Ilipoishia “Scola nijibu alikuja Mgeni si ndiyo?” Nilimuuliza tena baada ya kuona alikuwa hanipi jibu
“Lakini Dada..” alisema Scola, nikahisi kuna jambo
“Sitaki cha lakini nataka uniambie ukweli ni nani alikuja hapa?” Nilimkazia sauti na jicho
“Baba alisema nisiseme unanipa wakati mgumu Dada Jacklin” Nilimshika mkono Scola nikamuingiza chumbani kwangu nikamwambia
“Tupo Mimi na wewe naomba unieleze ukweli ni nani alikuja hapa” Endelea
SEHEMU YA KUMI NA NNE
“Kusema ukweli ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kumuona ila nakumbuka Baba alisema nisikwambie wewe, aliniambia niandae chakula chenye hadhi ya kuliwa na Bilionea. Aliniambia kuwa ni Mtoto wa tajiri Mkubwa sana anaitwa Dhabi” Alisema Scola
“Basi inatosha, Asante!!” Nilimkatisha Scola, nilifungua mlango na kumpa ishara kuwa atoke, alikuwa ameniambia ukweli ambao nilifichwa na Lidia na Dokta Simon.
“Dada naomba Usimwambie Baba” alisema Scola
“Usijali Scola siwezi kufanya hivyo, nenda nahitaji kupumzika” Basi Scola aliondoka zake
Unajuwa yale maumivu ya kuchomwa na msumari mguuni? Ndiyo ambayo nilikuwa nikiyapata kwenye moyo wangu, kulia haikuwa tiba, kukaa haikuwa tiba, nilitamani nipate sehemu yenye utulivu nipige ukunga hadi sauti yangu iishe.
Basi siku mbili zilipita, ilikuwa ni tarehe 25/09 ndiyo siku ambayo iliandikwa kwenye ile kadi, moyo wangu uliniambia kuwa ndiyo siku pekee ya kuonana na Osman, nilisoma muda ambao Harusi ilikuwa ikifanyika, ilikuwa ni saa 2 Usiku katika Hoteli ya nyota tano ya BAMOL DE HOTEL, muda nawaza yote ilikuwa ni mchana
Nilijaza jina langu kwenye ile kadi, nilijuwa tukio litawashangaza wengi lakini ili moyo wangu utulie ni lazima nionane na Osman na sehemu peke ilikuwa ni kwenye harusi yake.
Niliandaa gauni langu zuri jeusi, mishale ya saa moja nililivaa, nilijitazama kwenye kioo niliona jinsi nilivyopendeza ila nilipofunua gauni nilipata huzuni sana, sikuwa na mguu mmoja wa kuvalia kiatu, mkononi nilikuwa nimeshikilia kiatu cheusi cha kupanda
Nilikitupa pembeni, nilikusanya magongo yangu, nilimpita Scola akiwa anaingia jikoni, niliondoka nyumbani Usiku huo ili nielekee Hotelini, niliita Tax nikaanza safri huku moyo wangu ukiwa na maamuzi mawili ya kuacha au kuendelea na safari, niliazimia ni bora niende tu. Nikiwa kwenye Tax Lidia alinipigia simu akaniuliza nipo wapi, nilishangaa sana
“Nipo njiani narudi nyumbani” nilimjibu
“Ulikuwa wapi?” Aliuliza
“Nilikuwa kwenye matembezi kidogo nilichoka kukaa tu nyumbani”
“Sawa ukifika nipigie niongee na Scola”
“Sawa!” Alikata simu
Niliona ni bora niizime simu sikutaka tena kufikiria kuhusu wao.
Nilifika Hotelini mishale ya saa tatu kasoro, palikuwa pamepambwa sana kwa nje, ulinzi ulikuwa wa kutosha sana sababu aliyeko ndani alikuwa ni Bilionea Mkubwa sana.
Niliangalia kadi yangu, niliongoza kuelekea kwenye lango kuu ambalo lilikuwa na walinzi, kumbe nyuma yangu alikuwepo Dokta Simon alafu sikushtukia ila kwakuwa alikuwa na pirika nyingi wala hakuniona, nilimshtukia aliponipita.
“Kumbe mpo hapa Mjini eeh! Kitakachotokea hamtoamini, kama hamtotaka kuishi na Mimi tena ni sawa tu” nilijisemea ndani ya moyo wangu! Nilionesha kadi yangu pale mlangoni nilikaguliwa kisha niliruhusiwa kingia ndani ya Hoteli, nilielekezwa mahali ambapo harusi ilikuwa inafanyika.
Nilitembea na Magongo yangu kwa tahadhari sana maana kama nitakutana na Lidia au Mume wake mpango ungekufa. Watu walikuwa wamependeza sana, ile nakaribia nilimuona Mzee Dhabi akizungumza na Simu basi niligeuza haraka kama narudi nilipotoka maana kama ningeendelea mbele angeniona, bahati nzuri kulikuwa na chemba upande wa kushoto niliingia huko hadi pale alipomaliza kuongea na kurudi Ukumbini.
Nilijitoa na kuelekea Ukumbini, kweli ilikuwa ni harusi ya Kifahari ambayo hata kwnye Filamu sikupata kuishuhudia, roho iliniuma sababu nilipaswa kuolewa mimi, ilipaswa Mama yangu awepo kwa ajili ya furaha ambayo aliipigania.
Nilitafuta Kiti cha nyuma kabisa ili nisije onekana na wanafamilia, Muda ambao nilikuwa nimefika ndio kwanza ilikuwa inaanza. Matajiri wenye rangi nyeupe walikuwa wengi mno, nilijitahidi kuangaza huku na kule ili nimuone Osman.
Kweli nilimuona Osman, huwezi amini nilijikuta nikisimama bila kurajia, nilimtazama Osman akionekana kuwa mwenye furaha sana, pembeni yake alikuwepo Zahra naye akiwa mwingi wa tabasamu. Nilishuka na kuketi bila kutaka, Shughuli ilianza kwa kutambulisha baadhi ya Watu wakubwa waliohudhuria pale, Dokta Simon na Lidia walikuwa wakizungumza jambo huku wakionekana kupiga simu bila kupokea majibu, nilijuwa tu walikuwa wakinipigia Mimi kujuwa niko wapi naona hata wao hofu iliwaingia maana Scola sikumuaga kabisa.
Nilisubiria muda sahihi wa kuonana na Osman bila kubuguzi mtu yeyote wala kuharibu chochote kile ila kadili muda ulivyozidi kwenda ndivyo nilivyogundua kuwa hali yangu ya kuhitaji kuonana na Osman ilikuwa ikipanda.
Muda wa Osman kumvisha pete Zahra ulipowadia roho ilizidi kuniuma, wengi walisimama na kupiga makofi kwa ajili ya tukio, ila macho yangu yalikuwa yakibubujikwa na machozi mfululizo, nilijitahidi kujizuia nilishindwa, nilitamani kuondoka pale Ukumbini pia nilishindwa. Katika hali isiyo ya kawaida nilihisi kuguswa kwenye bega langu, nilipogeuka nilikutana na Lidia. Nilishtuka sana huku chozi likiendelea kunibubujika
“Jacklin umefuata nini hapa?” Aliniuliza Lidia kwa sauti ya Chini ambayo hakuna aliyesikia maana wengi akili yao ilikuwa kule mbele. Nilimpiga kofi Lidia
“Muongo Mkubwa wewe, kama ni furaha kusema uwongo na kuficha kilicho kizuri basi furaha yako haiwezi kudumu Lidia, wewe ni Muongo na mnafiki Mkubwa” Nilisema kwa sauti ya kawaida ambayo baadhi waliisikia
“Jacklin naomba tutoke tukaongee tusije haribu shughuli ya Watu” Alisema Lidia
“Tayari imesha haribika Lidia, unafikiri nitakubali kuondoka bila kumwambia Osman kuwa nipo hai, kumwambia kuwa Mimi ni kilema wa Mguu, kumwambia kuwa Mama yangu amefariki, kumshukuru na kumuomba Msamaha?” Watu wa karibu walianza kututazama, Lidia alishtukia hilo akasema
“Nakuelewa Jacklin, naomba tukaongee hilo halina shida” akaanza kutaka kunitoa pale kitu ambacho sikukubaliana nacho
“Niacheeee! Niache Lidia Niache…” nilisema kwa sauti ya Juu ambayo ilimshtua kila Mtu, macho yote yalikuja upande wetu. Bahati nzuri nilikuwa nimeonesha mgongo kule waliko akina Osman hivyo aliyeonekana vizuri alikuwa ni Lidia, Dokta Simon haraka alikuja baada ya kumuona Mke wake
“Jacklin hukupaswa kuja hapa kabla mambo hayajaharibika nakuomba urudi nyumbani, yote tutayaongea kule” Alisema Dokta Simon
“Siwezi kuondoka hapa bila kuongea na Osman, hamjui ni jinsi gani naumia Mimi, hamjui ni jinsi gani Maisha yangu yamejaa majuto, ili moyo wangu uwe sawa ni lazima nionane na Osman leo” nilisema kwa sauti ya Juu, Osman alinisikia, sauti yangu aliijuwa, alipiga hatua tatu mbele akiwa ameshikilia pete, Zahra alimshika mkono kumzuia asije upande wangu! Hakuna aliyeshtuka kuwa nilikuwa ni Mimi
Upande wa Familia ya Osman wote walisimama, taa ililetwa kwangu ili nionekane. Ilibidi nigeuke kutazama mbele ambako Osman na Watu wengine walikuwepo, Mzee Dhabi alishtuka sana kuniona, Osman alitumbua macho yake kwa Mshangao, hakutegemea kama angeniona tena katika Maisha yake.
Dokta Simon na Mke wake walitazamana ni wazi hawakufurahia Mimi kuwepo pale, chozi lilikuwa likinivuja, nilimtazma Osman ambaye naye alikuwa bize kunitazama, Zahra aliuacha Mkono wa Osman. Ukumbi mzima ulikuwa kimya sana
Nilichukua magongo yangu nikaanza kujongea kuelekea aliposimama Osman, nilimuona akiwa mwenye mshituko mkubwa baada ya kugundua kuwa nilikuwa kilema wa mguu, hata Mzee Dhabi na Mke wake nao walishangaa sana.
Nilisogea karibu na Osman nikiwa natabasamu kwa maumivu makali sana, Osman alidondosha chozi lake
“Jacklin?” Aliniita, niliitika kwa kutumia kichwa maana mdomo ulikuwa mzito sana
“Upo hai? Ulipatwa na nini, umepoteza Mguu?” Aliniuliza kwa hisia kali sana, nilitoa tabasamu lenye maumivu nikamwambia
“Nilipata ajali” nilitokwa na machozi nilishindwa kujizuia kabisa
“Mama yupo wapi?”
“Mama amefariki Osman”
“Mungu wangu! Mlienda wapi?” Aliuliza Osman, nilitaka moyo wangu uwe safi, nilimuonesha kidole Baba yake
“Baba yako alitufukuza kwenye ile nyumba, tulirudi Mtaani ndipo yalipotukuta haya yote, naomba unisamehe Osman, nilihitaji kukusaidia sana ila nilichelewa” Watu wote walimtazama Mzee Dhabi, ilitosha kuidhihirishia Dunia kuwa Baba yake Osman alitutendea Unyama!! Osman alimgeukia Baba yake akamuuliza
“Baba ni kweli?” Aliuliza Osman akiwa anatiririkwa na machozi, Mzee Dhabi hakuwa na jibu zaidi ya kuinamia chini.
“Baba ulisema waliuza kila kitu na kuhama Mji, ulisema haijulikani kama wapo hai au wamekufa, walikukosea nini Baba? Kumbe mkatili kiasi hicho Baba yangu! Mungu ameamua kukudhihirisha mbele za Watu wanaokuheshimu na kutaka kuwa kama wewe, ulitaka iwe hivi si ndiyo?” Alisema Osman kwa hisia kali ambayo hakuna aliyeweza kumzuia
“Osman imeshatokea! Hayo yamepita, nahitaji msamaha wako tu” Nilisema.
“Jacklin nilishakusamehe tokea ile siku ambayo ulikataa kuwa Mke wangu, niliheshimu maamuzi na mawazo yako” Alisema Osman, huzuni ilitanda pale ukumbini, wenye mioyo midogo walilia
“Baba ulitaka nimuowe Zahra kwasababu alikubali kutoa figo yake kwa ajili yangu? Ukasahau ndiye aliyesababisha jeraha ndani ya Moyo wangu, aliniacha katika wakati ambao nilikuwa sina chaguo lingine. Maumivu na mateso niliyoyapta ameyalipa kwa kutoa Figo lake, Hata Moyo wangu Baba unajuwa kuwa nampenda Jacklin, namuhitaji ila ulijaribu kumuweka mbali na Maisha yangu!” Alisema Osman kisha alinikumbatia, Huwezi amini Zahra alilia sana pale chini, alitoka mbio akakimbilia nje
Mzee Dhabi na Mke wake walilia kwa maumivu makali sana. Nilivyomkumbatia Osman nilihisi akiwa anapumua kwa shida sana, alikuwa akitaka kusema neno ambalo nilitamani kulisikia, neno ambalo hadi hivi leo sijui alikuwa anataka kuniambia nini, alisizi kwenye mwili wangu bila kuhema tena, ilikuwa ndiyo Pumzi ya Mwisho ya Osman katika hii Dunia, hakuna aliyejuwa kuwa Osman alifia kwenye mwili wangu. Mzee Dhabi alisogea na kupiga magoti akasema
“Osman! Nisamehe Mwanangu,,nisamehe kwa yote, nilifanya kwa hasira baada ya kuona amekataa kusaidia Maisha yako, nimekupa hasara Jacklin umempoteza Mama yako na Mguu wako naomba mnisamehe” Alisema Mzee Dhabi, ukimya wa Osman ulianza kunipa wasiwasi, nilimuacha lakini cha ajabu alienda chini kama Mzigo, haraka gari ya wagonjwa ilifika, Osman alipelekwa Hospitalini. Sote tulienda kusubiria hatma ya Osman, kila mmoja alikuwa kimya, nilikuwa mwingi wa kulia tu.
Masaa matatu Baadaye Dokta Simon alitoka chumba cha Wagonjwa mahututi, alitupa taarifa iliyoondoa uhai wa Bilionea Dhabi pale pale, Ndio, Osman alikuwa amefariki kwa mshituko na mfadhahiko. Mzee Dhabi na Osman walizikwa nyumbani kwa Osman,,,nilimshukuru Mungu kwa kila jambo lililonifika kwenye Maisha yangu. Nilipoteza kila kitu lakini Mke wa Bilionea Dhabi aliniambia kuwa ananipa Nusu ya mali zote za Bilionea Dhabi.
Nilipewa kila kitu nilichoahidiwa, japo havikuwa na thamani ya kuzidi uhai wa Osman, Bilionea Dhabi, Mama na Mguu wangu. Nilijiapiza kuwa sitokuja kupenda tena katika Maisha yangu.,,,,Miezi mingi ilipita, maumivu ndani yangu yalianza kupona, niliwekewa mguu wa Bandia.
Siku moja asubuhi nikiwa naelekea JM Motors nikiwa kama mmiliki wa kampuni hiyo ya Uuzaji wa magari, nilijikuta katika foleni eneo lile lile ambalo nilijikuta kwenye Foleni siku ya kwanza kabisa ambayo nilikuwa naenda JM Motors kuomba kazi, ndiyo siku ambayo nilikutana na Osman. Moyo wangu uliingiwa na maumivu makali sana, nikiwa nasubiria gari zianze kutembea, Mtu mmoja ambaye ni ombaomba aligonga kioo cha gari yangu! Nilikuwa ni Mtu ninayezijuwa shida sana kutokana na Maisha niliyopitia, nilifungua kioo, moyo uliniripuka sana. Aliyegonga kioo alikuwa ni Mosses Mwanaume niliyekuwa nampenda sana katika Maisha yangu, alikuwa haoni yaani kipofu wa macho yote mawili hivyo yeye hakujuwa alikuwa akimuomba pesa nani, sikujuwa alikuwa amekutwa na nini ila hata vidole vyake vilikuwa vimekatika.
Nilimpa noti ya Shilingi Elfu tano, kisha aliondoka zake, unajuwa kwanini nilimpa noti ya Elfu tano? Ni kwasababu ile siku aliniahdi kunitumia pesa ya pikipiki alafu hakunitumia wakati huo Elfu tano yangu nilimpa marehemu Osman, nilisema
“Malipo ni hapa hapa Duniani Mosses, Kwaheri ya kuonana” Nilifunga kioo kisha niliondowa gari yangu.
••MWISHO•••
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kununua SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho
19 Comments
Ongera nimeipenda
Ila wewe dada!!!!
So sad 😢
Mapenzi ni ugonjwa usio na dawa
Eeee Mwenyezi Mungu naomba unipe atakae nipenda kwa dhati kama mapenzi ya Osman kwa Jacklin.
Stori ya kuhuzunisha yenye Mafundisho tosha na maumivu makali ndani yake.😭
Maskini Jacklin kapoteza kila kitu maishani mwake😢
😭😭Dah wow asee nimeipenda sana🔥🔥🔥 hii episode imeniuma sana
😭😭😭😭😭😭😭
Una jua yale maumivu ya kuchomwa msumari kwenye isia feck 😆😆😆😆
💫💥💥💥💥💫
Appriciated @Kaka mkubwa
Live long…uzidi kutupa madude mkuu😎🤍
Una jua yale maumivu ya kuchomwa msumari kwenye isia feck 😆😆😆😆
Nampa pongezi mwandishi kalamu yake amejua kuitendea haki Yuko vizuri 😘😘😘
Kiukweli nimejifunza kitu asante mwandishi unajua unastahiri mauwa yako
Tamu sana inajenga hisia fulani
Chukua🌹🌺🌷🥀 yako
Kali kinoma
Kaka mkubwa KWELI wewe ni kaka mkubwa umeumba ulimwengu wa kufikirika mpaka basi……. SASA WATENGENEZA FILAMU MPOWAPI? HAMONI MNANGOJA NINI?…SHIRIKIANENI NA KAKA MKUBWA!!! MTUTENGENEZEE DUDE JAMANIEE
Inagoma nkitaka kutuma hela….inasema no hii haijathibitishws
Aiseee hii simulizi ni nzuri sanaa 🏆
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H