Ilipoishia “Lakini Mosses mbona hukuniambia kama unafungua Biashara?ย Unafikiria ndani ya huo mwezi Mimi na Mama tutakuwa tunaishiย wapi?” Nilimuuliza Mossesย
“Sasa Jacklin unafikiria pesa inahifadhiwa benki kama pamboย la nyumba? Pesa ni lazima izunguke ili izae halafu Mimi niย Mwanaume nimefanya maamuzi ya kiume” Alisema Mosses, suraย yake ilianza kutanda hasira. Sikutaka kuendelea kubishanaย naye nilimkubaliaย
“Sawa Mume wangu! Nakutegemea wewe kwasasa” nilisema “Usijali” alijibu Mosses, nilimuaga nikarudi nyumbani kwetu.ย Endeleaย
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Nilimuamini sana Mosses, nilijuwa nitaipata hiyo pesa ilaย sasa huo muda ambao alisema atanipa nilifikria tutaendaย kuishi wapi Mimi na Mama yangu? Nilipoongea na Mamaย sikumwambia kuhusu zile pesa istoshe alikuwa hajui kama kunaย pesa hiyo. Aliniuliza tu nina akiba gani, kiukweli sikuwaย hata na hamsini mbovu, maana nilijuwa na tumaini kubwa kwenyeย zile milioni 60 zilizo kwa Mosses, niliona aibu hata kumjibuย Mama kuwa sina pesa, nilikaa kimya japo Mama alinielewaย
“Mimi nina Milioni moja Jacklin, tufanye mpango wa kutafutaย chumba kimoja” Alisema Mama huku akitabasamu kwa maumivuย makali, kilikuwa ni kipindi kigumu sana kukielezea.ย
“Itabidi tutafute mahali pa kuishi Jacklin, imeshatokea niย lazima tukubaliane na hali halisi” Alisema Mama, nilitamaniย sana kumwambia tukaishi nilipompangishia nyumba Mosses lakiniย nilihofia kwa jinsi wawili hao walivyokuwa hawaivi chunguย kimojaย
“Sawa Mama haina shida” Huzuni ilitanda kwenye nyumba yetu.ย
Siku iliyofuata Mzee Dhabi alituma Watu, tuliwapa funguo zaย magari yote kuanzia na lile jipya na mengine ambayo hataย nilikuwa sijui kuendesha, yaliondoka yote. Nilianza harakatiย za kutafuta chumba cha kupanga ili niishi na Mama yangu,ย bahati nzuri nilipata japo uswazi huko ila ndiyo Maishaย ambayo tulishayaishi hivyo haikuwa shida sana kurudiย Uswahilini huko.ย
Baada ya muda ambao Mzee Dhabi aliusema, alirudi kwa ajili yaย kuchukua funguo za nyumba, Mama alijitahidi tena kuongea nayeย ila Mzee huyo hakusikiliza kabisa. Tulihama kwenye jumba laย kifahari ambalo Osman alitununulia, msichana wa kaziย aliondoka kwao, hatukujuwa maamuzi hayo yalitoka kwa mwenyeweย Osman au Mzee Dhabi aliamuwa kutumia hasira zake tu.
Tuliachaย kila kitu ndani ya Jumba hilo, nguo pekee ndizo tulizoondokaย nazo. Hatukuwa na godoro, tulinunua baadhi ya vitu kidogo iliย pesa itusaidie kwenye mahitaji ya hapa na pale, tumainiย lilibakia kwa Mosses japo kila nilipo mpigia simuย alinizungusha kuonana naye, nilipoenda anapoishi nilikutaย pamefungwa, niliishi kwa tumaini tu kuwa Maisha yaleย yasingekuwa ya muda mrefu.ย
Siku zilipita, tuliishi kwa matumaini, tulilala kwenye mkeka,ย niliona jinsi Mama alivyokuwa akiteseka roho iliniuma sababuย chanzo cha yote nilikuwa ni Mimi. Namba za Osmanย hazikupatikana kabisa, hatukujuwa kama alikuwa mzima auย alikuwa amekufa, mwisho tulifuta namba zake. Miezi ilisonga,ย Mosses hakupatikana kwenye simu kabisa, hata alipokuwaย anaishi alihama na sikujuwa ningempata vipi, moyo wanguย ulijawa na maumivu makali sana, pesa zilianza kuisha,ย tulishauriana Mimi na Mama tufanye nini kwa pesa iliyobakia,ย kila nilipojaribu kwenda kuomba kazi nilikosa, Mama alishauriย tuanze biashara ya Mboga mbogaย
Tulikuwa tunaamka asubuhi mapema tunaenda Bustanini,ย tunanunua mbogamboga tunaenda kuuza, Waliotujuwaย walitushangaa sana, waliosikia kilichotokea walitucheka naย kutuona hatuna akili, ningefanya nini zaidi ya kukubaliย masimango yao ili mkono uwende kinywani, Mimi na uzuri wanguย na usomi wangu niliishia kutembeza mbogamboga Mitaani.ย
Siku moja nikiwa nauza Mbogamboga nilimuona Mtu aliyefananaย sana na Mosses, nilitamani kumuona kwa ukaribu zaidi. Ndio!!ย Alikuwa ni yeye, alikuwa ameongozana na Mwanamke mmoja.ย Niliona kama vile nimeokota Almasi kwenye zizi la ng’ombeย nilimkimbilia Mosses na kumkumbatia. Hakuonekana kunifurahiaย kabisa, yule Mwanamke aliulizaย
“Wewe Dada vipi unakichaa au?” Nilijitoa mwilini mwa Mossesย
“Ndio! Mimi ni kichaa sababu Sijamuona huyu Mtu kwa mudaย mrefu, Mosses haujui ni jinsi gani nimekutafuta” Nilisema,ย beseni la mbogamboga lilikuwa limeanguka pembeni na mbogaย zote zilikuwa chini kwa jinsi nilivyokuwa nimefurahiย
“Kutokumuona muda mrefu na kumkumbatia mbele ya Mke wake kunaย husiana nini? Mosses huyu ni Nani?” Aliuliza yule Mwanamkeย
“Simjui Mimi” Nilishtukaย
“Mosses hunijui Mimi Jacklin? Au kwasababu nimebadilika?”ย Kiukweli nilikuwa nimebadilika, sio Jacklin yule ambayeย alikuwa akimfahamu, kutembea kwenye jua ilikuwa ndiyo Maishaย yangu hadi ngozi yangu ilibadili rangi.
“Sikujui kabisa, nimeshangaa sana unakuja kunikumbatia mbeleย ya Mke wangu” Alisema Mosses, nilisogea nyuma, niliokotaย mboga zangu na kuzirudisha kwenye beseni langu.ย
“Samahani nilikufananisha na Mosses wangu, mmefanana,ย Samahani Dada” Nilisema kijasiri sana kisha niliondoka zangu.ย Mbele ya macho yangu nilidondosha chozi, nilienda kukaa chiniย ya Mti nililia mno tena kwa kusaga meno. Niliumia kwa mamboย mawili kwanza kudharirika na pili kupoteza tumaini la kuipataย ile Milioni 60 ambayo Mosses aliichukua kwenye akaunti yanguย ya Benki.ย
Jua lilikuwa langu, mvua ilikuwa yangu, nilichotakiwa niย kuhakikisha napata pesa itakayoendesha Maisha yetu Mimi naย Mama yangu, nilijiuliza kitu kimoja kama nitaendelea kuliaย nini kitabadilika kwenye Maisha yangu? Hakuna, basiย nilinyanyuka na kuondoka zangu, nilirudi nyumbani maana mbogaย nyingi nilikuwa nimeshaziuza iliyobakia niliipigia mahesabuย nitakaporudi iwe ndiyo Mboga maana siku hiyo Mama hakwendaย kuuza mboga alikuwa hajisikii vizuri.ย
Mdogo mdogo nilifika nyumbani, kulikuwa na mmama anaitwa Mamaย Amina alikuwa ni Mpangaji mwenzetu. Alinisimamisha kabla hataย sijaingia ndani alinipa taarifa kuwa Mama yangu alikuwaย ameanguka chooni hivyo amekimbizwa Hospitalini, nilishtukaย sanaย
“Hospitali gani?” Nilimuuliza beseni likiwa chiniย
“Wamempeleka Kwa Dokta Simon” alipomaliza kunielekezaย nilitimua mbio kuelekea Hospitalini. Mama yangu alikuwa ndiyeย Mtu pekee aliyebakia na Mimi, alikuwa ndiye tumaini langu,ย taarifa ilinichanganya sana. Nilikuwa katika hali yaย kuchanganikiwa sana, nilijikuta nikigongwa na Pikipiki nikiwaย nakaribia Hospitalini.ย
Nilipoteza fahamu zangu kutokana na ile ajali mbaya yaย Pikipiki, nilipokuja kurudisha fahamu ilikuwa ni sikuย iliyofuata, nilijikuta nikiwa Hospitalini, nilihisi maumivuย makali sana ya Mguu wa kulia, kulikuwa na wepesi sana naย ubaridi hadi nilishangaa, nilipeleka mkono ili kuugusa mguuย wangu!! Nilishtuka sana, nilikuwa nimeshakatwa Mguu, nililiaย sana.ย
Dokta Simon alikuja kuniangalia maana mara nyingi alikuwaย akipita kukagua Wagonjwa, ndipo aliponiona, alinijuwaย kutokana na ile iliyotokeaga kati yangu na Osman, alishangaaย sana, nilikuwa katika maumivu makali na majonzi, alinipa poleย kisha aliniambia
“Pole sana kwa kilichokupata na kilichomfika Mama yako” Mwiliย ulisisimka ghafla sana, wazo la Mama kuwa alikuwa Hospitaliniย lilinijiaย
“Mama yangu anaendeleaje Dokta?” Nilimuuliza huku Kidonda chaย Mguu kikiwa na maumivu makali sanaย
“Mama yako alishafariki tokea jana”ย
“Nini?”ย
“Ndiyo Pole sana Jacklin, Mwili wa Mama yako umechukuliwa leoย kwa ajili ya mazishi, umezikwa na Manispaa sababu hakunaย ndugu aliyejitokeza!” Alisema Dokta Simon, moyo uliloa choziย la Maumivu, Nilijihukumu sana kwa kilichomfika Mama yangu,ย Nililia sana.ย
“Usilie Jacklin, Maisha ndivyo yalivyo. Kwasasa unaishiย wapi?” Aliniuliza, nilijawa na kwikwi sana sikuweza kumjibuย mwisho alisemaย
“Tutaongea utakapokuwa sawa Jacklin, pole kwa Msiba na poleย kwa yaliyokufika” Alisema kisha aliondoka, niligumiaย
“Mamaaaaa! Umeniacha kilema Mwanao!! Mamaaa umeondokaย umeniacha na Nani Mimi” Aaah! Chozi lilikuwa ndiyo rafikiย yangu, nililia sana, sikuwa na uwezo wa kunyanyuka walaย kutembea.ย
Baada ya wiki mbili kupita Dokta Simon alikuja tena kishaย aliketi kando yangu, angalau nilikuwa nimetuliza maumivuย yangu! Alinipa pole kabla ya kuanza kuzungumzia kilichokuwaย kimemletaย
“Kwanza pole sana Jacklin, Dunia yako imekugeuka lakiniย ndivyo ilivyo sababu siyo Watu wote wanakuwa na simulizi tamuย za Maisha yao, yako chungu sana. Osman alikutafuta sana,ย ilisadikika kuwa Mlikuwa mmeuza kila kitu na kuondoka”ย Alisema Dokta Simon, stori yake ilikuwa ngeni masikioniย mwanguย
“Tuliuza kila kitu?” Nilimuulizaย
“Ndiyo! Mzee Dhabi pia alihangaika kuwatafuta bila mafanikio,ย mwisho alikata tamaa baada ya kupata taarifa kuwa mliuzaย nyumba na kuondoka wewe na Mama yako!”ย
Haraka niligundua kuwa Mzee Dhabi alifanya yote pasipo Osmanย kujuwaย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA TATU Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย
ย ย
18 Comments
๐ญdunia simama mimi nishuke ๐ฎ๐daah had nmelia aseeeeeee
Tamu hiyooooo๐
๐ฅบ๐ฅบ๐ฅ๐ข
akome kabisaa aliyataka mwenyewe
Bamu balaha
Hujafa hujaumbika
What goes around is what comes around!!๐๐ mejaribu kingeresa jamn kama nimekosea mnambiee
Hujakosea upo sawa kabisa brother dunia ina zunguka. Ulipo anzia wakati fulani ndipo unapoishia.
Mara hutokea sivyo. HEBU TUANGALIE KIJACHO………
Hatari Yan jacklin yanamkuta mazito mno
Mmmh ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Mm nafurahi sana huyu dada yalomkutaa
Mmmh!! Usiombe yakukute kaka au dada sijui
Tuulize sisi yalotukuta
Jacklin hana tofauti sana na mm sema yeye mwanaume alompenda alimpa uhuru sana wa mali zake
Wanaume wa siku hisi wanapenda sana misaada kutoka kwa wanawake wakifanikiwa wanasahau kila kitu.
Ila kweli sister umenen huwa tunjisahaulisha sna baada ya kupat mali kutok kwen sas hili limekuw fundishoo
Dah
Ebu ngoja nimpigie mama angu๐๐๐
Siwezi mlaumu sana Jackline, mana story yake inaendana kidg na yangu
Mimi Tulipendna sana na mkaka flan ambaye huyo mkaka alikuwa na rafk ake na huyo rafk ake Tulikuwa Majirani nando Mwanaume wa kwanza kunitongoza, Wote tulisoma Pamoja Standard 3, bc nikadate na huyo mkaka Takriban miaka 12
Lakn lafk ake akiwa bado hajakata tamaa ya kunipenda, nilikuwa nikiumwa kwa haraka sana anafika Hospital nilipo lazwa, Nikiumwa hata kichwa, haraka alifika nyumbn lakn bado sikumkubalia, nilizidi kudate na rafk ake na sio yeye
2021 nikaumwa Ugonjwa wa MOYO nikalazwa Jakaya Kikwete Cardinal Institute (Muhimbili) Nikafanyiwa Operation da!! Yule Mpenzi wangu Akaniacha na wala hakuwahi kuja hospital wala Nyumban But yule anaye nipenda alikuja kila cku na cku zingne alivuta cku moja tu
Ndg zangu wakasema wanichangie Damu naye pia akaungana na ndg zangu kunichangia Damu.
Lakn bado sikumkubalia
Mwaka jana Mwishoni Nikajikuta nayatafakar Mengi aliyo yafanya kwangu da! Niliumia sana why nimemtenda hivo kwa muda mrefu toka tukiwa watoto wa darasa la 3
Basi nikajikuta naomba appointment bc tukakutana nikamwambia sorry kwa usumbufu wa miaka yote
NAKUPENDA NAOMBA TUOWANE TUWE MKE NA MME
Da!! Akasema Wewe ni msichana pekee niliye kupenda katika hii dunia na niliishi kwa kujipa moyo kuwa wewe ni mke wangu lakn Moyo wangu ukachoka sana baada ya wewe kutoka hospital bado ukawa unampenda mtu aliye kufanyia ukatili hivo ni Mwezi sasa toka niingie kwenye mahusiano na binti niliye muona ananipenda kwa dhati
Guys nililia sana na bado mpka leo naumia cz Kadi za mwaliko zimesha anza kugawiwa ANAFUNGA HARUSI DECEMBER
Pole kwa yaliyokupata, haya maisha ni fumbo, laiti tungejua yajayo huenda maisha yetu yangekuwa na raha, yule unaempenda hakupendi,. Usiye mpenda ndie anakupenda, kwa kweli maisha ni kitendawili, Mungu pekee ndie ajuaye mwisho wetu, SS niwakupokea tu
Admin mbona kuna siku una piga desh
Leo nimenunua bando kwa niaba ya Jacklin jamani ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ