Ilipoishia “Jacklin Mwanangu sijapata pesa kama unaweza kusubiria hadiΒ jioni sawa” Alisema MamaΒ
“Usijali Mama nitarudi tu” Nilisema, sikuwa na pesa ya nauliΒ ya kurudia nyumbani alafu mvua ilikuwa ikinyesha sana,Β kulikuwa na hali ya radi pia, nilifikiria kama OsmanΒ angelinikuta pale nje ingeleta picha mbaya zaidi, nilifikiriaΒ pia ile pesa niliyompa kwa hasira, nilijilaumu sana kwaΒ kiburi changu. Basi niliingia kwenye mvua, nilivua viatuΒ vyangu. EndeleaΒ
Kumbe yule Mdada msaidizi wa Osman alikuwa akiniangalia tu,Β alienda kumwambia Osman, nilitembea kwenye mvua nikiwaΒ natetemeka, kufika nyumbani kwetu kwa mguu ni zaidi ya masaaΒ matatu. Kwa jinsi mvua ilivyokuwa ikinyesha ilionesha waziΒ kuwa isingelinyamaza kwa muda huo, basi niliendelea kutembea.Β Osman alipopata taarifa kuwa natembea kwenye Mvua aliachaΒ kazi zake, alichukua Mwamvuli akaingia kwenye gari yakeΒ akaanza kunifukuziaΒ
Ilifika mahali baridi lilinizidia, nilitembea kwa maumivuΒ makali huku nikimfikiria sana Mosses, kwanini hakunitumiaΒ hiyo pesa? Kwanini alikuwa hapokei simu zangu, nilijikutaΒ nikilia njiani sababu moyo wangu nilimpa Mosses, niliulaumuΒ Β umasikini ambao Baba yangu alituachia, nilimlaumu MunguΒ kwanini alimchukua Baba wakati akiwa masikini?
Mara nilisikia Honi ya gari, niliipisha ipite lakiniΒ haikufanya hivyo, alikuwa ni Osman. Nilipogundua ni yeyeΒ niliondoa mikono yangu kifuani, nilitabasamu ili asione kamaΒ kutembea kwenye mvua kumetokana na kutokuwa na hela bali niΒ mazoezi tuu. Alishusha kioo akaniambiaΒ
“Ingia kwenye gari nikusogeze Jacklin” Alisema kwa busara naΒ hekima ya hali ya juu sana, pesa alizonazo Osman hakustahiliΒ kuninyenyekea namna ileΒ
“Hapana nafurahia maajabu ya Mungu” Nilisema huku nikiwaΒ napiga hatua huku Osman akiendesha taratibu.Β
“Hapana mvua ni kubwa sana Jacklin, twende nikupeleke kwenu”Β Alisema tena OsmanΒ
“Usijali Osman, nitachukua Tax mbele, nafurahia mvua kwanza”Β Nilisema nikiwa nimeshikilia viatu vyangu mkononi, Basi OsmanΒ alifunga kioo ili aondoke zake, kiukweli hali yangu haikuwaΒ nzuri, lile baridi lilinitesa sana, njaa ilikuwa ikinikwanguaΒ vibaya mno, nilijikuta nikianguka kwenye mvua.Β
β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’Β
Nilipokuja kurudisha fahamu zangu nilijikuta nikiwaΒ Hospitali, Osman alikuwa amekaa kitandani, Mama yangu alikuwaΒ pembeni yanguΒ
“Mama!” Nilimuita MamaΒ
“Jacklin Mwanangu, nesi Mwanangu ameamka” Alisema Mama,Β alinifanya nitabasamu sana, Upendo wa Mama ulikuwa Mkuu sanaΒ kwangu, niligeuza macho na kumtazama OsmanΒ
“Asante sana Osman” Nilisema nikiwa natabasamu japoΒ nilipoteza fahamu ila nilijuwa tu aliyenisaidia alikuwa niΒ Osman, kabla hajanijibu Chochote nesi alikuja kwa ajili yaΒ kuangalia hali yangu, Osman alimwambia MamaΒ
“Naomba tuongee kidogo Mama” Basi Mama na Osman walitoka hukuΒ Daktari akiwa ananiangalia kwa makini na kiniuliza baadhi yaΒ Maswali ili kujuwa nilikuwa najisikiaje.Β
Osman alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo, alimuulizaΒ MamaΒ
“Huyu ni Binti yako wa kumzaa?” Mama alitabasamu kishaΒ alimjibu Osman
“Ndiyo, ndiye Mtoto pekee ninayemtegemea, nakushukuru sanaΒ Baba japo sijakufahamu maana umenipigia tu simu na kunielezaΒ kuhusu hali ya Binti yangu, kwa jinsi nilivyokuwaΒ nimechanganikiwa wala sikuwa na muda wa kukuuliza” AlisemaΒ MamaΒ
“Naitwa Osman, Mimi ndiye mmiliki wa kampuni ambayo BintiΒ yako alikuja kuomba kazi” Alijitambulisha Osman kwa MamaΒ yanguΒ
“Ooh! Asante sana Baba” Alisema MamaΒ
“Sasa Mama! Pamoja kwamba hali ya Binti yako unaiyona ipoΒ sawa lakini kuna tatizo kubwa sana katika mwili wake,Β inaoneka figo zake zote mbili hazifanyi kazi ipasavyo,Β inatakiwa kubadilishwa, kama zitapatikana mbili au moja iliyoΒ imara sana” Alisema Osman, Mama alishindwa hata kusimamaΒ aliomba akae kwanza, akiwa kama Mama alichanganikiwa sanaΒ kusikia nina tatizo la figo zanguΒ
“Unasemaje?” Aliuliza Mama akiwa anakaribia kuanza kuliaΒ
“Ndiyo maana Mama nimekuita hapa iliniweze kuzungumza na weweΒ kuhusu hali ya Jacklin, ana siku 30 za kufanyiwa matibabu”Β alisema OsmanΒ
“Sasa mimi na umasikini huu nitaweza vipi Baba yangu? MunguΒ kwanini ananipa mtihani mzito kiasi hiki niimemkosea niniΒ Mimi?” Alisema Mama akiwa analia, Osman aliketi na kumwambiaΒ MamaΒ
“Mimi nina safari ya kwenda Dubai kesho, gharama zoteΒ nitazifanya. Mnapaswa kutafuta Mtu wa kumtolea figo Jacklin”Β Alisema Osman, angalau Mama alifuta mchozi wakeΒ
“Nitakuunganisha na daktari Bingwa wa hii Hospitali,Β mtasaidiana itakapopatikana hata moja imsaidie Binti yako”Β Alisema Osman, Mama alimtazama Osman akamwambiaΒ
“Wewe ni Binadamu mwenye moyo wa peke yako Mwanangu, MunguΒ azidi kukubariki kwenye kila hatua” Alisema MamaΒ
“Ila Mama naomba hili liwe siri yako, Jacklin hapaswi kujuwaΒ kama ana tatizo la figo sababu akijuwa inaweza leta shidaΒ zaidi” Alisema Osman, walipomaliza kuzungunza walirudiΒ wodini, walinikuta nikiwa ninafakamia vyakula maana njaaΒ niliyokuwa nikiisikia haikuwa ya kawaida, sura zaoΒ hazikuonesha dalili ya tatizo lolote lileΒ
“Jacklin!” Aliniita Mama kisha aliketi kitandani
“Kama kuna Binadamu ana roho nzuri katika hii Dunia basi huyuΒ Kijana ni namba moja, namshukuru kwa kuokoa Maisha yako”Β Alisema Mama kisha alitabasamu, kumbe Osman alikuwaΒ amewasiliana na Mosses na kumwambia kuwa nilikuwa nina umwaΒ sababu namba ya Mosses nilisave kama Mume wangu, alikuja mudaΒ huo, alinikumbatia na kunipiga busu mbele ya Mama na Osman,Β Mama alishangaa sana sabahu alikuwa hamfahamu MossesΒ
“Mama!! Huyu anaitwa Mosses, ni..ni…ni” nilishindwaΒ kumtambulisha Mosses mbele ya Mama na Osman, Basi muda huoΒ huo Osman aliaga na kuondoka zakeΒ
“Mama huyu ni Mchumba wangu anaitwa Mosses…..Mosses huyu niΒ Mama yangu” Nilijitahidi hadi kumtambulisha Mosses kwa MamaΒ yangu, japo niliona Mama hakufurahia ila alijikaza tuΒ
“Oooh!! Sawa, basi mpate muda wa kuongea Mimi naenda kwaΒ daktari” Alisema Mama, kumbe alikuwa anataka kumuwahi OsmanΒ nje, kweli alimkimbilia Osman kabla hata hajapanda kwenyeΒ gari akamuita, alipomfikia alimwambia OsmanΒ
“Baba upo sawa?” Aliuliza MamaΒ
“Ndiyo Mama nipo sawa, naenda kuendelea na kazi” AlisemaΒ Osman, ila Mama alihisi kuna jambo lipo ndani ya Osman kwaΒ jinsi alivyoaga pale wodini.Β
“Nakuomba Mwanamgu, msaidie Jacklin apone na Mungu atakulipaΒ zaidi” Alisema Mama, Osman alimsogelea Mama akamwambiaΒ
“Ni jukumu nililokuahidi Mama, Mwanao atarudi kuwa sawa tuΒ wala usijali, hii hapa ni kadi yangu ya Biashara” alimpatiaΒ Mama kadi yenye mawasiliano yake, Osman aliingia kwenye gariΒ yake na kuondoka.Β
Mosses alikuwa ndiyo Mwanaume niliyempenda sana katika MaishaΒ yangu, ndiye aliyenitoa usichana wangu, nilimuulizaΒ
“Kwanini ulikuwa haupokei simu yangu?”Β
“Samahani Mke wangu, unajuwa muda ule nilipatwa na dharuraΒ nikaenda kumuona Mdogo wangu alikuwa ana tatizo” AlisemaΒ MossesΒ
“Ooh pole sana, anaendeleaje”Β
“Yupo sawa, hivi huyu jamaa aliyekuwa amekaa hapa ni nani?Β Mbona baada ya kukupiga busu aliaga?” Aliuliza Mosses
“Mmmh! Jamani Mosses, ni rafiki tu, ndiye aliyenisaidia”Β nilimjibu Mosses, kitu kilichokuwa kikinivutia zaidi kwaΒ Mosses ni wivu wake kwangu, yaani nisisimame na Mwanaume auΒ kuongea nayeΒ
“Anhaa! Sasa sitaki hayo mazoea na huyo jamaa sawa?” AlisemaΒ
“Mmmh! Sawa” Nilimjibu, Mama aliporudi alitukuta tukiwaΒ tumemaliza mazungumzo, basi alimuita Mosses pembeni naΒ kumueleza kilichokuwa kikinisibu sababu alikuwa Mtu wangu waΒ karibu sana.Β
Mosses alipoambiwa hivi kuwa nina tatizo la Figo alimuulizaΒ MamaΒ
“Mama unajuwa matibabu ya Figo yana gharama kubwa sana naΒ kama hivyo umesema yanahitajika ndani ya siku 30 tu,Β itakuwaje?Β
“Sasa unafikiria nitafanya nini Kijana? Japo yupoΒ aliyejitokeza kugharamia matibabu ila hatuwezi kumuachia yeyeΒ kila kitu ndiyo maana nimekueleza na wewe ili nione kwaΒ upande wako utajitoa vipi maana Jacklin ni wako wewe” MamaΒ alisema, maneno ya Mama yalijaa uchunguzi sanaΒ
“Mama naomba siku moja ya kutafakari kisha nitakupa mrejeshoΒ wa nini ambacho mimi nitafanya, ila nakuahidi kuwa tupoΒ pamoja” Alisema Mosses, basi siku hiyo niliruhusiwa kurudiΒ nyumbani ila nilikuwa nahisi maumivu kiasi fulani kwenyeΒ mbavu zangu, jinsi Mama alivyokuwa akinifanyia kila kituΒ ilinitia shaka sana nilimwambiaΒ
“Mama Mimi nipo sawa huna haja ya kunifanyia kila kitu” “Nafanya sababu nakupenda Jacklin” alisema MamaΒ
“Najuwa kuwa unanipenda lakini nilianguka sababu ya baridi tuΒ Mama hakuna kingine, nipo sawa” Mama hakusema chochote kileΒ kuhusu tatizo nililokuwa nalo la figo, siku iliyofuata OsmanΒ alienda Dubai kama alivyomwambia Mama.Β
Usiku wa siku hiyo, kilikuwa kipindi cha mvua hivyo kulikuwaΒ na baridi sana, Mama alikuja na kuniambia kuwa Osman alikuwaΒ ameshaondoka, ilinishangaza sana namna ambavyo Osman na MamaΒ awalikuwa karibu kiasi hicho hadi kuanza kujuwa kuhusu safariΒ Β
za Osman, nilicheka kwanzaΒ
“Mmh! Mama nawe, yote hayo umeyajuaje? “
“Si kaniambia mwenyewe jana kule Hospitali, alafu JacklinΒ ngoja nikuulize swali, unamuonaje Osman?”Β
“Mh! Mama hebu liweke vizuri hilo Swali, namuonaje kivipiΒ tena?”Β
“Hujausoma Moyo wake? Hujahisi kitu ndani ya moyo wa yuleΒ Kijana?”Β
“Sasa Mama naanzaje kuusoma moyo wa Mtu ambaye sina ukaribuΒ naye? Alafu hata kama akiwa na kitu moyoni mwake mimi tayariΒ nina Mtu wangu..”Β
“Sijamaanisha eti uwe naye hapana ila nimekuuliza tuuΒ Jacklin, anaonekana ana upendo sana yule Kijana” MamaΒ aliendelea kusema mafumbo ila niliijuwa nia yakeΒ
“Yaani Mama kisa tu ana hela basi umechanganikiwa kiasiΒ hicho, kweli umasikini mbaya sana Mama, ila usijali siku siyoΒ nyingi nitaanza kazi nitakufanyia kila kitu, sawa Mama?”Β
“Mmh! Sawa” Mama alisema kisha aliondoka zake ila aliniachaΒ na jambo la kufikiria ndani ya akili yangu, nilikumbukaΒ kitendo chake cha kuondoka pale wodini baada ya MossesΒ kuingia, ila ni yeye ndiye aliyempigia simu Mosses baada yaΒ kuchukua namba kwenye simu yangu.Β Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Tatu Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ
15 Comments
Dooohhh π₯΄huyu moses apotelee mbali bhn abaki Osmanπ
πππkivumbi
Hii inanikumbusha kuna tamthiliya moja ya mfadhili …kiswahil Advance level
Mm limoses nshaanza kuliona n jau …awe n Osman tu
Lus unapenda ela wewπ
sidhani kama moses atapatikana tena kwenye simu
Huyo Moses ayeyukiee juani
Ef 5 tu alizima itakuwa kuchangia Figoπ π π π
Dada wa wap uyu mbona achangamkii fursa
Aah uhondo huu natamani usiishe hongera Kwa kaz mzuri π
Ongeza kidogo urefu wa liwaya mtunzi tunaenjoy sana.. ππΏ
I SEE MFADHILI ON ONE AND TWOππ
Mwandishi ungekuwa mcheza mpr.. bc tungekuita pele..
https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J
Osman anaenda kuchukuwa mzigo kupitia ushawishi wa mama