Ilipoishia “Yote yaliyo mema, mazuri na yenye uelekeo mzuri zaidi, mudaΒ siyo mrefu maono yangu yatadhihirika” Sikutaka kuendeleaΒ kumuuliza, nilimwambiaΒ
“Sawa Mama nasubiria hayo Mema, nipo chumbani kwangu”Β Nilisema kisha nilielekea Chumbani kwangu, tulikuwa tukiishiΒ Watu watatu tu, yaani Mimi, Mama na Mdada wa kazi. HadiΒ naondoka sikujuwa Mama na Osman walikuwa wamewasiliana naΒ kuambiana kuwa nilienda kwa Osman. EndeleaΒ
SEHEMU YA SABA
Ila ndani ya moyo wangu nilihisi amani sababu tayari nilikuwaΒ nimeshamuomba msamaha Osman, na pia nilikuwa nimeweka mamboΒ sawa kwa Mama yangu. Siku zilipita, niliendelea na kazi,Β Mapenzi yangu kwa Mosses yaliendelea bila tatizo lolote tenaΒ alikuwa akininyenyekea sana tofauti na mwanzo, kaziΒ ziliendelea kule kwenye kampuni ya Osman, niliendelea kupataΒ uzoefu huku ukaribu kati yangu na Osman ukizidi kuongezeka.Β Osman alikuwa akiumwa sana ila alikuwa akijikaza mno mbeleΒ yangu ila sura yake ilionesha wazi kuwa alikuwa akiumwa,Β sikutaka kumuuliza sana sababu kama ningekuwa na unuhimu waΒ kulijuwa hilo angelikuwa ameshaniambia muda mrefu.
Alinipeleka sehemu mbalimbali, ndani na nje ya Nchi,Β alinifundisha vingi sana Osman. Namna tulivyokuwa tumezoeanaΒ kama ikitokea umetuona kwa mara ya kwanza ingekuwa rahisiΒ kuhisi ni wapenzi, Osman alikuwa akijaribu kunionesha hisiaΒ zake lakini hakusema kwa kinywa chake, nakumbuka siku yanguΒ ya kuzaliwa alininunulia gari aina ya Cadilac, aliniandaliaΒ kila kitu kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa, nilimuarikaΒ Mosses kwasababu ndiye Mwanaume aliyekuwa akinipa furaha.Β
Mama aliniita pembeni, akaniulizaΒ
“Hivi Jacklin unatumia ubongo wako vizuri kuwaza?” AliulizaΒ kwa sauti ya Juu sababu kulikuwa na kelele za Mziki, wakatiΒ huo Watu ndio walikuwa wakifika nyumbani kwetu kwenye hiyoΒ sherehe ya siku ya kuzaliwaΒ
“Mama! Nimefanya kitu gani kibaya?” NilimuulizaΒ
“Mosses amefuata nini hapa? Hii ni sherehe yako wewe, OsmanΒ amefanya kila kitu bado unashindwa hata kumuheshimu?” AlisemaΒ Mama ilinibidi nishushe mzuka wanguΒ
“Hivi Mama kwanini tunaishi kwa kuhofia fulani atasema nini?Β Osman ni rafiki yangu, na Bosi wangu. Kuniandalia shereheΒ haimaanishi mimi na yeye ni wapenzi Mama, Nitasherehekea vipiΒ siku yangu ya kuzaliwa bila Mosses?” Nilimuuliza MamaΒ
“Huyo Mosses anajulikana na nani? Amekusaidia nini hadi hiviΒ sasa kama siyo kula pesa yako ambayo imetokana na Osman?Β Jacklin, hujui kilichopo kichwani kwa Osman na hujui kwaniniΒ aliandaa hii sherehe yako ya kuzaliwa. Unaiyona ile gariΒ pale? Ile ni zawadi kutoka kwa Osman, huyo Mosses wakoΒ anaweza kukununulia japo Pikipiki?” Mama alisema na nilionaΒ wazi alikuwa amepaniki.Β
“Samahani Mama” Nilisema, nilikuwa sipendi kumuona Mama yanguΒ akiwa katika hali ya kuhuzunika kisa MimiΒ
“Mwambie huyo Mosses aondoke hapa kabla Osman hajafika, OsmanΒ ni mfadhili wetu hivyo ni lazima tuheshimu hisia zake” MamaΒ alisema Maneno ya mwisho kisha aliondoka pale, aliniacha naΒ mawazo lukuki sana nikajiuliza maswali mengi ambayo sikuwa naΒ majibu yakeΒ
Nikiwa nimesimama alikuja Mosses akiwa ameshikilia glasiΒ yenye kinywaji, aliniulizaΒ
“Mama alikuwa anasemaje? Nimewaona kama mlikuwa mkigombanaΒ hivi” nilimtazama Mosses kisha nilitabasamu tu nikamwambia
“Hapana kuna jambo alikuwa ananielekeza ndio tukawaΒ hatuelewani, lakini usijali” nilisemaΒ
“Mlisema Sherehe inaanza saa moja usiku, sasa inakimbilia saaΒ mbili, anasubiriwa nani?” Aliuliza Mosses, nilikosa chaΒ kumjibu. Mara zilisikika honi za gari huko nje,Β
“Wageni hao hebu twende” Nilisema lakini Mosses alinishikaΒ mkono akanivuta pembezoni kwenye mnazi. Alitupa glasiΒ pembeni, akaanza kunila mate yangu. Nilishindwa kujizuiaΒ nikajikuta namba sapoti Mosses, eneo ambalo sisi tulikuwaΒ tumesimama lilikuwa na mwanga hafifu sana.Β
Wakati magari yanaingia sisi tulikuwa bize kupeana mate paleΒ kwenye mnazi, bahati mbaya Osman aliangalia tulipo japoΒ hakunitambua kutokana na lile giza. Alikuwa ameingia na BabaΒ na Mama yake, Zilipokuja kuwashwa taa zote ndipo tuliposhtukaΒ tukaacha ule mchezo, ila mashine ya Mosses ilikuwa imesimama.Β Tuligawana njia, mimi nilipitia upande wangu na Mosses upandeΒ wake, nilipowaona Wazazi wa Osman nilishangaa sana sababu waoΒ walikuwa Dubai au inamaana walikuja kwa ajili ya ShereheΒ yangu ya siku ya kuzaliwa tu au kulikuwa na jamboΒ lililowaleta pale? Nilisimama kwa sekunde kadhaa kabla yaΒ kujitokeza huku bado mawazo yakiwa yananizonga kichwaniΒ kwangu, sikuamini Sherehe yangu ya kuzaliwa ihudhuriwe naΒ Bilionea Mkubwa kama Baba yake Osman?Β
Nilipojitokeza sikuonesha dalili yoyote kuwa nilikuwaΒ nimetingwa na mawazo, nilienda kumsalimia Baba yake Osman,Β alikuwa akinipenda sana na mara zote alikuwa akisema natembeaΒ na kiungo chao japo alikuwa akisema kama utani ila ilikuwa niΒ kweli nilikuwa natembea na figo ya Osman, tulicheka pamoja,Β nilipogeuka nilikutana na Mama yake Osman naye alitabasamu,Β tulisalimiana vizuri sana, ilikuwa ni sherehe ndogoΒ iliyobadilika na kuwa kubwa tena yenye heshima sana hadi WatuΒ tuliowaarika walishangaa. Walinionesha mahali alipo Osman,Β alikuwa amesimama na rafiki zake, nilienda kumsalimia hukuΒ macho yangu yakimtafuta Mosses alipo, Osman alinikumbatiaΒ kisha alinishika mkono huku akiendelea kuniuliza maswali yaΒ hapa na paleΒ
Punde shughuli ilianza, Mama yangu sikumuona kabisa licha yaΒ kupepesa macho huku na kule. MC wa shughuli aliniita katikatiΒ ya Watu waliokuwa wamesimama, nilitembea taratibu sababuΒ nilivalia gauni refu lenye rangi ya Dhahabu. Nijisifie tuΒ maana ukisubiria kusifiwa hapa Duniani utazeeka, nilipendezaΒ mno.
“Leo ni siku nzuri na nyenye baraka kutoka kwa Mungu, nduguΒ yetu Jacklin leo ametimiza miaka 28. Bahati ilioje kwake niΒ kwamba sherehe yake imehudhuriwa na Bilionea ambaye ndiyeΒ Baba wa Osman ambaye pia ameandaa shughuli hii kwa ajili yaΒ Jacklin” Alisema MC kisha Watu walipiga makofi mengi sana,Β bado nilikuwa nikiangaza macho yangu kumtafuta Mosses, bahatiΒ nzuri nilimuona akiwa amesimama nyuma akiwa anaangalia tukioΒ lilivyokuwa likiendelea.Β
Nilitabasamu ili tu mambo yaende ila nilipoteza uwezo waΒ kujiamini kabisa, MC aliendeleaΒ
“Namkaribisha Osman Dhabi aje mbele atuambie siku ya leoΒ amemuandalia nini Jacklin” Makofi mengi yalipigwa, BilioneaΒ Mzee Dhabi naye alikuwa akifurahi pamoja na Mke wake hapoΒ ndipo nilipomuona Mama yangu akiwa amesimama kando ya familiaΒ hiyo ya Kitajiri, Mama alinipa ishara ya kukubaliΒ kitakachotokea pale, nilishindwa kumuelewa ni kwaniniΒ nikubali kwasababu sikujuwa kilichotaka kwenda kutokea. OsmanΒ alipofika karibu na Mimi alisemaΒ
“Wakati nakutana na Jacklin kwa mara ya kwanza nilimuona niΒ Mwanamke Msumbufu, asiyejali, mkorofi lakini nilivyokujaΒ kumuelewa niligundua ni Mwanamke wa tofauti sana” AlisemaΒ Osman, wote walipiga makofi hata Mimi nilitabasamu maanaΒ nilikumbuka jinsi nilivyokutana na Osman kuanzia kwenyeΒ Pikipiki hadi kwenye mvua, nilicheka.Β
“Kwa muda mfupi anenitengenezea kumbukumbu zisizofutikaΒ katika Maisha yangu, leo kwenye siku yake ya kuzaliwaΒ nilifikiria ni zawadi gani naweza kumpa ili afurahi, nilionaΒ nimnunulie gari aina ya Cadilac escaled ya Mwaka 2021”Β Shangwe ziliibuka pale, makofi yalipigwa sanaΒ
“Gari hii ina thamani ya Milioni 600, ni zawadi ambayo moyoΒ wangu umeridhia kwake lakini pia napenda kumuomba Jacklin”Β Alisema Osman kisha alipiga magoti akanitazama, nikaiyonaΒ ishara kuwa anataka kunivika pete kidoleni, nilishtukaΒ nilipomuona Akitoa pete kwenye mfuko wa koti lake la sutiΒ
“Nipe ruhusa niwe Mumeo Jacklin, maneno haya si rahisi MtotoΒ akayazungumza mbele ya Wazazi wake lakini nimeshindwaΒ kufikisha hisia hizi kwako, nimeona leo ni wakati sahihi waΒ kufanya hivi” Nilimtazama Osman kama vile nataka kumuulizaΒ maswali ambayo hata sikujuwa niulizaje, nilipogeuza machoΒ nilikutana na Mosses, Mama na Wazazi wa Osman, wote walikuwaΒ kimya kusikiliza nitasemaje. Niliishiwa nguvu jamani
Osman alinishika mkono akawa ananivisha ile pete taratibu,Β nilikuwa kama Mgonjwa wa koma, ghafla nilishtuka nikasemaΒ
“Hapana Osman, siwezi” nilisema kisha niliivua ile peteΒ nikamtupia Osman, Watu walijawa na mshangao mkubwa sana,Β Chozi lilimbubujika OsmanΒ
“Jacklin tafadhali, fanya kwa ajili ya Wazazi wangu nakuomba”Β Alisema OsmanΒ
“Siwezi Osman, siwezi kuidhurumu nafsi yangu, siwezi kuuzaΒ upendo wangu Osman, unajuwa fika nina Mtu wangu” Nilisema,Β Watu walikuwa kimya sana kusikiliza maongezi yetuΒ
“Jacklin, hili ni ombi langu kwako, baada ya hapa sitakuwa naΒ uwezo wa kukuomba chochote tena, tafadhali” Alisema OsmanΒ kisha aliushika mkono wangu ili anivishe tena ile pete,Β nilimsukuma kisha niliondoka pale, nilikimbilia nje kabisa,Β Mosses alinifuata huko nje, tulichukua Bajaji na kuondokaΒ pale nyumbani. Nilipomsukuma Osman alianguka, hali yakeΒ ilibadilika alikimbizwa Hospitalini, Hekaheka ilikuwa kubwaΒ pale nyumbani, Watu walikuwa wakijiuliza kulikoni, Mzee DhabiΒ alihangaika kwa ajili ya Mtoto wake. Muda mchache watuΒ waliondoka pale nyumbani, alibakia Mama akiwa analia tu, namiΒ nilikuwa nikilia ndani ya Bajaji, siyo kwamba nilikuwaΒ simpendi Osman ila tayari nilikuwa na Mwanaume niliyempendaΒ ambaye ni Mosses.Β
Nilikuwa nimeshabadilisha hali ya hewa, nililia sana nikiwaΒ ndani ya Bajaji, Mosses alinibembeleza hadi tulipofika kwake.Β
Tukiwa chumbani aliniulizaΒ
“Nini kinaendelea Jacklin?” Aliniuliza akiwa amekaa pembeni,Β chozi lilikuwa likinibubujika, nilimuwaza Mama yangu,Β nilijuwa nimemkosea sana.Β
“Mosses, hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Osman,Β nimeshangaa ameita wazazi wake kwenye sherehe yangu yaΒ kuzaliwa istoshe hakuwahi kuongelea kuhusu mapenziΒ nimeshangaa alipotaka kunivesha pete” Nilisema huku nikiwaΒ najifuta mchozi, simu yangu ilikuwa ikiita sana na aliyekuwaΒ akinipigia alikuwa ni Mama yangu, niliamuwa kuizima kabisa.Β
“Yule ndiyo amebadilisha Maisha yenu?” Aliniuliza “Ndiyo Mosses, ni yeye”
“Haiingii akilini Mtu aje tu atake kukuvesha pete, lazimaΒ kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kati yenu”Β
“Mosses tafadhali naomba uniamini, nisingelimkimbia kwa ajiliΒ yako, ile ni familia ya kitajiri sana. Kama siyo weweΒ ningelikuwa nimekubali lile jambo ila upo wewe MwanaumeΒ nikupendaye Mosses” nilisema kisha nilimuona MossesΒ akitafakari jambo, kilio changu kilikata nikawaza labdaΒ alikuwa anataka aniacheΒ
“Hebu tuliza akili yako Jacklin, kesho asubuhi tutaongeaΒ jambo moja” Alisema Mosses, nilipata muda wa kupumzika.Β
β’β’β’β’β’β’β’β’Β
Mama yangu hakulala, hakula chakula, alikesha kunipigia simuΒ bila kupokea majibu yoyote. Usiku ulikuwa mwingi ilimbidiΒ aingie ndani, Usiku huo taarifa kutoka maabara zilisema haliΒ ya Osman inaweza kuwa mbaya zaidi baada ya miezi mwiliΒ kutokana na figo lingine kufanya kazi kwa kiwango kidogoΒ sana. Taarifa hii ilikuwa mbaya na isiyopendeza kabisa, MzeeΒ Dhabi na Mke wake walihuzunika sana, walimuuliza Dokta SimonΒ
“Kwanini hukusema kabla Osman hajachukua uamuzi wa kuondoaΒ figo moja?” Ilikuwa ni sauti yenye maumivu sana iliyotokaΒ kwenye kinywa cha Bilionea DhabiΒ
“Niliongea naye kabla ya kuchukua uamuzi huo, cha ajabuΒ alimuhamisha mgonjwa na kwenda kufanya upasuaji India,Β aliniomba nisiwaambie chochote kwasababu alikuwa na uhakikaΒ wa kupata figo haraka iwezekanavyo. Tukio lililotokea leoΒ siyo tu limemletea mshituko bali mfadhahiko mkubwa ndaniΒ yake” Alisema Dokta Simon, Chozi lilimbubujika Mama yakeΒ Osman, alikuwa ndiyo Mtoto wao wa pekee hawakubatika kupataΒ Mtoto mwingineΒ
“Laiti kama mioyo ingekuwa inahamishika basi ningehamishaΒ moyo wa Osman, mara zote tuliamini tukimpa pesa nyingi MtotoΒ wetu itampa jeuri na kuondoa mapenzi katika Moyo wake lakiniΒ Osman amekuwa dhahifu sana linapokuja suala la Mapenzi” MzeeΒ Dhabi alimtuliza Mke wakeΒ
“Dokta inahitajika huduma gani kwa Mtoto wangu, HospitaliΒ gani Duniani, Pesa Kiasi gani? Nipo tayari kutoa nusu yaΒ utajiri wangu kwa ajili ya Osman” Alisema Mzee Dhabi, DoktaΒ Simon alimwambia Mzee DhabiΒ
“Unaweza ukapata figo, ukapata kila kitu lakini huweziΒ kuuondoa mfadhahiko alionao Mwanao. Kitu cha kwanza niΒ kumuondolea mfadhahiko Osman ili kumuandaa kwa ajili yaΒ upasuaji wa kupandikiza figo” Alisema Dokta SimonΒ
“Pesa siyo tatizo Simon, niambie hiyo huduma inapatikanaΒ Hospitali gani Duniani, kiasi gani kinahitajika?” AliulizaΒ Bilionea Dhabi, walionesha kumpenda sana Mtoto wao.Β
“Mfadhahiko huondolewa na kilichosababisha mfadhahiko,Β tumaini alilokuwa nalo ndilo lenye kuuondoa huo mfadhahiko waΒ Osman”Β
“Unamaanisha nini?”Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ
12 Comments
Duh ya moto sana.
Duuuuh….. Si mchezooooππ₯
Hadithi tamu Sana
Pumzi ya mwisho kipande kimoja Ni kitamu sana, ladha haiishi, ongeza viwe viwili kwa siku chief
ππ mpka kieleweke
Huyo dada anatia hasira π€π£π hv ana akili zote mpuuzi huyoooo
Aise imenigusa sana dah
Hadithi tamu balaaa
Kwan adinimi story unatowa wap mbon kama muvi iv tunaangalia jamani
Admin nikutmie shingap unitmie vipande vyote
πππ
Nzurii