Ilipoishia “Ndiyo! Unapaswa kukubali kuolewa na Osman ili apone naย afanyiwe upasuaji wa kupandikiza figo” Mama alirudia kauliย yake, akili yangu ilihama na kumuwaza Mosses, manenoย aliyoyasema wakati naondoka kwake, achilia mapenzi yanguย kwakeย
“Mama naweza vipi kuolewa na Osman, siyo chaguo langu lile,ย wala siyo aina ya Mwanaume ninayemtaka katika Maisha yangu,ย Mama nina Mtu wangu….Siwezi” Nilisema huku nikiwa ninalia,ย chozi lilikuwa likinivuja. Endeleaย
SEHEMU YA TISA
Aliingia Bilionea Dhabi, alitukuta tukiwa katikati yaย maongezi yetu. Mzee Dhabi aliponiona alitabasamu tuu, alikuwaย ameongozana na Mke wake ambaye ni Mama Mzazi wa Osman,ย Alinisogelea kisha aliniambiaย
“Jacklin! Hujakosea, upo sahihi, ni ngumu sana kuolewa naย Mwanaume ambaye hayupo ndani ya moyo wako, upo sahihi sababuย huwezi ndiyo maana uliondoka jana Usiku. Lakini Jacklin, hebuย tazama macho ya Mama yake Osman, ona lile chozi kwanza”ย Niligeuza macho yangu kumtazama Mama yake Osman, Ni kweliย alikuwa akivuja mchoziย
“Analia kwasababu Osman ni Mtoto wake wa kipekee, hana Mtotoย mwingine kama ulivyo wewe kwa Mama yako, lile chozi ndiloย ambalo Mama yako alikuwa akilia wakati alipopoteza tumaini laย wewe kuishi. Unakumbuka kilichotokea, Mungu alimleta Osmanย katika Maisha yako, alipambana hata kutoa figo lake iliย upone, hakufanya kwa ajili ya mapenzi bali kwa huruma yakeย kwa Mama yako, ulilala Jacklin hukumuona Mama yako alivyokuwaย anahangaika hata kutaka kutoa figo lake akuwekee wewe”ย Bilionea Dhabi alizungumza maneno mazito sana ambayoย yalimfanya Mama ajiinamie akiwa analiaย
“Nakuomba sana Jacklin, okoa Maisha ya Mwanangu, hatuna Mtotoย mwingine zaidi yake, Osman ndiye Maisha yetu, kufa au kuponaย kwa Osman kunakutegemea wewe Jacklin” Alisema Mzee Dhabiย kisha alienda kuketi kando ya Mke wake, maneno yakeย yalinifanya nishindwe kuendelea kuketi pale sebleniย nilikimbilia chumbani kwangu. Ni kweli Osman alijitoa naย kuhakikisha Maisha yangu yanarudi, tumaini la Mama yanguย linarudi, leo yupo Kitndani na Mimi ndiye ninayepaswaย kumuamsha, Daaah roho iliniuma sana.ย
“Usilie Mama Jacklin, Binti yako ni Mtu mzima anajuwaย anachokifanya. Kama amekataa kumsaidia Osman hakuna njiaย nyingine tutaondoka naye kuelekea Dubai tukajaribu huko,ย ikishindikana basi haikuwa ridhki yetu kuwa na Osman” Alisemaย Baba yake Osman, Mama yake Osman alikuwa akilia huku akiwaย amejifunika na kitambaa alishindwa hata kusema chochote, Mamaย yangu alinyanyuka na kunifuata chumbani, alinikuta nikiwaย nimeshikilia simu yangu, alisogea kisha aliketi kando yanguย kwa upole sana alisemaย
“Jacklin Mwanangu! Nilikuzaa na kukulea katika Mazingira yaย kujuwa nini Maana ya utu na shida, pengine ndiyo nguvuย iliyomvuta Osman kuja kwenye Maisha yako, alikuja kama Masiaย akaokoa Maisha yako, leo amegeuka kikwazo cha furaha yako.ย Nikiwa kama Mama yako nakueleza jinsi ninavyojisikia Jacklin”ย Alisema Mama kisha alifikicha jicho lake moja ambalo lilikuwaย likimwaga chozi
“Moyo wangu umevunjika Jacklin, furaha imenitoweka kamaย Kizimikavyo kibatari wakati wa upepo Mkali, Jacklin Mama yakoย nimeumia sana. Siku Osman akiondoka hapa Duniani ndiyoย itakuwa mwisho wako kusikia sauti yangu, yule Kijanaย alirudisha tumaini kwenye moyo wangu, alinifanya nijisikieย amani sana lakini leo umeiondoa yote” Mama alisema,ย nilitamani kumjibu na Kumwambia kuwa kama nitaolewa na Osmanย basi Mosses atasambaza video zangu za faragha, hadi Mamaย anaondoka chumbani kwangu mdomo wangu ulikuwa mzito sana kamaย samaki aliyejaza maji mengiย
Niliangalia ujumbe ambao Mosses aliutuma, alikuwaย akinikumbusha kuwa endapo nitamuacha atasambaza hizo video,ย nilivujisha chozi machoni mwangu. Yalikuwa ni maumivu makaliย sana ambayo hata sikuwahi kuyahisi katika Maisha yangu.ย Nilipaswa kuokoa Maisha ya Osman kama ambavyo aliokoa yanguย ila ningefanya kitu gani? Kama video zitasambaa naweza hataย kujitoa uhai kukwepa aibu nzito lakini je Mama yangu Mzaziย akiziona video hizo naye atakuwa katika hali gani? Vipiย Familia ya Osman itajisikia vipi, ndio maana nasema kilikuwaย ni kipindi kizito na kigumu kwangu.ย
Mama aliporudi Sebleni hakuwakuta Baba na Mama yake Osman,ย aliangusha kilio kama kuna Mtu amefariki, nilishtuka naย niliumia sana. Nyumba ilikosa ile amani iliyokuwepo Mwanzo,ย ukimya ulitawala hakuna aliyetoa neno lolote zaidi ya sautiย za kufungwa na kufunguliwa kwa milango. Nilijitupa kitandaniย nikawaza sana nifanye jambo gani ili kumsaida Osman bilaย kuchukua uamuzi ambao ungesababisha kusambaa kwa video hizoย za faragha. Kadili nilivyokuwa natulia kitandani ndivyo pichaย ya tukio la kukataa kuvishwa pete na Osman lilivyokuwaย linajirudia katika akili yangu, nilikosa utulivu kama Mtuย anayesumbuliwa na mizimu, niliamka bado Mama alikuwaย akiendelea kulia, nikiwa kama Mtoto nilijivuta kwendaย kumbembeleza.ย
Nilimkuta akiwa amekaa chini ameegemea sofa, niliketi kwaย adabu na utulivu mkubwa sana, Mama alihisi ujio wanguย alitulia kimya huku akihema sana. Nilishusha pumzi zanguย kisha nilisemaย
“Samahani Mama najuwa nimekuvunja moyo ila..” Kabla hataย sijamaliza nilichokitaka kukisema Mama alinikatishaย
“Ishia hapo hapo Jacklin, Wazazi ambao Mtoto wao aliokoa uhaiย wako wameondoka kwasababu umekataa kuokoa uhai wa Mtoto wao,ย nimeonekana Mama mbaya sana, Mama mbinafsi ambaye hajaliย kuhusu Mtoto wa mwingine” Alisema Mama kisha aliendelea
“Kama Osman atakufa basi juwa ni kwasababu yako, hupaswiย kusameheka katika hilo Jacklin” Alimaliza kusema kishaย alinyanyuka na kwenda zake chumbani kwake, choziย lilinimwagika Mimi Jacklin niliona kila Kiti kipo dhidiย yangu, sikuwa na Mtu wa kunisemea kabisa.ย
Usiku ulipofika niliondoka nyumbani nilienda kulala Hotelini,ย nilihitaji muda wa kuwa peke yangu ili niweze kutafakariย mambo kwa umakini zaidi. Nilizima simu zangu ili nisipateย usumbufu wowote ule, hakuna aliyejuwa niko wapi, Si Mossesย wala Mama yangu niliyemwambia, nilitaka kutafakari ili nijuweย nafanya nini katika kipindi kigumu kama hiki.ย
Hali ya Osman haikuwa nzuri kabisa kule Hospitalini, alikuwaย kila azindukapo anataja jina langu tu, alikuwa anachomwaย sindano za usingizi ili kumtuliza. Familia ya Bilionea Dhabiย iliingia gizani, tumaini lao juu yangu liliondoka kabisa,ย wakiwa nyumbani kwao Mke wa Bilionea Dhabi alimwambia Mumeย wakeย
“Twende kwa mara ya mwisho kuzungumza na Jacklin kamaย atakataa kwa kinywa chake basi hatutokuwa na namna nyingineย bali kuondoka na Osman” Alisema kwa sauti ya Kimama iliyojaaย maumivu ya kumuona Mtoto wake akiwa kitandani na hana tumainiย lolote lileย
“Sasa hata kama tutafanya hivyo Mama Osman, Binti haweziย badili msimamo wake, hampendi Osman na hilo lipo wazi sana”ย Alijibu Baba yake Osman, Mara mlango uligongwaย
“Ingia” Alisema Bilionea Dhabi baada ya kumtambua aliyekuwaย akigonga, alikuwa ni Mlinziย
“Samahani Baba na Mama, kuna mgeni hapo nje anasema anahitajiย kuonana na Osman” Alisema Mlinzi huyo baada ya kuwa tayariย ameingia ndani, Mzee Dhabi aliangalia saa yake aliona niย mishale ya saa 4 za Usiku alimuuliza Mlinziย
“Huyo Mtu yupoje?”ย
“Mwanamke, mweupe” Alisema Mlinzi kisha alitabasamu tu baadaย ya alichotaka kukisema kuhisi hakina maana hapo mbele ya Mzeeย Dhabi na Mke wake lakini Mzee Dhabi alimuelewa Mlinziย akamrahisishiaย
“Mzuri Eeh” Basi mlinzi alitoa tabasamu zitoย
“Mh! Atakuwa Nani huyo!” Alisema Bilionea Dhabi kishaย alitafakari
“Utamjuwa vipi bila kumuona, Mlete” Alidakia Mke wa Mzeeย Dhabi. Mara moja Mlinzi aliondoka, dakika moja baadayeย alirudi akiwa ameambatana na Mgeni huyoย
Mzee Dhabi na Mke wake walisimama kwa Mshangao Mkubwa sanaย baada ya kumuona Mgeni huyo kisha Mzee Dhabi alisemaย
“Mlinzi nenda” Mlinzi aliondoka zakeย
- โขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขโขย
“Zahra?”ย
“Zahra?” Mzee Dhabi na Mke wake alisema kwa pamoja baada yaย kumuona Zahra mbele yao, Si unamkumbuka Zahra? Ni yuleย Mwanamke aliyechota kiasi kikubwa cha pesa na kutimkia zakeย Ughaibuni, alikuwa ni mpenzi wa Osman ambaye aliuteka moyo waย Osman miezi kadhaa iliyopita aliondoka na kusema kuwa anaย Mwanaume mwingine hivyo Osman asihangaike kumtafuta, tukioย hilo lilisababisha Osman kupata Mshituko na kukimbizwaย Hospitalini.ย
Zahra alishtuka kuwaona Wazazi wa Osman, alitetemeka kwa Hofuย
“Hebu keti” Alisema Mzee Dhabi, wote waliketi kisha Mzeeย Dhabi na Mke wake walitazamanaย
“Ni wewe Zahra au tunaota ndoto ya Mchana?” Aliuliza Mamaย yake Osmanย
“Ni Mimi Mama naomba msamaha wenu kwa kila kilichotokea,ย natamani kumuomba msamaha Osman na ndiyo sababu ya kuja hapa”ย Alisema Zahraย
“Unataka kumuomba Msamaha Osman?”ย
“Ndiyo Baba! Najuta kwa kila nilichomfanyia.ย
“Nifuate” Alisema Mzee Dhabi, walitoka ndani Bilionea Dhabiย na Zahra, waliingia kwenye gari ya kifahari ya Mzee huyoย kisha safari ilianza, Zahra hakujuwa alikuwa akipelekwa wapiย
“Baba tunaenda wapi?” Alihoji Zahraย
“Si umesema unataka kumuomba msamaha Osman? ”ย
“Ndiyo Baba”ย
“Tunaenda alipo Osman”
Usiku huo nilikuwa nimeamua jambo moja, kumsaidia Osmanย kwasababu alisaidia Maisha yangu, akili yangu iliniambia kuwaย Osman alikuwa mwenye huruma na mapenzi ya kweli kuliko Mossesย ambaye alianza kutishia kusambaza video zangu za Faragha.ย Niliondoka Hotelini nikaelekea nyumbani, Nilipochunguliaย ndani nilimuona Mama akiwa amekaa kando ya Mlango waย kuingilia ndani nilijuwa tu alikuwa akinitafuta japoย alinichunia, nilitabasamu sababu Mama yangu alikuwa ni Mamaย mwenye upendo wa Hali ya juu sana kwangu, nilifuangua geti,ย nilitupa macho upande wa kushoto nililiona lile gariย aliloninunulia Osman kwenye siku yangu ya Kuzaliwa, moyoย uliniuma sana.ย
Nilisogea alipo Mama kisha nilimwambiaย
“Mama nipeleke Hospitalini alipo Osman” Kauli yangu ilimfanyaย Mama anitazame mara mbili mbiliย
“Mama moyo wangu unaniambia tufanye haraka sana” Nilisemaย nikiwa kwenye hali ya Haraka, lilikuwa ni jambo ambalo Mamaย alikuwa akilisubiria. Haraka alikimbilia ndani akatoka naย mtandio, tulitoka tukachukua Tax kisha safari ya kuelekeaย Hospitali ilianza.ย
Upande wa pili, Baba Osman na Zahra walikuwa wanaingiaย Hospitalini, walisogeza gari kwenye maegesho kisha walielekeaย Wodini ambako Osman alikuwepoย
“Baba Osman anaumwa? Mbona umenileta Hospitalini?” Aliulizaย Zahraย
“Ndiyo Osman ni Mgonjwa sana ndiyo maana nimekuleta hapaย Zahra” Alijibu Baba Osman, walishuka kisha walielekea ilipoย wodi hiyo. Bahati nzuri walikutana na Dokta Simon ambayeย alikuwa akitoka wodini humo, alipomuona Zahra alishangaa sanaย
“Najuwa una maswali mengi Simon lakini hiyo ndiyo haliย halisi” alielezea Mzee Dhabi baada ya kuisoma sura ya Doktaย Simon ilivyokuwaย
“Lakini Mzee, Osman hapaswi kushtushwa na jambo lingineย mnaweza kumpoteza kabisa, kwanini aje leo?”ย
“Maswali yako Simon hayawezi kujibiwa kwasasa, nina imani naย hiki atakachokiona Osman” Aliesema Mzee Dhabiย
“Lakini sikushauri kabisa kwenda huko Mzee Kwasasa yupo Machoย angalau anajisikia vizuri mgesubiria kidogo basi” alisemaย Dokta Simon
“Mimi ni Baba yake Osman, najuwa nini nafanya Simon….Twendeย Binti” Alisema Mzee Dhabi akiwa amemshika mkono Zahra,ย waliingia wodini bila kusikiliza alichokisema Dokta Simonย
Kitendo cha kufungua mlango kilihamisha macho ya Osman,ย aligeuza na kuangalia aliposikia sauti ya Mlango kufunguliwa.ย Alitoa macho yake, alijaza hewa kwenye kifua baada ya kumuonaย Zahra Mwanamke ambaye alimfanya ayachukie Mapenzi, Mwanmkeย ambaye alimtafuta sana Ughaibuni bila Mafanikio.ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย
ย ย
9 Comments
https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J
Dah toa nyingine ata usiku wa leo๐ญ๐ญ
Nimepumua baada ya kumaliza kusoma
Dah naona kesho mbal tuendeleee hadith imejoga sasa apo kwa akili ya haraka haraka julieth akimuona zarha atagoma ten kumhudumia osman ๐ค๐ค๐คuwiiiiiiiiiiii hadith tam nyie ๐๐๐๐๐๐๐ค๐ค๐ค๐ค๐คNATAFTA MPENZ KAMA OSMAN๐ค
Lete mbili juzi uliruka
Mshtuko umuue osman wazazi wa osman wamfukuze jack moses amuache jack mama yake ammchukie hyo pumzi itakuwa ya mwsho
Mtunzi apewe maua yake ๐ ๐น
Jmn wanawake!!! ๐ค๐ค khaa
Sehemu ya nane IPO wapi