Ilipoishia “Sikujuwa hata mtandio wangu niliudondoshea wapi, nilikuwa kama Chizi maana wakati nalia nilitimua sana nywele zangu. Nilikaa hapo kama Bubu, niliwaza sana hadi kichwa kiliacha kufikiria tena, Sikujuwa niende wapi maana Sikuwa na namba ya Mtu yeyote yule Kichwani, sikuwa na kumbukumbu ilipo Ile kumbi ya Sterehe maana nilienda mara moja tu, kingine sikuwa na kumbukumbu pale nilipokuwa naishi na Shonaa palikuwa panaitwaje maana napo nilikaa kwa siku mbili tu, nilikuwa Mgeni Dar, Nilimkumbuka sana Shonaa hadi Chozi likawa linanidondoka tu. Endelea
SEHEMU YA TANO
Laiti kama Shonaa angekuwepo asingeruhusu napata tabu, nilijilaumu hata kwanini nilishuka kwenda kujisaidia, Maisha yangu yaliingia kwenye Dunia nyingine ngumu zaidi tofauti na Mwanzo, niliivua ile Rozali kisha niliitupa kwenye mtaro mdogo ulio mbele yangu, niliona Mungu amenisahau katika Hesabu zake au alikuwa akinifanyia makusudi
“Sasa kwanini ulimchukua Mama yangu, hukujuwa kama nitateseka? Kama Mungu una nguvu nitoe hapa nipae hadi Tabora” Nilisema maneno ambayo hata Kichaa hawezi kuyafikiria, niligumia kwa nguvu sana hadi Watu walio karibu walisimama kuniangalia kwa muda kisha waliondoka zao.
Nilikaa pale kwa zaidi ya Masaa matatu, baadaye alikuja Mwanaume mmoja alikaa kando yangu, alikuwa bize na simu yake hata hakunisalimia. Nilipata akili ya kumsalimia
“Mambo Kaka?” Nilisalimia nikiwa namtazama
“Powa” Alijibu bila hata kunitazama Usoni, niliona potelea mbali nimuombe msaada tu hata kama anaonekana ana dharau
“Naitwa Jojo, Kaka yangu naomba msaada nilikuwa nasafiri naenda Tabora bahati mbaya nimeachwa na gari, sina ndugu hapa Mjini wala sijui leo nitakula nini na nitalala wapi” Niliposema hivi alinitazama, nililiona jicho lake la kunichunguza
“Una shida kweli wewe?” Aliniuliza kwa sauti kavu sana, mkononi alikuwa na tatuu, alikuwa na kifua cha kujaza alafu alikuwa mweusi hivi, nilimjibu
“Ndio”
“Subiri kuna mzigo napokea” Alisema yule Mkaka, niliona kama ngekewa vile maana nilishakata tamaa kabisa, kusikia Mtu atanisaidia ilikuwa faraja kubwa kwangu. Ilituchukua nusu saa tukiwa kimya huku yeye akiendelea kuchezea simu yake.
Alikuja Mwanaume mwingine aliyefanana na yeye, alimpatia Boksi hivi dogo kisha aliondoka jamaa yule alafu yule Mkaka akaniambia
“Twende” alisema kikauzu sana, unafikiria nilitilia shaka msaada wake? Wala sikuwa na mashaka hata kidogo, nilimfuata kwa nyuma. Kumbe alikuja na Pikipiki yake aliiacha nje, alinipa lile boksi dogo kisha aliniambia nipande kwa nyuma. Nilipanda kisha safari ya kuelekea nisipopajua ilianza, angalau chozi lilikuwa limekauka, niliona mwangaza mpya katika Maisha yangu.
Ilikuwa ni safari ndefu kutoka Ubungo, nilisoma vibao vya Njiani ili kujuwa tupo wapi, niliona tupo mwenge kisha baadaye niliona Mbezi Africana, hapo ndipo safari yetu ilipoishia kwenye nyumba moja hivi ambayo ilikuwa kimya sana. Aliniambia nimpe Boksi lake baada tu ya kushuka, kisha aliekelea kufungua geti, tuliingia humo. Ilionekana ni nyumba ambayo haikuwa na Mtu kabisa maana alifungua milango yote hadi tulipofika sebleni kisha alisema
“Karibu” Alisema alafu alijitupa kwenye kochi, akawa analifungua Boksi lile alilopewa na yule jamaa kule Ubungo.
Alitoa vitu kama Unga fulani hivi ila hata sikutaka sana kujiuliza maswali mengi, akaingia chumba kimoja alafu akatoka akiwa ameshikilia kisu, nilihofia sana maana nilikumbuka lile tukio la Kutaka kubakwa kule kwa Shonaa. Yule Mkaka alikuja karibu yangu akavuta kiti kisha akakaa mbele yangu, hofu ilianza kunijaa
“Umesema unaitwa Nani?” Aliniuliza
“Naitwa Jojo” nilijibu kwa woga sana
“Jojo…sasa Jojo, mimi najuwa kama wewe ni Askari na kwanini uko hapa, umetumwa kunipeleleza si ndiyo?” Aliniuliza yule Mkaka ambaye hata Jina lake sikulifahamu, stori ya Maisha yangu ilianza kunichanganya maana kila nilipoenda nilikutana na kikwazo kikubwa zaidi.
“”Mimi siyo Polisi Kaka yangu, Nahitaji msaada wa Mimi kurudi Tabora kama hauwezi kunisaidia basi niruhusu niondoke” Niliona ni bora hata kuondoka kuliko kuendelea kuwa pale
“Wengi waliotumwa kwangu walipotea kama ambavyo wewe unaenda kupotea,”.
“Unamaanisha nini?” Niliuliza kwa hofu kubwa sana, niliona sasa Maisha yangu yanaenda kufika kikomo
“Mimi ndiye Juma Baro, najua nini nafanya” alinivamia, nilijitahidi kupiga kelele kuomba msaada, alinikamata vizuri kisha aliniweka unga kwenye pua yangu, sikuchukua raundi, nilihisi mwili hauna nguvu kisha niliona giza zito, sikujuwa kilichoendelea.
Niliporudisha fahamu zangu nilijikuta kwenye chumba chenye giza, ghafla taa iliwashwa, Yule Mkaka aliyejitaja kuwa ni Juma Baro alisimama kando yangu. Nilikuwa nimechoka sana, nilikuwa nahema juu juu, alinimwagia maji ya Baridi, angalau alifanya mwili wangu uanze kuwa sawa.
“Kaka yangu naomba uniruhusu niomdoke Mimi siyo Polisi” Nilisema.
“Najuwa wewe siyo polisi, dakika chache nimelitambua hilo, lakini bahati mbaya ni kuwa umejuwa baadhi ya vitu na wapi yalipo makazi yangu, sitokuruhusu kwenda popote badala yake utaishi hapa” Alisema, nilishtuka nikamwambia
“Sijui chochote kuhusu wewe Kaka yangu, naomba tafadhali sana uniache niende nikatafute msaada sehemu nyingine, nakuomba Kaka yangu nipo chini ya Miguu yako” Nilisema, alikuwa amenifunga kamba mikononi na miguuni.
“Hutoweza kutoka hapa tena utaishi hapa kama Mke wangu” Alisema Juma Baro
“Tafadhali Sana Kaka yangu nakuomba usifanye hivyo, nina apa kwa Mungu wangu kuwa sijui chochote, ninachotaka ni kurudi Tabora tu”
“Mungu? Kumbe Mungu wako yupo? Yupo wapi sasa? Basi huyo Mungu amekusahau, angekuwa anakukumbuka angekutoa hapa kwenye hiki chumba” Alisema Juma Baro kisha aliondoka na kufunga mlango kwa nje, kamba zilikuwa zimeniumiza mno mikononi, kauli moja ya Juma Baro ilijirudia katika akili yangu kuwa “MUNGU AMENISAHAU” Ndiyo niliitafakari sana, niliona ina ukweli ndani yake sababu kama angekuwa ananikumbuka basi angenitoa kwenye matatizo na kuniweka salama, kwanini anazamisha Maisha yangu kila wakati.
Niliishi pale kwa Juma Baro kama Mfungwa ndani ya Chumba chenye giza, nilililaani Jiji la Dar-es-salaam, nilimlaani Msonjo kwa kunileta katika Jiji hili lenye kila aina ya ukatili. Alikuwa akija kuniletea chakula, alikuwa akija kwa siku mara mbili, sikujuwa ilikuwa ni siku gani, sikujuwa ulikuwa ni wakati gani, chumba hicho kilitengenezwa mfano wa chumba cha Kulala maabusu, hakikuwa na Choo, dirisha lake lilikuwa juu sana hata sikuweza kuangalia nje.
Nilikuwa najisaidia kwenye ndoo kisha anakuja kuchukua, anaenda kumwaga, sikujuwa nilikuwa kwenye ile nyumba ya mwanzo au alinipeleka kwenye nyumba nyingine, Basi niliishi Maisha hayo.
Usiku mmoja alikuja, alinifungua kamba mikononi kisha alinitoa humo akiwa amenifunga kitambaa usoni, alinipeleka kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kizuri sana, kilikuwa na kila kitu akaniambia
“Kuanzia leo utakuwa unaishi hapa”
“Kwanini unanifanyia hivi Kaka yangu, unajuwa ni kiasi gani nateseka Mimi?” Nilisema kwa maumivu makali sana ndani ya moyo wangu.
“Unayajua mateso wewe? Katika watu nimeishi nao vizuri wewe namba moja, unajuwa kwanini?” Aliniuliza akiwa amenisogelea, nilitikisa kichwa changu ishara kuwa sijui
“Kwasababu wewe ni Mzuri sana Jojo, ni hasara kubwa kuishi na wewe katika mateso makubwa ndiyo maana nimekuleta hapa” alisema, kusema ule ukweli woga uliniisha kabisa sababu sikuwa na uwezo wa kufanya chochote kile. Alianza kunishika shika kitu ambacho kilinifanya nichukie, nilimpiga kofi
“Ukiendelea kunishika nitakufanya kitu kibaya” Nilisema, Juma Baro alipandwa na hasira akanitandika kofi na Mimi kisha alinitupa kitandani, alitumia nguvu zote aliniondoa nguo zangu na kunibaka.
Ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuingiliwa na mwanaume, tena kwa kubakwa, nilipata uchungu na maumivu makali sana katika sehemu zangu za siri, roho iliniuma sana. Damu zilinitoka lakini hata hakujali aliondoka zake na kufunga mlango, katika mateso ambayo yaliniumiza moyo na akili yangu ni pamoja na kubakwa, nilijiona nimeondolewa thamani yangu, nilijiona nimepoteza kila kitu katika Maisha yangu
Nililia sana, mwili ulishika moto vibaya mno. Baadaye alikuja akanipa dawa za kutuliza maumivu kisha aliondoka zake
Hayo yalikuwa ndiyo Maisha yangu nyumbani kwa Juma Baro, niligeuzwa kuwa Mtumwa wake wa ngono, alinifanya apendavyo tena bila kujali kuwa nilikuwa ninaumia sana kuingiliwa bila ridhaa yangu. Nilipiga sana kelele lakini sikuuona msaada wowote ukija mle ndani, nilienda mwisho nilikata tamaa ya kutoka kabisa.
Niliishi hapo kwa miezi miwili nikiwa sijui siku wala muda, niliona jua likizama na kuchomoza. Madirisha yalikuwa yamewekwa nondo ngumu na kioo hivyo hata ningefanyaje nisingeliweza kufungua na kutoka, niliishia kufungua dirisha na kuangalia mwanga wa jua tuu.
Juma alipojisikia kufanya mapenzi alikuja na kunitumia vile apendavyo yeye hadi pale anapokuwa ameridhika ndiyo anaondoka, nilizoea maisha hayo hata nikawa silii hovyo tena sababu tumaini la kuondoka hapo halikuwepo kabisa, sikumtaja tena Mungu katika Maisha yangu sababu niliona hanisikii tena.
Kufanywa bila kinga kulisababisha nipate mimba, nilimueleza Juma Baro kuwa Mimi ni Mjamzito, alichukia sana akawa ananiambia kuwa nimefanya makusudi wakati anajuwa fika alikuwa akinifanya Bila kinga. Roho iliniuma sana akaniambia atanipa vidonge nitoe ujauzito, sikuwa na pingamizi istoshe sikupenda kuzaa na Mtu katili kama Juma Baro, Basi jioni aliniletea vidonge nikameza, cha ajabu mimba haikutoka kabisa wala sikuhisi maumivu yoyote yale wakati nilikuwa nikisikia kuwa Mtu anapotoa Mimba anapata maumivu ya Tumbo ila kwangu haikuwa hivyo kabisa, nilirudia kumeza kwa hasira yani sikutaka kuwa na kiumbe cha Juma Baro.
Asubuhi nilipoamka niliona damu kidogo sehemu nyeti ila ilitoka bila maumivu yoyote. Juma alipokuja aliniuliza
“Hivi umemeza vidonge wewe?” Aliniuliza kwa dharau sana kama vile mimi nilikuwa nataka kuzaa na yeye
“Ndiyo” nilimjibu kwa kifupi sana
“Yaani umeze vidonge na uwe sawa hivyo, unanitania si ndiyo?” Aliuliza Juma Baro, nilinyanyuka nikamsogelea bila woga
“Unafikiri nataka kuzaa na Mwanaume katili kama wewe? Ungejua jinsi ninavyo kuchukia hata usingenisemesha, natamani hii Mimba itoke kimiujiza” Nilisema kwa hasira mbele yake
“Ok! Ngoja” Alisema Juma kisha alisogea mezani akachukua vidonge kama vitano kisha akaniambia
“Meza hivi vidonge mbele yangu vinginevyo nitaitoa hiyo mimba kwa mikono yangu” Alisema kwa jazba, nilivichukua vidonge kwa hasira sana kisha nikachukua maji na kuvimeza vyote
“Ungejua natamani kufa kuliko kuendelea kuwa hapa, kama kuna sumu nipe ninywe nife, bora kufa kuliko kuishi maisha yaliyojaa mateso kama haya” Nilisema, Juma alinisogelea kisha akaniuliza
“Unataka kufa?”
“Ndiyo! Kama siyo kunifunga mikono na miguu ningekuwa nimeshaondoa Maisha yangu” Nilisema huku chozi likinimwagika
“Nakurahisishia kazi” Alisema Juma, aliacha mlango wazi kisha alitoka, niliketi kitandani, alirudi na Madawa ya kulevya
“Tumia haya, dakika chache utakuwa umefika kwa Mungu wako” Alinipatia kifuko kidogo sana kilichofungwa Unga huo, kiukweli nilisema tu yale maneno ila kufa sikufikiria kabisa niliamini ipo siku nitatoka pale, hivyo nilibakia nikiwa nimesimama tu na kumtazama Mwanaume huyo kwa jinsi alivyoamua kuwa katili wa Maisha yangu.
“Unasubiria nini?” Vuta huo Unga, natumaini nitakaporudi nitakuja kutoa maiti yako na kwenda kuitupa” Alisema Juma kisha aliondoka zake na kunifungia mlango.
Nilichoka sana nilijitupa kitandani, sikuwa na ujanja wala sikujua nafanya nini, nilisikia mlio wa gari yake kisha geti kufunguliwa akawa ameondoka zake, ilikuwa ni ngumu sana Mimi kujuwa nipo wapi sababu dirishani niliona ukuta mrefu, sikuona nje. Hata hivyo nilijiuliza kwa kelele nilizokuwa napiga kama nyumba ile ingekuwa kwenye makazi ya Watu basi wangenisikia na kunisaidia haraka sana.
Ilikuwa ni wakati wa jua kuwaka, baadaye lilizima na giza liliingia, mlio wa gari niliusikia kisha geti lilifunguliwa, baadaye mlango wa chumba nilichopo ulifunguliwa, alikuwa ni Juma Baro, aliponiona alinicheka, nilimtazama kwa hasira sana
“Nilijuwa utakuwa umeshakufa Jojo, nilijiandaa kukuchimbia kaburi hapahapa nyumbani kwangu nikuzike, inaelekea una damu kali sana hadi dawa hazikufanya kazi si ndiyo?” Aliuliza nikiwa nimejilaza tu nikiwa namtazama, aliuchukua ule unga wake kisha akaniambia
“Ngoja nikuoneshe kitu” Alinifuata akanifunga miguu na mikono yangu, yalikuwa ni maisha niliyoyazoea wala sikuwa mkorofi hadi alipomaliza, nikawa siwezi kufanya chochote. Alitoboa kifuko kisha akatoa unga kwa kutumia kidole chake
“Usihangaike sawa?” Alisema, sikujuwa alikuwa anataka kunifanyia nini, nilishtuka aliponikamata kichwa na kunipakaza ule unga eneo la pua, nilihisi maluwe luwe ambayo sikuwahi kuyahisi kabla, Niliona nyumba inageuka alafu mwili ukawa unawasha sana
“Unanifanyia nini Mshenzi wewe” Nilisema kwa sauti kavu iliyotoka kwa nguvu sana nikaambatanisha na kelele
“Shiii!” Alinitaka kunyamaza kisha aliniweka tena, basi nililegea mno nikajikuta napoteza uwezo wa kufikiria.
Alinifanyia huo mchezo kwa siku saba mfululizo hadi nilijiona mdhahifu sana, kisha aliniacha. Cha ajabu ambacho kilinishangaza nilijiona nakuwa na hamu ya kupakwa yale madawa, nilikuwa nahisi mwili una baridi mno, nikawa natetemeka mwili mzima na vipere vya msisimko vilikuwa vikinitoka, kwa mara ya kwanza nilipata maumivu makali ya tumbo kisha niliona mabonge ya Damu yakinitoka huku chini, nilijisafisha ila mwili haukuwa na nguvu hata kidogo, nilijuwa tu yale maumivvu yalitokana na mimba kuharibika.
Aliponiletea chakula nilimwambia Juma Baro kuwa mwili wangu ni dhahifu sana, alicheka tu kisha aliondoka zake, nahisi alikuwa anajuwa alichokiwa akikifanya kwangu. Hali ile iliendelea kwa wiki mbili mfululizo, siku moja alikuja akanipa kifuko cha Madawa ya kulevya akaniambia
“Tumia utakuwa sawa” Kutokana na jinsi nilivyokuwa natetemeka na kuhangaika ilinibidi nikubali kutumia madawa ya kulevya, basi nikawa naweka puani ndiyo najisikia unafuu na uchangamfu wa hali ya juu sana. Nikawa na nguvu ila nikawa sipendi kula chakula zaidi ya kupenda sana kuvuta yale madawa ambayo alikuwa akiniletea kwa kunikadilia sana, siku nyingine alikuwa haniletei hivyo nilishi kwa kuhangaika sana pale chumbani na kuishiwa nguvu, nilikuwa napiga mlango kwa nguvu ili aniletee madawa, nilijiona nimekuwa Mwanamke wa hovyo sana.
••••••••••••••
Alitumia mwanya huo kunitumia kingono kisha ananiahidi kunipa madawa ya kulevya, basi nilimpa penzi la kweli kabisa Juma Baro kisha ananipa madawa ya kulevya na pombe, alipoona nimekuwa Mtumwa akaniambia naweza kutoka na kwenda sebleni kukaa, basi nikawa natoka chumbani naenda sebleni nakaa hapo kwa muda fulani kisha narudi chumbani kwangu. Nilianza kuwa mlevi wa pombe na madawa ya kulevya, siku nyingine Juma alikuja chumbani kwangu na kuvuta pamoja na Mimi, tukawa marafiki mno
Nilijiona nimekuwa wa hovyo kuanzia mwili na akili yangu, nikawa nawaza pombe, madawa ya kulevya na kufanya mapenzi tu. Alikuwa akileta zile pombe kali sana!
Nakumbuka siku moja ilikuwa Usiku, Juma alikuwa Chumbani kwake na Mimi nilikuwa chumbani kwangu, alikuja haraka chumbani kwangu akaniambia kuwa polisi wanakuja, nilishajenga uadui na hao polisi kutokana na vitu nilivyokuwa natumia, nilimuuliza
“Tufanye nini sasa?”
“Tuondoke hapa haraka” Alisema Juma Baro, mara moja alirudi chumbani kwake na kuchukua Bastola yake, aliniambia nichukue vitu muhimu. Tukaelekea getini, ikawa ndiyo mara yangu ya kwanza kupunga upepo wa nje kwa zaidi ya mieizi mitano nikiwa nafungiwa ndani tu, ile anafungua geti na kutoka alipigwa risasi ya tumbo. Nilitupa vitu nilivyobeba kisha nikakimbilia nyuma ya nyumba, huko nikapanda juu ya Ukuta huku majibizano ya Risasi kati ya Juma Baro na polisi yakiwa yanaendelea, nilichumpa hadi nje, niliangukia kwenye kifusi cha mchanga ambacho kilinisomba kwa safari hadi chini ambako kulikuwa na kama machimbo ya Mchanga hivi, eneo hilo lilikuwa kimya mno alafu kulikuwa na pori, hakukuwa na nyumba yoyote eneo hilo, taa zilikuwa zikiwaka kwa mbali sana.
Niligeuka nilipotoka, nikaanza safari ya kukimbia kutoka pale na kuzifuata taa ambazo zilionesha kuwa ni makazi ya Watu, ujasiri ulinikamata kwa kiasi kikubwa ila tochi za polisi zilinifuata porini, kelele za mbwa zilisikika huku ile milio ya risasi ikiwa imekata kabisa nikajuwa tu lazima Juma Baro atakuwa ameuwawa.
Nilikimbia kwa umbali mrefu bila kupumzika ila baadaye nilihisi nguvu zikiniisha, tochi za polisi sikuziona tena, nilijitahidi kuendelea kukimbia ila baadaye nilianguka na kujigonga kwenye mti. Nilipoteza fahamu zangu sikujuwa kilichoendelea.
Fahamu ziliponirudia nilijikuta nikiwa kitandani, pembezoni mwangu alikuwepo Baba mmoja na Mama mmoja ambao walikuwa wakiniangalia sana. Sikujuwa hapo ni wapi na wale Watu ni akina Nani, nilijaribu kujiinua ila maumivu ya kichwa yalinizuia
“Polepole Binti utakuwa sawa tu” Alisema Huyo Baba
“Nipo wapi na nyie ni akina Nani?” Niliuliza huku nikiwa ninawatazama
“Upo sehemu salama sana, Naitwa Baba Nesha na Huyu ni Mama Nesha” Alisema Baba huyo kisha Huyo aliyemtambulisha kama Mama Nesha alisema
“Jinsi ulivyokuwa katika hali mbaya sikutegemea kama ungeamka na kujitambua, ulikuwa umepoteza fahamu kwa siku mbili” Alisema, nilishtuka sana
“Siku mbili?” Niliuliza kama vile sikusikia sawa sawa alichokisema
“Ndiyo, siku mbili”
“Jumaa….” nilitaka kuuliza kuhusu Juma Baro ila nilipokumbuka kuwa Mwanaume yule alikuwa Muuza Unga nikaacha
“Leo ni Juma tatu Binti” alijibu Baba Nesha akihisi labda nilitaka kuuliza ni Siku gani
“Hapa ni Rufiji”
“Rufiji?”
“Ndiyo kwanini umeshangaa? Tulikukuta Shambani kwetu ndiyo tukakuleta hapa Binti” Alisema Baba Nesha, nyumba yao ilikuwa nzuri sana na ilionesha walikuwa ni Watu wenye uwezo mkubwa kifedha.
“Unaitwa Nani Binti na nini kilikusibu?” Aliuliza Baba Nesha akionesha kuwa na hamu kubwa ya kutaka kujuwa, niliwaangalia ikanijia akili ya ghafla kuwa nisijimalize sana maana wanaweza kunichoma kwa polisi
“Naitwa Jojo” nilijibu
“Nini kimekusibu?” Aliuliza yule Mama
“Sikumbuki chochote” Nilisema kisha walitazamana
“Pole sana basi taratibu utakuwa unarejesha kumbukumbu” Nilikuwa na kovu upande wa kulia lililotokana na vurugu za kule nyumbani kwa Juma Baro kipindi cha nyuma nililishika, nililetewa Chakula lakini nilipokula nilitapika kutokana na ile hali ya kutumia madawa ya kulevya kwa wingi.
Walihisi labda ninaumwa, wakanitengenezea vyakula vilaini sana ambavyo angalau nilikula kidogo, niliishi hapo kwa Baba Nesha na Mke wake, walinichukulia kama Binti yao. Baba Nesha alikuwa ni Mtu wa kusafiri safiri kwasbabu alikuwa ni dereva wa Mabasi
Ile hali ya kuhitaji Madawa ya kulevya ilianza kunitesa, bahati nzuri wenyeji walikuwa wanywaji wa pombe hivyo angalau nilijituliza kwa kunywa pombe kali, lakini japo nilitumia pombe ila nilihisi mwili unakosa nguvu, nashikwa na baridi mara kwa mara.
“Unaumwa Jojo?” Aliniuliza Mama Nesha siku moja tukiwa jikoni “Hapana Mama nipo sawa” nilimjibu
“Nakuona ukiwa hauna amani, unatetemeka utasemaje upo sawa Jojo? Kama unajisikia homa basi nikupeleke Hospitali maana usije zidiwa usiku na Baba Nesha hayupo ikawa shida” Alisema Mama Nesha akiwa anaendelea kupika, mimi nilikuwa nimekaa tu
“Hapana Mama usijali nipo sawa tu” nilimwambia
“Haya! Ila Jojo tunakutendea vizuri hapa nyumbani?”
“Ndio Mama, siku 17 nilizokaa hapa naona nipo nyumbani, nashukuru sana nina amani ya Moyo wangu” Nilimwambia huku vipele vikianza kunitoka yaani vile vya msisimko wa kuhitaji madawa na hivyo ndivyo nilivyokuwa nikijisikia.
“Haya Nenda kapumzike” Alisema Mama Nesha ila kwa jinsi nilivyokuwa najisikia niliona bila kupata Madawa ya kulevya ningekuwa katika hali mbaya zaidi baada ya masaa kadhaa mbele.
“Mama naenda Dukani kununua Juisi” Nilisema
“Haya Jojo” Alijibu Mama Nesha, ila akili yangu ilijuwa nataka kufanya nini, kuna hela ambayo aliniachia Baba Nesha kama Elfu 40 niliona ni bora niutumie muda huo kutafuta Madawa ya kulevya. Nilikumbuka kuna sehemu Niliambiwa nisipite na Mama Nesha kwasababu Watu wa hapo ni wahuni wavuta Bangi hivyo nilijuwa tu nikienda huko nitapata madawa kirahisi mno, kingine nilishazijuwa mbinu na mameno ya kuzungumza ambayo Wahuni wangemielewa kwa haraka sana.
Haraka nikiwa nimevalia pensi na tisheti nilielekea huko, kweli niliona Kijiwe cha Watu watatu hivi ambao baada ya kuniona Mimi walikaa tayari, nilitoa ishara ya vidole ambayo Juma Baro aliniambia, ilikuwa ni ishara ya kuwaambia kuwa kuna amani, ishara hiyo ilikuwa ikitumiwa na Wauza unga pekee, walipoona Ishara hiyo walikaa kisha nilisogea hadi hapo, nilinunua kete mbili za madawa kwa shilingi elfu 20 kisha nilirudi kwa Mama Nesha nikiwa na shahuku ya kutuliza kiu yangu.
“Jojo?” Alisema Mama Nesha baada ya kusikia mlango ukifunguliwa
“‘Ni Mimi Mama, nimerudi” Nilisema mkononi nikiwa na Juisi ili kusiwe na maswali
Nini Kitaendelea?
Usikose SEHEMU YA SITA ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx
5 Comments
Unatusahau sana kama mungu wa Jojo mzee😀😀😀,,,tuletee kula siku hii kitu bhna🤣
Kaaaaah
Hauna baya mtunzi
Kila siku boss
Woowh hadithi nzuri sana