” Noela aliondoka Hospitalini hapo.
Desmond alibakia Hospitali kwa ajili ya kuangalia kama kunaΒ chochote Mandy anaweza akakumbuka, hii ilimfanya yule DaktariΒ ashindwe kumpa taarifa muhimu Noela.Β
Jioni ilipoingia ilimkuta Noela akiwa nyumbani kwao akiwaΒ kwenye tafakari nzito kuhusu Desmond ambaye alimdanganya jinaΒ kama Joshua, alikumbuka vingi ikiwemo walipotoka, alijikutaΒ akiangusha chozi lenye maumivu makali sana, mapenzi aliyompaΒ Desmond yalikuwa ya dhati sana kwa kipindi chote, kugunduaΒ kuwa Desmond alikuwa Muuwaji na Muongo kulimliza sana Noela.Β
Alijikuta kwenye wakati mgumu sana, ndiyo alimpenda sanaΒ Desmond hadi kufikia hatua ya kuvishwa pete lakini angefanyaΒ nini wakati Mwanaume huyo alikuwa Muongo na Muuwaji.Β
Jioni hiyo alitoka akarudi kule Hospitali, Desmond alikuwaΒ wodini kwa kipindi chote akiwa na mawazo kuwa huwenda MkeΒ wake atarudisha kumbukumbu muda wowote ule, ili kumtoa paleΒ Noela alimtumia meseji Desmond akimwambiaΒ
“Mpenzi naelekea kwenye pori ambalo Lucia aliuawa, kunaΒ taarifa kuwa alipotoka nyumbani kwao alitoka na kitabu chenyeΒ siri pengine nacho kilikuwa ni sababu ya kifo chake,Β inasemekana kilipotea porini” Alipotuma meseji hiyo alijuwaΒ wazi kuwa Desmond ataenda huko porini ili kuhakikishaΒ alichoambiwa, kweli muda huo huo Desmond alikurupuka kutokaΒ pale wodini akaingia kwenye gari kisha akatoka.Β
Lakini wakati anatoka Desmond, yule Mwanaume anayetumwa kaziΒ na Mwanasheria Joel alikuwa pale ndani akamuona DesmondΒ akitoka kisha Noela aliingia wodini, yule Mwanaume alimpigiaΒ simu Joel haraka sana akamwambia alichokiona, basi harakaΒ Joel alimpigia simu Desmond na kumueleza kuwa kulikuwa naΒ mchezo uliokuwa ukichezwa hapo na kwamba mpenzi wake NoelaΒ alikuwa hapo Hospitalini na baada ya yeye kutoka Mpenzi wakeΒ huyo aliingia wodini kwa Mke wake Mandy.Β
Desmond alisitisha safari ya kwenda eneo ambalo Lucia aliuawaΒ baada ya kuambiwa kuwa kuna mchezo mchafu Hospitalini, harakaΒ aligeuza gari akarudi kule Hospitalini, akiwa hoi haiΒ aliingia wodini na kumkuta Mandy akiwa amelala huku chumbaΒ hicho kikiwa kimya sana, Desmond alishangaa sana wakatiΒ aliambiwa na Joel kuwa mpenzi wake alikuwa hapo, akaamuwaΒ kumpigia simu ili ajihakikishie alichoambiwa, simuΒ ilipopokelewa ilionesha wazi kuwa Noela alikuwa barabaraniΒ hivyo alishindwa kuthibitisha alichoambiwa, alimpigia simuΒ Joel na kumwambia alichokiona lakini Joel alimtaka DesmondΒ kuwa makini sana maana Mpenzi wake alikuwa hapo HospitaliniΒ na huwenda anafahamu kuhusu Mandy.
Alienda kukutana na Mwanasheria Joel ambaye alikuwaΒ akimchezea Mchezo mchafu, Joel alimuonesha video DesmondΒ iliyomuonesha Noela akiingia na kutoka pale wodini, ndipoΒ alipopata picha kamili kuwa Noela alikuwa amefanikiwaΒ kumfahamu, Joel alimuulizaΒ
“Huyo ameshajuwa siri kuwa wewe ni Muuwaji, kibaya zaidi huyoΒ ni mpenzi wako alafu mpelelezi utafanya nini?” Desmond alikaaΒ kimya baada ya sekunde kadhaa akamwambiaΒ
“Nitajuwa cha kufanya” Desmond alitoka kuonana na Joel,Β alionekana kuwa mwenye mawazo sana ya nini afanye, alimpigiaΒ simu Noela akamuuliza kama alifanikiwa kukipata hicho kitabu,Β alifanya hivyo makusudi ili kumfanya Noela afahamu kuwa badoΒ Desmond hajajuwa chochote.Β
Noela alimwambia kuwa hawakufanikiwa kukipata kitabu ilaΒ uchunguzi bado unaendelea, Desmond alipata wazo la harakaΒ nalo ni kuondoa uhai wa Noela maana Mke wake hakumbukiΒ chochote hivyo kwa vyovyote Mtu anayeweza kusema ukweli niΒ Noela.Β
Alimtunia ujumbe wakutane nyumbani kwake usiku wa siku hiyo,Β baada ya kuupata ujumbe Noela aliwataarifu polisi aliokuwaΒ akifanya nao kazi maana alihisi huwenda Desmond alishafahamuΒ kuwa anaijuwa ile siri ya Mauwaji. Usiku ulipofika NoelaΒ alienda nyumbani kwa Desmond, alimkuta akiwa ameketi mahaliΒ anapata biaΒ
Noela aliketi naye akapata chupa ya Bia bila hata kumsemeshaΒ Desmond, waligida kidogo kisha Desmond alimuuliza NoelaΒ
“Umemuaga Mama?”Β
“Ndiyo!!” Alijibu NoelaΒ
“Siku moja ya uchumba wetu umeshavua pete ya uchumba” AlisemaΒ Desmond ndipo Noela aliposhtuka sasa kuwa Desmond alikuwaΒ ameshafahamu.Β
“Nafikiri ni kitu cha kawaida, inakuwaje kwa Mtu akawa naΒ majina mawili, la uhalisia analificha na kutumia jina feki?”Β Alisema Noela, hakukuwa na siri tena sababu kila jamboΒ lilikuwa waziΒ
“Noela umekuwa kikwazo kwangu, ili niwe salama ni lazimaΒ nikutangulize” Alisema Desmond kisha alitoa bastola akawaΒ anaifutafuta
“Kwa mpelelezi ambaye amefanya kazi nyingi hawezi kuogopaΒ kufanya kazi hata kama ni hatari kiasi gani au inamgusaΒ ampendaye, Desmond….kumbe una Mke tena ni Mke ambayeΒ ulitaka kuutoa uhai wake kisa pesa, unakumbuka kuhusu MamaΒ Mandy?” aliuliza Noela, Desmond alijawa na hasiraΒ akamnyooshea NoelaΒ
“Kabla hujaniuwa Desmond, nataka nikwambie kitu kimoja. PesaΒ haiwezi kukupa kila kitu katika Maisha yako, ila MaishaΒ yanaweza kukupa kila kitu ikiwemo na pesa, waliochagua kuishiΒ walifanikiwa lakini wewe ulichagua pesa ili uishi”Β
“Ishia hapo hapo Noela” Alisema Desmond kisha alifyatuaΒ risasi iliyowashtua polisi aliokuja nao NoelaΒ
Haraka waliingia na kumkuta Noela akiwa chini anauguliaΒ maumivu ya bega, bastola ikawa udhibiti kwa Desmond,Β alikamatwa na wale polisi. Taarifa ya kukamatwa kwa DesmondΒ ilimfikia Joel, akapata wazo la kuikimbia Nchi maanaΒ alishajuwa kuwa atatajwa na kukamatwa, Naam!! alitajwa naΒ Desmond, Joel alienda kukamatwa Uwanja wa ndege….Β
Taarifa ya kukamatwa kwa Joel na Desmond ilimfanya Mandy alieΒ kwa uchungu mkubwa, baada ya kupona kwa Noela, Desmond naΒ Joel walifikishwa Mahakamani kwa makosa ya Mauwaji, MandyΒ alisimama kama Shahidi namba moja, Hatimaye Desmond na JoelΒ walifungwa kifungo cha Maisha jela, Mandy alimshukuru sanaΒ Noela kwa msaada huo hadi kukamatwa kwa WauwajiΒ
Noela aliishia maisha ya majuto sana sababu aliamini kamaΒ angelifanyia kazi mapema bahasha aliyopewa na Lucia basiΒ rafiki yake huyo asingeliuaawaΒ
MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & PainΒ
Β Β
8 Comments
Mapenzi na Maumivu ββ
Mapenzi ni Maumivu β
Na Pesa sio kitu
Utu ndio kila kitu.
Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mafunzo na mazingatio katik maisha yetu ya kila siku hususan maisha yetu ya saiv.
Asanteni.
Mtunzi na Adminβ€οΈ
Asant adimin
Mapenzi na pesa
Uki ambatanisha na jua
Oyaa oyaa oyaa
πππππ
ππ
Imeisha ghafula π₯Ί
Upendo na maumivu
.pesa SI Kila kitu. ??
.Kila kitu ni pesa??
π₯Ίπ₯Ίπ₯Ίπ₯Ί
Duh
apo safi bora imeisha imenisubirisha sana hii admin siku nyingine tuwekee ratiba mambo ya mpira yakiwa mengi