Ilipoishia “Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo Machoย angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisemaย Dokta Simon
“Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….Twendeย Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra,ย waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta Simonย
Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman,ย aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa.ย Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuonaย Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, Mwanmkeย ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio.ย Endelea
SEHEMU YA KUMI
“Zahra?” Aliita Osman akiwa anaendelea kumuangalia Zahraย ambaye alikuwa akitembea taratibu kuelekea kilipo kitandaย alicholala Osman, alitikisa kichwa kuashiria kuwa alikuwa niย Yeyeย
“Baba! Huyu ni Zahra?” Osman alimuuliza Baba yakeย
“Ndiyo Osman huyu ni Zahra” Alijibu Mzee Dhabi, Choziย lilimbubujika Osman, Dokta Simon alikuwa akiangaliaย kilichokuwa kinaendelea kwa kutumia mlangoย
Zahra alisogea na kumkumbatia Osman akiwa analia, Osmanย aliweka mikono yake kwenye mgongo wa Zahra. Muda huo Mimi naย Mama tulikuwa tumeingia wodini, tulikuta hali hiyo. Ilitubidiย Mimi na Mama kusizi kwa dakika ili kuangalia kilichokuwaย kikiendelea, walipoachana Zahra aligeuka nyuma alimtazamaย Mzee Dhabi aliyekuwa akipepesa macho yake baada ya kunionaย Mimiย
Macho yangu yaligongana na Macho ya Zahra, nilimtambuwa kuwaย ndiye Mwanamke aliyekuwa akiuendesha moyo wa Osman lakiniย nilijiuliza aliweza vipi kurudi tena katika Maisha ya Osman,ย roho iliniuma sababu alirudi wakati ambao nilikubaliย kumsaidia Osmanย
Osman alinitazama, ukimya ulitawala huku kila Mtu akiwaย kwenye taharuki ya kilichokuwa kinaendelea pale.ย
“Baba! Nimerudi” Alisema Zahra akiwa analia, jinsiย nilivyomtazama niligundua alikuwa na jambo zito lililomfikaย ambalo lilimrudisha kwa Osmanย
Nilihema sana nikihisi maumivu makali sana kifuani,ย niliondoka nikaenda nje ambako nilijikuta nikiwa nimekaa pekeย yangu usiku ule.ย
Mama hakuwa na neno la kuzungumza ilimbidi aangalie tuย kilichokuwa kinaendelea paleย
“Zahra” Osman aliita, mara moja Zahra alimgeukia Osman
“Ulikuwa wapi siku zote, nimekutafuta kila kona ya Dunia hiiย bila mafanikio yoyote” Alisema Osman, Zahra alidondosha choziย akasemaย
“Nisamehe Osman, najuta kwa Ujinga wangu, najuta sana.ย Nimerudi kukufuta chozi lako” Alisema Zahra kisha alipigaย magoti akiwa analia, hata Mama alidondosha chozi lakeย
“Niambie nifanye nini Osman ili uamini kuwa nimerudi kwaย ajili yako, nimekukosea sana” Alisema Zahra akiwa anaendeleaย kulia, Bilionea Dhabi alimsogelea Zahra na kumyanyua kishaย alimfuta chozi kwa kutumia mkono wake, akamwambiaย
“Osman anaumwa sana, hakuna tumaini la yeye kupona isipokuwaย kupata Figo na kumuondolea mfadhahiko” Alisema Mzee Dhabi kwaย sauti yenye kunong’oneza masikio ya Zahra, hii ilimshtua sanaย Zahra alimfuata Osman alipolala kisha akamwambiaย
“Utapona Osman” Zahra alimshika mkono Bilionea Dhabi wakatokaย ndani, walinipita mahali nilipokuwa nimekaa, walielekeaย ofisini kwa Dokta Simonย
“Baba kama kutoa kiungo changu kutamfanya Osman awe salamaย nipo tayari hata sasa hivi, pimeni figo zangu zikifaa mnitoe”ย Alisema Zahra mbele ya Dokta Simon na Bilionea Dhabi ambaoย walijawa na mshangao, chozi lilimtoka Bilionea Dhabiย
“Zahra!” Aliita Bilionea Dhabi kwa sauti ya Chini sana, Zahraย alitikisa kichwa ishara kuwa alichokisema ndicho alichoย kimaanisha.ย
Mzee Dhabi alimkumbatia Zahra kwa Uchungu sana, alikuwaย ameshakata tumaini, Ujio wa Zahra ulimfanya Osman arudiย katika hali ya kawaida hata ile hali ya kunitaja ilikata.ย Mama alimuuliza Osman kule Wodiniย
“Huyu Mwanamke ni nani?”ย
“Ni Mwanamke niliyampenda sana lakini alinikimbia na kwendaย Ughaibuni” Alijibu Osmanย
“Osman Mwanangu, Jacklin amekuja kwa ajili yako, yupo tayariย kufunga ndoa na wewe” Mama alisema kwa uchungu sana, Osmanย alitikisa kichwa chake ishara ya kukataa huku akisemaย
“Jacklin hanipendi Mama, hawezi kukubali nimuowe”ย
“Tafadhali sana Osman, Jacklin anakupenda na yupo tayari”ย Alisema tena Mama wakati huo Mimi nilikuwa ninachunguliaย mlangoni, niliumia sana. Sikuona umuhimu wa kubakia paleย Hospitali niliondoka zangu. Mama alijitahidi sanaย kumbembeleza Osman lakini haikusaidia, kilichomtesa Sana Mamaย yangu ni ule wema ambao Osman alitutendea na jinsi ambavyoย Mimi niliulipa wema huo kwa ubaya sana, Mama alilia sana hadiย Mzee Dhabi aliporudi akiwa ameambatana na Dokta Simon naย Zahra, Mzee Dhabi alimwambia Mama yanguย
“Nashukuru kwa msaada na Mchango wako Mama Jacklin lakiniย kwasasa wewe nenda”ย
“Lakini Mzee Dhabi…” Mama alikatishwa na Mzee Dhabi kishaย alipewa ishara ya kuondoka, chozi lilikuwa linamvuja Masikiniย Mama yangu, aliondoka zake.ย
Mama alilia njia nzima hadi anafika nyumbani nguvu zilikuwaย zimemuishia, bahati nzuri nilikuwa sebleni. Nilipomuonaย Nilimkimbilia na kumdaka asianguke, mwili wake ulikuwa waย moto sana, jasho lilikuwa likimtoka, sikupata kumuona Mamaย akiwa katika hali hii hata siku moja, nilimlaza kwenye Kochiย nikawasha Feni ili apate ubaridi kisha niliketi pembeni,ย ukimya ukatawala huku nafsi yangu ikiwa imejaa majuto makubwaย sana, niliamini hali ya Mama ilitokana na makosa yangu.ย
“Jacklin” Mama aliita kwa Maumivu makali kisha alisemaย
“Tumechelewa lakini Mama yako nakupenda sana, Dunia nzimaย inaweza ikakuona mbaya lakini Mama yako nitahangaikaย kukusafisha. Osman amekataa kufunga ndoa na wewe” Alisemaย Mama huku chozi likimbubujika, kusema ule ukweli niliumia mnoย ndani ya nafsi yangu.ย
Moyo wangu nilishaufungua kwa Osman lakini niliufungua nikiwaย nimechelewa, nilijuwa Zahra ndiye aliyeharibu kila kitu,ย nilimyanyuka na kuondoka nyumbani kwa hasira na maumivuย makali, sikutaka kujuwa kuhusu Hali ya Mama tena, kichwaย changu ni kama kilijaa moshi mkali sana.ย
Nakumbuka ilikuwa ni majira ya saa 6 Usiku, nilimpigia simuย Mosses, zaidi ya mara sita mara ya saba ndio alipokea simuย yangu ikionesha kuwa alikuwa amelala. Aliniuliza nataka nini?ย Nilimwambia nahitaji kuonana naye, aliniambia niende kwake,ย nilianza safari ya kuelekea huko Usiku huo.ย
Nilipofika kwa Mosses kuna hali nilianza kuihisi ndani yaย nafsi yangu, niliona kabisa mapenzi kwa Mwanaume huyoย yalianza kuondoka ndani yangu, niliigiza tu na kumwambia kuwaย nammiss sana ila ukweli ni kwamba akili yangu ilikuwa kwaย Osman, kila nilipomfikiria Osman nilijikuta nikiumia tenaย kibaya zaidi nilipofikiria kuwa Zahra amechukua nafasi yanguย ndani ya moyo wa Osman ndiyo nilizidi kupagawa, hali hiiย Mosses aliiona kwangu kwasababu mara nyingi nilikuwa nikitokaย kifikra akaniulizaย
“Unawaza nini? Haupo kabisa” Aliuliza Mosses, huwezi aminiย tulikuwa katikati ya tendo lakini akili yangu hata haikuwaย hapo, Mosses alishuka kisha alielekea Bafuni aliporudiย alihitaji majibu kutoka kwangu.ย
“Sijui Mosses! Najikuta tuu” Nilimjibu nikiwa ninavuta Shuka,ย kweli mapenzi yanaumiza sana Aisee kumbe Osman aliumia hivi?ย Sikuwahi kuumia kama ambavyo nilikuwa naumiaย
“Umenisaliti eeh?” Aliuliza Mosses kama kawaida yake alikuwaย na tabia ya wivu sanaย
“Siwezi kukusaliti Mosses, unanijuwa vizuri. Sina ujanjaย kwako” nilisema lakini bila kumaanisha chochote na ilikuwaย ndiyo mara ya kwanza nasema kitu mbele ya Mosses bilaย kumaanisha, katika nyakati fulani nilijikuta nikianzaย kujichukia Mwenyewe.ย
Mosses alitabasamu tuu kisha alinivuta na kunipiga busu, namiย nilitoa tabasamuย
“Tulale” alisema Mosses, Basi tulilala Usiku huo hadiย kulipopambazuka.ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI NA MOJA Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย
ย ย
14 Comments
Dah fupi sana admin tuma mbili Leo Jana hukutuma hii pumz ya mwisho ni ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Waoooow ๐ฅฐ๐ฏ
Admin nyingn jmn ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Admini hii ni ya jana bado ya leo
Atleast sasa nimeanza kufurahi zahra kuwepoo
Jana hujatumia na leo ndio imeishia hapa
Admin umerudia mbn ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญ๐ญila ๐คฃjack kaulambaaaaaaa akome ingekua mm toka kitamb san nihsaolewana huyoooo osman๐คฃhata hila kusem yy ungekuta nishamtongoza zangu๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐
Hiyo ndo dawa ya wanawake kama kina jacklin….๐
Akomee huyu dada ..pumbaf
Adimin unasikia oja za ndugu zako tuma nyengne
Kusema ukwel j kayatimba hapo
๐๐ Lakini atajua mwenyew cz aliyataka
Leo n 11 jamn
admn vp ten tuma ya 11 Leo bwan
Admin umezinguwa see ya 11 pumzi ya mwisho hujatuma ,