Ilipoishia “Umenisaliti eeh?” Aliuliza Mosses kama kawaida yake alikuwa na tabia ya wivu sana
“Siwezi kukusaliti Mosses, unanijuwa vizuri. Sina ujanja kwako” nilisema lakini bila kumaanisha chochote na ilikuwa ndiyo mara ya kwanza nasema kitu mbele ya Mosses bila kumaanisha, katika nyakati fulani nilijikuta nikianza kujichukia Mwenyewe.
Mosses alitabasamu tuu kisha alinivuta na kunipiga busu, nami nilitoa tabasamu
“Tulale” alisema Mosses, Basi tulilala Usiku huo hadi kulipopambazuka. Endelea
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Siku iliyofuata ilikuwa ni Jumatatu iliyoanza kwa jua kali la mvua, nilimuaga Mosses, nilirudi nyumbani kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini japo Mosses aliniambia niache kazi, hata Mama aliniuliza
“Ulilala wapi na unaenda wapi?” Aliniuliza nikiwa tayari kwa ajili ya kutoka nyumbani kuelekea kazini
“Shikamoo Mama!!” Nilimsalimia kwanza
“Marahaba! Siku hizi unaamuwa tu kulala unapopajuwa wewe, kufanya unachowaza wewe si ndiyo?” Aliniuliza, niliutupa mkoba kwenye sofa kisha niliketi Mama akiwa amesimama
“Mama nililala Hotelini” Nilimjibu Mama huku Moyo ukinisuta “Na unaenda wapi?” Aliniuliza
“Naenda kazini” Nilimjibu Mama nikiwa ninafinya vidole vyangu, Basi Mama alisogea kisha aliketi kando yangu
“Jacklin ningekushauri usiende huko sababu ile ni kampuni ya Osman na Baba yake, kilichotokea baina yetu na ile Familia hakiwezi kuleta picha nzuri endapo tutaendelea kujihusisha na ile Familia” Alisema Mama
“Mama chochote kilichotokea hakina mahusiano ya moja kwa moja na kazi ninayoifanya kwao, hii ni kazi ambayo
tumeandikishiana mikataba labda waamuwe kuvunja mikataba” Nilisema
“Inatosha Jacklin, usiende huko Mwanangu” Alisema Mama lakini sikutaka kumsikiliza, moyo wangu uliniambia kuwa napaswa kuwa karibu zaidi na Osman japo yupo Hospitalini lakini kuwa ofisini kwake kungefanya moyo wangu utulie
“Mama najuwa ninachokifanya, usijali kila kitu kitaenda sawa” Nilisema kisha nilinyanyuka na kuondoka zangu.
Nilizongwa na mawazo kichwani, nilizongwa na hisia kali ndani ya moyo wangu, hisia ambazo zilinikosesha raha kabisa. Niliingia ofisini kwangu na kuanza kazi, nilitekeleza majukumu yangu ndani ya kampuni ya JM Motors. Siku hiyo Mzee Dhabi alikuja kwenye kampuni kukagua utendaji wa kazi unavyoendelea, hakujuwa kama Mimi ni mmoja wa wafanyakazi, aliponiona aliniuliza
“Wewe ni miongoni Mwao?” Akimaanisha hao Wafanyakazi “Ndiyo Baba” Nilimjibu tukiwa wawili tu ofisini
“Usiniite Baba, Niite Mzee Dhabi inatosha” Alisema Mzee Dhabi, hapo ndipo nilipokumbuka maneno ya Mama kuwa siyo busara sana kurudi kufanya kazi ndani ya kampuni ya Bilionea Dhabi kutokana na kilichotokea kati yangu na Kijana wake
“Mbona katika orodha ya Wafanyakazi wewe haupo, Osman alikuajili vipi?” Aliuliza Mzee Dhabi kisha aliketi, niliiyona chuki ndani yake, nilijawa na kigugumizi
“Mbona nilishajaza mkataba na kupewa hii Ofisi” nilijibu
“Hapana, Mimi ndiye Mwenye hii kampuni, Osman anasimamia sababu ni Kijana wangu! Sikutambui, hakuna mkataba ulio mbele yangu” Alisema Bilionea Dhabi tena kwa sura kavu sana
“Lakini mbona nilifanya usahili hapa na kujaza mkataba wa kazi iweje leo nisitambulike” Niliuliza
“Ni huruma ya Osman ambayo imemteketeza ndiyo iliyokufanya wewe kuwa hapa lakini hukupaswa kuwa hapa, nikiwa kama Mmiliki wa hii kampuni, sihitaji kukuona hapa kuanzia muda huu, kusanya kila kilicho chako” Alisema Bilionea Dhabi kama vile hakuwahi kuniona kabla, ujuwe nilichoka sana kuanzia roho hadi mwili, ningesema nini na aliyesimama mbele yangu alikuwa ndiye mmiliki wa kampuni hiyo
Nilifanya kama alivyosema tena akiwa amenisimamia, niliondoka kwenye kampuni ya JM Motors, nilijuwa chuki aliyoionesha Mzee Dhabi ilitokana na jinsi nilivyokataa kuokoa uhai wa Kijana wake japo dakika za mwisho niliufungua moyo wangu ila nilikuwa nimeshachelewa, Chozi lilinibubujika. Tayari mvua ilikuwa imeanza kunyesha.
Nilitembea kwenye mvua huku nikikumbuka siku ya kwanza kabisa ambayo Osman alinisaidia kwenye mvua, nilipofika nyumbani nilimsimulia Mama kile kilichotokea.
“Nilikwambia Mwanangu lakini hata Usijali sana sababu umesoma utapata kazi sehemu nyingine na Maisha yataendelea” alisema Mama
“Lakini Mama, natamani sana kulipa fadhila za Osman, amebadilisha Maisha yetu kutoka kwenye Umasikini, ameokoa Maisha yangu kutoka kifo, nilichelewa kuiyona thamani ya Upendo na huruma yake” Nilisema nikiwa nimeegemea ukuta
“Usijutie kwa chochote sababu anayepanga kila kitu ni Mungu pekee, Maisha lazima yaendelee” Alisema Mama, mara tulisikia honi ya gari. Mama alichungulia, aliona gari ya Mzee Dhabi ikiingia,
“Baba yake Osman anakuja” Alisema, nilikuwa nimelowa kutokana na ile mvua hivyo nilihitaji kubadilisha nguo haraka, nilielekea chumbani kwangu kubadilisha nguo, nilipotoka niliwakuta Mama na Bilionea Dhabi wakiwa wameketi hapana shaka walikuwa wakinisubiria Mimi.
Niliketi kwa utulivu sana, nilimtazama Bilionea Dhabi ambaye alikuwa ameongozana na Mke wake.
“Shikamoo Mama” Nilimsalimia Mama yake Osman ambaye hata hakuitikia, nilipata ishara kuwa hawakuja kwa lengo zuri, alianza Bilionea Dhabi kusema
“Tumekuja kwa ajili ya mambo mawili makubwa, moja ni kuchukua magari ambayo Osman alikununulia, mbili ni kuchukua nyumba hii ambayo mnaishi” Alisema Mzee Dhabi kwa sura kavu sana. Mama alishtuka sana
“Unasemaje?” Alihoji
“Pesa iliyotumika hapa ni pesa yangu Mimi, maamuzi ninayoyatoa yanatoka kwangu Mimi pia. Iwe mlipewa hati au hamkupewa Hati ya Hapa, mnaondoka na jeuri yenu” Alisema Bilionea Dhabi
“Baba tafadhali sana hebu fikiria tutakwenda wapi sisi? Fikiria kwa kipindi hiki tutafanya nini?” Alisema Mama akiwa analia, nilizidi kuumia ndani ya nafsi yangu
“Kwani zamani mlikuwa mnaishi wapi? Mlikuwa mnaishi vipi kabla ya kuanza kutumia pesa za Osman?” Aliuliza Bilionea Dhabi, nilikaa kimya bila kusema chochote sababu sikuwa na cha kusema
“Nionee huruma Mimi, Mimi ni mtu mzima nitaishi vipi Baba, fikiria hilo ina maana makosa ya Binti yangu yanatufanya tuwe maadui?” Aliuliza Mama akiwa katika hali ile. Ile ya kilio
“Siyo maadui tu bali ni maadui wa Maisha, adui wa Maisha ya Kijana wangu ni adui yangu pia, mna siku mbili za kuhakikisha mnahama hapa, gari zinaondoka sasa hivi” Alisema Bilionea Dhabi kisha yeye na Mke wake walinyanyuka, Mke wa Bilionea Dhabi hakusema chochote kama ambavyo Mimi sikusema chochote, Mama na Bilionea Dhabi ndio ambao walikuwa wakirushiana maneno
“Nakuomba tuonee huruma sisi, tutaenda wapi, siku mbili jamani Aaah” Mama alisema lakini hakukuwa na maelewano, Mzee Dhabi aliondoka bila hata kuchukua Funguo za Magari. Nililia sana, nilikumbuka kuwa Kulikuwa na pesa kwenye akaunti ya Benki zaidi ya Milioni 60 ambazo Osman alinipatia, kadi ilikuwa kwa Mosses, haraka nilimpigia na kuhitaji kuonana naye.
Alinielekeza alipo niliondoka na kumuacha Mama akiwa analia, nilienda kuonana na Mosses. Nilimsimulia kilichotokea, nilihitaji Milioni 40 ili kununua nyumba ya kuishi Na Mama ila majibu ya Mosses yalinigandisha damu, alisema Pesa zote aliziweka kwenye Biashara yake ya Mazao hivyo nisubirie ndani ya mwezi mmoja angenipatia pesa hizo.
“Lakini Mosses mbona hukuniambia kama unafungua Biashara? Unafikiria ndani ya huo mwezi Mimi na Mama tutakuwa tunaishi wapi?” Nilimuuliza Mosses
“Sasa Jacklin unafikiria pesa inahifadhiwa benki kama pambo la nyumba? Pesa ni lazima izunguke ili izae halafu Mimi ni Mwanaume nimefanya maamuzi ya kiume” Alisema Mosses, sura yake ilianza kutanda hasira. Sikutaka kuendelea kubishana naye nilimkubalia
“Sawa Mume wangu! Nakutegemea wewe kwasasa” nilisema “Usijali” alijibu Mosses, nilimuaga nikarudi nyumbani kwetu.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA MBILI Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx
13 Comments
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Thank you, hapo good,
Fupi sana Jamani dah
Anakumbuka shuka kumesha kucha
Mambo ni Fire ooooooh🔥🔥🔥🔥🔥 amechezea bahati ona anavyopata tabu…! Hivi dunia ya sasa wapo watu kama kina jack maaaana oh mie weeee mapema na kwa haraka sana ningemkubalia osman I don’t care na mahusiano yangu🤪🤪👌🏼👌🏼👌🏼👌🏼
Unyama liwaya zuri
Kwann hamna comment ya voice note jmn duuh ila admin endelea ubaya ubwela🔥🔥🔥🔥🔥
Kilanga koma
🤣ukiskia mtot kautak ndy huku saaa 🤣kibur hakisaidii kitu jack na kibur chak cha uzima xhek xx🤣👌
Ya leo umetuonea fupi sana..
Au kwasababu ya utamu?
Ivi mnaniruhusu nmtukane Jack maana nnavompatia hasira jaman 🤨😠
Jaman jack amazingatia mno mapenz kuliko maokoto
Shida yangu afee tuu uyo binti
Jack chan🤔🤔