Ilipoishia “Alipotoka Hospitalini Osman alikuwa mwenye mawazo na maumivu makali sana, alipigiwa simu na Wazazi wake na kumtaka aachane na mpango wa kutaka kutoa figo kwani haitokuwa na faida yoyote kwake, Wazazi wa Osman waliamini kuwa Osman alikuwa akitaka kutoa figo kwa ajili ya Mapenzi, walinuonya sana kwa kile kilichomtokea kwa Zahra ila Osman aliwaambia Wazazi wake kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Mimi bali ni ubinadamu tu wa kutaka kuhakikisha afya yangu inaimarika.
Osman aliwasiliana na Hospitali nyingine ambayo ingefanya operesheni ya kupandikiza figo kwenye mwili wangu, kutokana na utajiri alionao aliweza kupata Hospitali Nchini India, tulisafiri kwenda huko. Osman alishauriwa na kuambiwa kila kitu kiafya kuhusu uamuzi wake. Endelea
SEHEMU YA NNE
alikubali kutoa figo.
Baada ya siku tatu, tulifanyiwa Operesheni, Osman aliondolewa Figo yake ambayo ilikuwa safi kabisa, Mimi niliondolewa Figo zangu ambazo zilikuwa na matatizo kisha ilipandikizwa Figo ya Osman katika mwili wangu. Mama yangu alikuwa ni Mtu wa kulia na kuomba Mungu kila jambo liende sawa, siku zilienda, unafuu ulianza kuniingia, hata Osman unafuu ulimuingia, sikujuwa kilichokua kimetokea.
Ilipita miezi miwili tukiwa Hospitalini India, hali yangu ilizidi kuimarika siku hadi siku hatimaye nilipona kabisa, Mimi na Osman tulipona, tuliruhusiwa tukarudi Nchini. Tulifikia kwenye jumba la kifahari sana ambalo Osman alitununulia, Maisha yalibadilika sana kwetu, Osman alitufungulia Biashara kubwa. Nilisimuliwa kila kilichotokea, niliuona upendo wa Osman, pia niliuona upendo feki wa Mosses
Siku moja Osman alinipeleka kwa Wazazi wake huko Dubai, Walifurahika kuniona. Walitupokea kwa shamra shamra sana, familia yao ilikuwa ni familia ya kitajiri sana.
“Karibu Jacklin katika Familia yetu” Alisema Baba yake Osman tukiwa tunapata chakula
“Asante Baba, nafurahika kuwaona” nilijibu
“Usijali Jacklin, wewe ni damu yetu sababu una kiungo cha Mtoto wetu, naona hata sura ya Osman imeng’aa kwa furaha, natumaini hautofanya kama alichokifanya Zahra” Alisema Mama yake Osman, nilishtuka kidogo sababu nilikuwa simjui huyo Zahra, nilimtazama Osman akanipa ishara ya kutabasamu tu kuwa atanieleza kila kitu, kilichonishangaza ni yale maongezi yao, ilionesha kuwa wao walikuwa wakijuwa kuwa Mimi na Osman ni wapenzi wakati hatukuwahi kuongelea kuhusu Mapenzi.
Baada ya Chakula tulioneshwa chumba cha kulala, kilikuwa ni chumba kimoja tu tulale mimi na Osman, tulipofika Chumbani nilimuuliza Osman
“Zahra ni nani?” Nilimuuliza nikiwa nimekaa kitandani, yeye alikuwa ameketi juu ya kiti.
“Mwanamke niliyempenda sana, aliyenifanya nikalia na kupoteza kila kitu katika Maisha yangu” alisema Osman
“Kwahiyo ulinisaidia ili unitumie Osman, umewaambia nini Wazazi wako na kwanini waseme maneno yale? Lengo lako nije kuonekana mbaya mbele za macho yao wakati unajuwa hali halisi kuwa nina mpenzi?” Nilisema japo Mosses alikataa kutoa figo na kumjibu Mama vibaya, niliamini pengine kuna jambo hawakuelewana tuu ila bado alikuwa akinipenda nami nilikuwa nikimpenda.
“Una mpenzi? Aliyekuacha ufe wakati alikuwa na uwezo wa kukusaidia?” Alisema Osman akiwa anakaa vizuri
“Yeye alikataa ila wewe umenisaidia ili unitumie Osman, huna tofauti na mtu anayetoa msaada na kusubiria kulipwa. Mosses ni Mwanaume anayenipenda sana pamoja na yote yaliyotokea” Nilisema nikiwa ninajilaza
“Samahani Jacklin, usiwachukie Wazazi wangu wala usiumie, sikukusaidia ili niwe na wewe ila samahani sana kwa kukufanya uhisi hivyo” Alisema Osman, sikumjibu chochote kile, niliona alikuwa akinipenda sana ila sikuwa na hisia za kimapenzi na Osman, moyo wangu ulikuwa kwa Mosses. Tuliishi Dubai kwa wiki mbili, tulikuwa tukiongea mbele ya Wazazi wa Osman lakini tukiwa wawili kila mmoja alikuwa kimya, tulirudi Nchini, nilifurahika sana kuonana na Mama yangu kwa mara nyingine tena.
“Maisha ya huko yalikuwaje Mama” Aliuliza Mama yangu, wakati huo Osman alikuwa ameshaondoka
“Mazuri sana Mama, nimefurahi sababu ilikuwa ndiyo mara ya kwanza naenda nje ya Nchi” Mama alinikumbatia akaniambia
“Muweke Osman katika Maombi yako kila siku Mwanangu, jitihada zake zimeokoa Maisha yako, usilisahau hilo” Alisema Mama
“Sawa Mama ngoja nikapumzike” Sikutaka kumwambia chochote Mama sababu niliamini yupo upande wa Osman, nilielekea chumbani kwangu, ilikuwa ni nyumba nzuri ambayo sikuwahi kuiota katika Maisha yangu, umasikini tuliupa mkono wa kwaheri.
Nilitazama nje niliiyona gari yangu aliyoninunulia Osman, nilikumbuka kipindi ambacho nilikuwa natembea kwa mguu, nilikumbuka siku ambayo homa ilinianzia jinsi nilivyokuwa nikitetemeka kwenye baridi, jinsi Osman alivyojitolea kiungo chake ili kuokoa Maisha yangu, nilimshukuru kwa kumtumia ujumbe lakini hakujibu kabisa.
Siku iliyofuata nilipigiwa simu na Mmoja wa Wafanyakazi wa kampuni ya JM Motors kuwa natakiwa kuanza kazi, japo nilikuwa na uchovu ila kazi hiyo ilikuwa ni ndoto yangu, pia niliona ni bora nifanye kazi kwa Osman ili kumshukuru kwa ukarimu na msaada wake, basi nilijiandaa kisha nilielekea kazini kwa kutumia usafiri wa kukodi maana nilikuwa sijui kuendesha gari. Nilipokelewa vizuri sana, nilioneshwa ofisi yangu, ilikuwa ni ofisi iliyotengenezwa kwa ajili yangu, nilikuta picha yangu ukutani
Nikitabasamu sababu nilijuwa kuwa ni Osman ndiye aliyefanya hivyo, nilianza kazi rasmi katika kampuni ya JM Motors, mahusiano yangu na Osman yalipungua kwa kiasi kikubwa, alikuwa akinisalimia tu kisha kila Mtu alikuwa akiendelea na Maisha yake. Siku moja nilihitaji Mafaili kutoka kwenye ofisi yake, bahati mbaya hakuwepo ofisini, nilizungumza na Msaidizi wake akaenda kunichukulia Mafaili hayo.
Aliponiletea nilianza kazi yangu, lilikuwa ni faili la Watu waliokuwa wanasubiria mzigo wa Magari ambao ulitakiwa kuingia kesho yake, nilitakiwa kuhakiki taarifa zao, wakati naendelea kufungua mafaili hayo nilikutana na picha ya Mwanamke mzuri sana, tena Mzuri kuliko Mimi, yaani mzuri hadi ukimtazama unagundua kuwa alikuwa mzuri kuliko mfano. Sikujuwa Mwanamke huyo alikuwa akiitwa nani, nilipogeuza nyuma ya picha nilikutana na jina limeandikwa “ZAHRA”
Nilishusha pumzi zangu kisha niliigeuza tena ile picha, ooh! Huyo Zahra kumbe ndiye huyu? Anastahili kuugalagaza moyo wa Osman,,hakika ni mzuri sana. Nilisema na Moyo wangu, niliirudisha picha nilipoitoa.
Katika hali ambayo sikuielewa nilijikuta nikikosa raha hata kufanya kazi nilishindwa nilihisi moyo unaniuma, ilikuwa ni mishale ya saa saba Mchana, nilimuaga Mtu wa Usaidizi pale kazini kisha niliondoka, nilifanya safari kwenda anapoishi Mosses maana simu yake ilikuwa haipatikani, nilitumia usafiri wa gari ya kukodi, nilipofika niligonga mlango kwenye chumba cha Mosses, alikuwa ni Kijana mwenye Maisha ya kati tu. Nilisubiria mlango ufunguliwe, aliyefungua alikuwa ni Mosses mwenyewe, alinishangaa kisha alitabasamu, dimpozi zake zikajiachia. Mosses alikuwa anajuwa kuugalagaza moyo wangu vile atakavyo, pamoja na yote kukataa kunitolea figo bado nilikuwa nikimpenda na sikufikiria hata siku moja kama ningelimpenda Mwanaume mwingine, alinikumbatia akiwa amevalia taulo tu. Mwili ukaanza kunisisimka kama napandwa na sisimizi hivi, mikono ya Mosses ilikuwa kama sumaku vile yaani hata anishike wapi alikuwa akinipandisha ashki zangu.
Nilivuta hewa kisha nilimwambia Mosses
“Nimekumiss sana Mosses” nilisema nikiwa nimemkumbatia kwa nguvu, nilikuwa na hisia kali sana kwa Mosses
“Nimekumiss pia Jacklin, pole kwa matatizo yaliyokupata, siamini kama bado unaishi, nilijuwa umeshakufa ndio maana niliamuwa kubadilisha namba” Alisema Mosses akiwa ananipiga busu shingoni, nilifumba macho kwa utamu wa Busu, nilikuwa nusu Chizi kwa Mwanaume huyu
“Naishi kwa ajili yako Mosses, kama siyo wewe ningelikuwa nimekufa zamani sana ila nguvu ya Mapenzi niliyonayo juu yako ndiyo iliyonipa uhai nikaamka tena” Nilisema pia, aliniachia akanitazama jinsi nilivyokuwa nimependeza ilitosha kumfanya Mosses atambuwe kuwa maisha yangu yalikuwa yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana.
“Nakupenda sana Mosses” Nilimwambia, naye alirudisha jibu zuri sana
“Umenipa sababu ya kuendelea kuishi Jacklin, niliposikia kuwa huwezi kupona nilihisi unakufa, nilitamani kufanya kila kitu ili niokoe uhai wako” Alisema Mosses, nilijuwa ni uwongo lakini nguvu ya mapenzi iliniambia kuwa anachokisena Mosses kina ukweli
“Tuachane na hayo Mosses naomba tuongee ndani” Nilisema kisha tuliingia chumbani kwa Mosses. Nilitazama jinsi chumba cha Mosses kilivyo, sikupenda aendelee kuishi hapo, nilikuwa na uwezo wa kubadilisha Maisha ya Mosses sababu nilikuwa nikimpenda sana.
“Mosses kwasasa nafanya kazi, Maisha yangu yamebadilika sana. Sitopenda uendelee kuishi hapa nitakupangia sehemu nzuri ya kuishi” Nilimwambia Mosses
“Jamani kweli Jacklin?” Aliuliza kama Mtu ambaye alikuwa amechanganikiwa
“Ndiyo! Hadhi yako ndani ya moyo wangu ni kubwa sana hustahili kuishi hapa, tafuta nyumba eneo lililotulia nitalipia kila kitu na kununua vitu vipya” Nilisema, mara moja Mosses alinivaa na kuanza kunipiga mabusu ambayo yaliamsha hisia zangu, nilijikuta nikiwa na hamu ya kufanya Mapenzi na Mosses, daktari alisema sipaswi kufanya hivyo hadi miezi sita itakapoisha lakini nilijikuta nikifanya mapenzi na Mosses, baada ya kumaliza nilimshukuru Mosses kwa penzi tamu alilonipa.
“Usijali Jacklin nipo kwa ajili yako mara zote” alisema Mosses na kunifanya nitabasamu kwa uchovu, shughuli ilikuwa pevu na vile nimetoka kuumwa basi nilichoka sana nikalala palepale.
Osman alipofika ofisini alihitaji kuniona ila aliambiwa kuwa nimetoka, akiwa kama Bosi wangu alihitaji kujuwa niko wapi, alinipigia sana simu lakini haikupokelewa maana nilikuwa nimelala chakali, basi alipiga kwa Mama na kumuuliza kama nitakuwa nimeenda nyumbani, Mama alimwambia Osman kuwa sipo nyumbani.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TANO Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx
31 Comments
Huyu dada n jauuuuuuuuu
Uyu dada wawapi vp mbona siyo muelewa kweli mapenzi ni giza
Mbona fupiiii leo
Ila jackline ni kiazi sana😂😂
Dah bora uyu mdad angekufa2😢
MH!
Jacqueline hafai hata kwa kulumagia Dah!!😭😭😭😭😭
Ivi hii ndo maana ya “ the when a woman loves….”😰 namhurumia Osman
Maskini osmani daah!! Jacklin bora angekufa mwandishi naomba hii story isituboe
Siyo kuboa tuu inaweza kukuliza huko mbelee😃😃😃
Yani ishaanza kuboa ila sisi wanawake basi tu jacklin wewe mmh😅😅😅
MH!
Sjawahi Comment Ila WANAWAKE JAU 😒😒😒
Fear women..
kesho muendeleze jaman kali kinoma
kesho muendeleze jaman kali
Jau kubabeq
Adimn kuchoshana ww andik zeEND…..mosses anamzurum jack……akn bado Osman anamsamehe
Ahahahaha siyo kumdhulumu atakuja kumcheat uyo demu….. hii story naifananisha na tamthiliya moja inaitwa mfadhili yaani ni mule mule..badae kati ya osman ama uyo jack mmoja atakufa
Kumbe na ww umeona eh…huyu ni dania kabisa yan…
Jacklin, sio
Fwalaaa sanaa mpaka hasira zimenipandaa wanawake bhanaa afukuzwe hata kazi tuu ubwa huyu
Madem jau sana duuh
💔
Dah huyu dad ni zaidi ya shetan ani
Mwenye huruma hanaga bahati
EWAAAH!! DATS KAMA MLIFATILIA COMMENT ANGU YA SIKU ZA NYUMA…NILISEMA HAPO LAZIMA KUNA NAMNA ITAKUWA ANI UYO JACKLINE MPKA AJE KUFUNGUKA AKILI NI BAADAE SANA WAKATI MAMB YAMEHARIBIKA🥲🥲🥲 KAMA UNAE MOYO MDGO UTALIA 😄😄 ILA KI UHALISIA WATU NDO WALIVO JMNIII
Wakina moses mikono juuu…….yaaan zitoke tatu kwa siku
Sasa osmad anashida gani, anatongoza kwa kuhonga, binafsi sijaona kosa la jackline, kwani wameshakubaliana kuwa wapenzi?????
😄😄😅
figo ya kiume imeingiliwa au figo haina jinsia
Kama ni Mimi naenda kuchukua Figo yangu