Ilipoishia “Yaani Mama kisa tu ana hela basi umechanganikiwa kiasiΒ hicho, kweli umasikini mbaya sana Mama, ila usijali siku siyoΒ nyingi nitaanza kazi nitakufanyia kila kitu, sawa Mama?”Β
“Mmh! Sawa” Mama alisema kisha aliondoka zake ila aliniachaΒ na jambo la kufikiria ndani ya akili yangu, nilikumbukaΒ kitendo chake cha kuondoka pale wodini baada ya MossesΒ kuingia, ila ni yeye ndiye aliyempigia simu Mosses baada yaΒ kuchukua namba kwenye simu yangu.Β Endelea
SEHEMU YA TATU
Sikutaka sana kuanza kufikiria hilo jambo, niliona ni boraΒ niwasiliane na Mosses maana baada ya kuachana naye kuleΒ Hospitali sikuongea naye kabisa, simu ya Mosses ilikuwaΒ imezimwa, ilinipa maumivu makali sana ndani ya moyo wangu,Β nilijigeuza geuza kisha Usingizi ulinichukua.Β
Kulipopambazuka nilianza kuhisi hali ya tofauti, mwiliΒ ulianza kuchoka hadi nilijishangaa, Mama aliendeleaΒ kunihudumia huku akiendelea kutafuta uwezekano wa kupataΒ Figo, alienda kwa daktari ambaye aliunganishwa na Osman,Β upatikanaji wa Figo ulikuwa mgumu sana huku hali yanguΒ ikizidi kudhohofu, nilikuwa napewa dawa tu nimeze, maumivuΒ niliyokuwa nikiyasikia kwenye tumbo langu yalikuwa makaliΒ sana nilitamani hata kufa kabisa, kwa siku zote hizoΒ sikumuona wala kumpata Mosses kwenye simu, ilizidi kunifanyaΒ niwe mgonjwa zaidi.Β
“Mama Mosses hapatikani leo siku ya kumi na mbili”Β Nilimueleza MamaΒ
“Usijali pengine amepatwa na tatizo kama hapa anapajuwa basiΒ atakuja siku moja” Alisema Mama, angalau alinipa moyo naΒ tumaini, lakini nilimuuliza
“Haya maumivu makali yanatokana na nini Mama? Mwili wanguΒ hauna nguvu kabisa nazidi kudhohofu” Nilipomuuliza nilionaΒ macho ya Mama yaliyojaa maumivu, alitamani kulia lakiniΒ hakusema shida iliyokuwa ikinisumbuaΒ
“Utapona Mwanangu! Mungu ni mwingi wa huruma, atakujalia afyaΒ njema Binti yangu” Alisema Mama kisha alininywesha ujiΒ
“Hivi umewasiliana na Osman Mama?” Nilimuuliza MamaΒ
“Ndiyo usiwe na wasiwasi ukipona tu utaanza kazi, pumzika kwaΒ sasa” Mama alikuwa ameshamaliza kuninywesha uji, alinifuta naΒ kuondoka zake, alipofika chumbani kwake alilia sana sababuΒ tumaini la Mimi kupona lilikuwa hafifu sana, siku zilisogea.Β
Mama pamoja na daktari walijitahidi kutafuta Mtu wa kunitoleaΒ Figo, walitangaza dau kubwa kadili siku zilivyokuwa zikiendaΒ ila waliojitokeza walikuwa ni Watu wenye Afya zisizoridhisha,Β figo zao pia zilionekana kuwa na Hitilafu, hazikufaa.Β Ilipofika siku ya 20 nilipekwa Hospitalini nikiwa katika haliΒ mbaya sana, nilikuwa sijitambui kabisa. Mama yangu alikuwaΒ Mtu wa kulia kila wakati, pesa ilipatikana kwa ajili ya FigoΒ lakini mtoaji wa figo hakupatikana, daktari alimwambia MamaΒ
“Hakuna namna tunaweza kufanya, nahisi kukata tamaa MamaΒ Jacklin” Alisema Daktari wakiwa ofisini kwa Daktari huyoΒ aliyeitwa Dokta SimonΒ
“Unaposema hivyo daktari unanipa wakati mgumu wa kuangaliaΒ mbele, sitaki kuamini kama siku za kuishi za Jacklin zimefikaΒ mwisho, Huyu ndiye Binti yangu wa pekee, sisi ni masikiniΒ sana, basi toa figo yangu kwa ajili ya Binti yangu” AlisemaΒ Mama, ilifika wakati ambao Mama alishindwa kuhimili maumivuΒ aliyokuwa akiyasikia katika kifua chakeΒ
“Mama Jacklin, umri wako na hilo jambo haviwezi kwendaΒ sambamba. Najuwa tumaini ni dogo sana katika jambo hili,Β lakini…”Β
“Dokta, kama kufa Mimi kutamsaidia Binti yangu hilo siyoΒ tatizo, hajawahi kuishi Maisha ya furaha katika Maisha yake,Β ndiyo kwanza alikuwa amepata kazi….leo afe aaaah hapana”Β Alisema Mama akiwa analia, alionesha uchungu wake kwanguΒ
“Sawa Mama! Ngoja tuiangalie kama itafaa” Alisema DoktaΒ Simon, kisha waliongozana hadi chumba cha Uchunguzi. MamaΒ alitakiwa kufanyiwa uchunguzi wa figo yake ili niwekewe MimiΒ nipate kunusuru Maisha yangu ambayo yalikuwa hatua za mwishoΒ sana.
Huu ndiyo upendo ambao Mama huwa nao kwa Mtoto wake,Β watakukimbia wote katika Maisha lakini Mama yako atasimamaΒ kwa ajili yako kila siku za Maisha yako, Mama alianzaΒ kufanyiwa uchunguzi. Bahati mbaya figo ya Mama ilikuwa naΒ Mawe hivyo isingeliweza kunifaa, Mama alilia sanaΒ
“Dokta weka hiyo hiyo ili Jacklin aamke, tumaini langu niΒ yeye pekee” Mama alilia hadi Dokta Simon alidondosha ChoziΒ lakeΒ
“Mama usilie, tuna siku 10 zilizobakia, Mungu atafanya wepesiΒ wa hili jambo, kwasasa Jacklin anahitaji Maombi” AlisemaΒ Dokta Simon, Mama alifikiria afanye nini, alichukua namba yaΒ Mosses kisha aliipiga akiwa HospitaliniΒ
Bahati nzuri siku hiyo simu ya Mosses iliita aliipokea, MamaΒ alimueleza Mosses hali ya afya yangu kwa wakati huo, MossesΒ alimwambia Mama kuwa alipata tatizo ndiyo maana alishindwaΒ kuja akaahdi kuwa atakuja Hospitalini. Kweli, Mchana MossesΒ alifika Hospitalini, aliishuhudia hali ya Afya yangu ambayoΒ alisimuliwa kama hadithi za Amza Stories, alikubali kuwa MimiΒ nilikuwa mgonjwa sana kwa jinsi nilivyodhohofu, pumua yanguΒ ilikuwa ya shida mnoΒ
“Hali ndiyo hiyo, leo siku ya tatu haongei wala hafumbuiΒ Macho. Kama unampenda Jacklin jitolee Mosses Mungu atakulipaΒ kwa wema wako” Mama alisema, walikuwa wodini wakiwa na yuleΒ Daktari SimonΒ
“Mama Mimi nitajitoa kwenye nini tena ikiwa mmetangaza dauΒ kubwa na bado figo haijapatikana, tumuombee Jacklin pengineΒ Mungu atampa nafuu” Alisema MossesΒ
“Kuomba tunaomba lakini hatuwezi kukaa kimya bila kufanyaΒ jitihada zozote Baba, mimi leo siku ya tatu sijala chochote,Β nione sina raha kwasababu ya Jacklin” Alisema Mama hukuΒ akibubujika Mchozi, Dokta Simon aliingilia kati akamwambiaΒ MossesΒ
“Ndugu najuwa inaweza kuwa ngumu kwako lakini kama huyu MtuΒ ana umuhimu kwako jitolee figo moja kwa ajili ya kumuamsha”Β Alisema Dokta, Mosses alishtuka akaulizaΒ
“Nitoe nini?”Β
“Figo kwa ajili ya Mpenzi wako” Alijibu Dokta Simon huku MamaΒ akiwa analia pembeni,
“Nitoe figo? Hiyo ni hatari sana Dokta nitafanya vyote lakiniΒ siyo kutoa figo yangu, ingekuwa wote wanaopendana wanatoleanaΒ viungo basi hii Dunia ingejaa walemavu kila kona” AlisemaΒ Mosses, Maneno yake yalimchukiza sana Mama alinyanyuka naΒ kumpiga kofi MossesΒ
“Mama hupaswi kufanya hivyo hapa ni Hospitalini istoshe niΒ wodini ambako panahitaji utulivu sana” Alisema Dokta SimonΒ
“Dokta huyu ni mshenzi anawezaje kusema maneno ya kikatiliΒ namna hiyo hakuona neno lingine la kusema? Huyu si ndiyeΒ ambaye alikuwa akikupa furaha, leo amelala hujali tena siΒ ndiyo?” Alihoji Mama huku akiwa anahema juu juuΒ
“Unathubutu vipi kunipiga Mimi? Unanijuwa Mimi? Kama MaishaΒ yake ni muhimu kwangu basi hata kwako ni Muhimu kwanini weweΒ usitoe hiyo figo? Siwezi kutoa kiungo kisa Mapenzi tena kwaΒ kiumbe anayeitwa Mwanamke, Jacklin akipona Mimi nipo akifaΒ Maisha yataendelea” Alisema Mosses kisha aliondoka Wodini,Β Mama alilia sana, kauli ya Mosses ilizidi kumfanya akateΒ tamaa, Dokta Simon alimwambia MamaΒ
“Siku bado zipo tuzidi kufanya jitihada na Maombi” AlisemaΒ kisha aliondoka zake, Mama aliendelea kulia kwa kukata tamaaΒ alinisogelea akasemaΒ
“Jacklin nimekuzaa kwa shida sana, nimekulea kwa tabu mno,Β leo nakupoteza Mama kwa shida sana, Nisamehe Mama yakoΒ nimefanya jitihada zote lakini nimeshindwa Mimi sababu hataΒ Mungu hayupo upande wangu tena” Maneno ya Mama niliyasikia,Β Chozi lilinivuja, sikuwa na nguvu ya kufanya chochote kileΒ
β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’Β
Ndani ya Dubai, Kilichompeleka Osman Dubai kilikuwa niΒ kumtafuta Zahra, achana na kiasi kikubwa cha pesa ambachoΒ Mwanamke huyo aliondoka nacho na kwenda huko kuishi naΒ Mwanaume mwingine, Osman alikuwa akimpenda sana MwanamkeΒ huyo, jitihada za kumpata Zahra ziligonga mwamba. AlirudiΒ Nchini, aliitafuta Familia ya Zahra lakini wazazi wa ZahraΒ walionekana kufurahia ambacho Bitni yao alikifianya.Β
Hawakuwa na huruma, Osman alijitoa sana kuhakikisha Maisha yaΒ Wazazi wa Zahra yanakuwa bora, aliwajengea jumba la kifahari,Β aliwanunulia magari ya kutembelea, alibadilisha Maisha yaoΒ kwa kiasi kikubwa sana, Osman aliondoka na kwenda kwenyeΒ gari, alikumbuka jinsi ambavyo aliishi kwa furaha na amani naΒ Zahra, alilia sana, Maumivu yalijaa ndani ya kifua chakeΒ alipoikumbuka meseji ya mwisho ambayo Zahra aliituma, mesejiΒ hiyo ilisema
“Osman! Najua ujumbe wangu utakupa maumivu makali sana lakiniΒ inabidi uupokee sababu ndiyo maamuzi yangu, asante kwaΒ kubadilisha Maisha ya Wazazi wangu kwa kiasi kikubwa lakiniΒ hukuwa chaguo la Moyo wangu japo ulinipenda sana, kwasasaΒ mimi nipo Dubai na Mwanaume ambaye ninampenda. UsiwazumbueΒ wazazi wangu wala usinitafute, pesa zote zilizo kwenyeΒ akaunti yako ya Benki nimezichukua, unaweza kujiona MjingaΒ lakini hiyo ndiyo nguvu ya Mapenzi ambayo ninayo, nilikufanyaΒ ukawa dhahifu kwangu! Nakutakia Maisha Mema, ni Mimi Zahra”Β
Ulikuwa ndiyo ujumbe wa Zahra baada ya hapo simu yakeΒ haikupatikana tena,, alipoupata ujunbe huo Osman alipotezaΒ fahamu akaenda kuzinduka kwenye Hospitali ya Dokta Simon,Β aliishi Maisha yaliyojaa maumivu na aliapa kuwa hatokujaΒ kupenda tena.Β
Basi, alifuta chozi akiwa ndani ya gari yake ya kifahari,Β alipotoka kwa Wazazi wa Zahra alikuja moja kwa mojaΒ Hospitalini maana aliwasiliana na Mama na akaambiwa kuwa haliΒ yangu siyo nzuri na haina tumaini.Β
Alimkuta Mama akiwa analia nje, Osman alimuuliza Mama “Hali yake kwasasa ipoje Mama?” Alimuuliza baada ya salamΒ
“Kama nilivyokueleza Baba, hali ya Jacklin ni mbaya sana,Β ninahofu juu ya uhai wake” Alisema Mama akiwa anaendeleaΒ kumwaga choziΒ
“Pole Mama, wakati mwingine Dunia inakuwa katili sana, naombaΒ nikamuone” Alisema Osman, walirudi wodini, Osman aliponionaΒ hakuamini kama ni Mimi ndiye niliyemchachafya siku kadhaaΒ zilizopita, nilikuwa nimekonda sana, nilikuwa nikipumua kwaΒ shida sana, alidondosha chozi akamuuliza MamaΒ
“Upatikanaji wa figo?” Mama alitikisa kichwa kuashiria kuwaΒ hakukuwa na uwezekano wa kupatikana figo kabisa japoΒ zilisalia siku 10Β
“Nitarudi Mama” Osman alitoka haraka akaelekea ofisini kwaΒ Dokta Simon.Β
“Bilonea Kijana karibu sana” Alisema Dokta Simon sababuΒ alikuwa akimfahamu sana Kwa ukaribu OsmanΒ
“Dokta Simon, Mama Jacklin amesema uwezekano wa kupatikanaΒ Figo ni mdogo sana, nataka kusikia kutoka kwako!”Β
“Huo ndiyo ukweli Osman, kilichobakia ni kudra za MwenyeziΒ Mungu pekee, tumepima Watu wengi lakini hakuna hata mmojaΒ mwenye figo yenye afadhali alafu kibaya zaidi Mpenzi wa huyoΒ Jacklin amegoma kufanya hivyo” Alisema Dokta SimonΒ
“Nitatoa Figo yangu” Alisema Osman, kauli hii ilimshtua sanaΒ Dokta SimonΒ
“Unatoa figo yako? Umefikiria mara mbili Osman? Hii familiaΒ inakuhusu nini wewe ikiwa mpenzi wa Jacklin amekataa, ufanyeΒ hivyo wewe kama Nani? Umesahau kilichokutokea Osman?”Β Aliuliza Dokta SimonΒ
“Natoa kama Binadamu niliyeguswa na hili Dokta Simon, MaishaΒ ya yule Msichana ni tunu Kwa Mama yake, ni furaha kwenyeΒ macho ya Mama yake ambaye muda wote analia. Umewahi kufikiriaΒ jinsi Mama yule anavyokosa raha kwasbabu ya Binti yake?Β Unajuwa ni furaha kiasi gani ataisikia endapo Binti yakeΒ atasimama tena?” Aliuliza Osman kwa hisia kali sanaΒ
“Fikiria mara mbili sikushauri kufanya hivyo Osman, wewe niΒ Bilionea Mkubwa hupaswi kuishi Maisha yenye kasoro kiasiΒ hicho!”Β
“Mkamilifu ni Mungu pekee, nitatoa Figo yangu kuokoa MaishaΒ yake” Alisema Osman kisha aliondoka akarudi Wodini, DoktaΒ Simon hakukubaliana na uamuzi wa Osman alinyanyua simu naΒ kuwapigia Wazazi wa Osman, aliwapata taarifa hiyo ambayoΒ iliwakasirisha sana Wazazi wa OsmanΒ
Basi, Osman aliporudi alimwambia Mama kuwa nitapona na kuanzaΒ kazi mara moja, japo Mama alikuwa katika hali ya huzuni sanaΒ ila maneno ya Osman yalimjaza tumaini.Β
Alipotoka Hospitalini Osman alikuwa mwenye mawazo na maumivuΒ makali sana, alipigiwa simu na Wazazi wake na kumtaka aachaneΒ na mpango wa kutaka kutoa figo kwani haitokuwa na faidaΒ yoyote kwake, Wazazi wa Osman waliamini kuwa Osman alikuwaΒ akitaka kutoa figo kwa ajili ya Mapenzi, walinuonya sana kwaΒ kile kilichomtokea kwa Zahra ila Osman aliwaambia Wazazi wakeΒ kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Mimi bali ni ubinadamu tuΒ wa kutaka kuhakikisha afya yangu inaimarika.Β
Osman aliwasiliana na Hospitali nyingine ambayo ingefanyaΒ operesheni ya kupandikiza figo kwenye mwili wangu, kutokanaΒ na utajiri alionao aliweza kupata Hospitali Nchini India,Β tulisafiri kwenda huko. Osman alishauriwa na kuambiwa kilaΒ kitu kiafya kuhusu uamuzi wake.Β
Nini Kitaendelea? Osman atatoa FIGO? Usikose Sehemu Ya NNE Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ
14 Comments
Duuuh Osman ni mwanaume wa maanaπ
Ila sas ili ujue binadamu jauπππ au ngoja …. nisiharibu uhondo siku ikifikia ntakwambiaa…hii tamthiliya inaweza kuliza watu huko mbele π₯²π₯²π₯² me siyo mtabiri akin
π mule mule baba admin…..hujai kosea
Sas huyu binti akitaka kutukera apone af arud kumpenda mosses tena wakat osman katoa figo hapπ
Wanaume kama osman tumebaki wachache sanaa
Calvin kabisa ππππ
Huyu dada nna was was akipona …atanboaaaa
Niko njia Panda naomba mosses
Afutwe uhusikaπ£
Huu uzi sio poa hatariii kama ungekuwa unaachia mbili mbili vile daah hatariiπ₯π₯
Yani wanawake sisi Sijui kama atakumbuka wema Na fadhila
π
Mmmh tusubili namba 04 π€π€
NAUZA FIGO +255788414957
!!!!!!!! Kuna mtu ata π
ππ