Ilipoishia “Tulienda moja kwa moja anapoishi Shonaa akaniambia kesho yake atanipeleka kwa huyo Bosi, nilikuwa nimechoka hivyo sikuwa na maswali mengi zaidi ya kuhitaji Kupumzika tu, kweli nilipumzika hadi asubuhi kulivyo pambazuka. Shonaa aliamka mapema sana, alikuwa amepangisha chumba kimoja na sebule, nilienda hadi sebleni nilimsalimia
“Mambo Dada?” Aliacha alichokuwa anakifanya kisha alitabasamu akanijibu
“Poa tu umeamka salama?” Aliniuliza
“Ndiyo nipo sawa! Umedamka hivyo?” Nilimuuliza
“Si unajuwa tena Maisha ya Mjini ndugu yangu, ukiendekeza Usingizi utakufa masikini” Alisema kisha tulicheka, niliona nimepata Mtu wa kuzungumza naye na kumuuliza maswali yangu
“Jana ulisema utanipeleka kwa Bosi asubuhi hii” “Usijali, subiria nimalize kupasi nguo zangu” Alijibu Shonaa
Endelea
SEHEMU YA PILI
“Unaitwa Nani?” Nilimuuliza
“Naitwa Shonaa, wewe ni Jojo Eeh?”
“Ndiyo Naitwa Jojo” nilijibu huku nikiwa ninatabasamu.
Punde mlango wake uligongwa waliingia wasichana wengine wawili ambao walikuwa wamelewa, walisema maneno ya hovyo hovyo kisha walipitiliza hadi chumbani, mmoja alinisukuma nikaangukia kwenye kochi, kiukweli nilishtuka sana.
“Usijali Jojo utazoea, ndiyo Maisha yetu” Alisema Shonaa nilimsogelea
“Ndiyo Maisha yenu? Ina maana mnaishi Watatu hapa?” Nilimuuliza Shonaa, alinisogelea akaniambia, Bado watatu hawajarudi
“Eeeh?” Nilishangaa Watu sita wanaweza vipi kuishi hapo
“Wewe ni wa saba Jojo, utazoea tu najuwa inakupa wakati Mgumu sana. Atakaye wahi kurudi analala Kwenye kitanda, ukichelewa kwenye kochi, ukichelewa zaidi unalala chini” Alisema Shonaa kisha aliendelea na kazi yake, kusema ule ukweli nilijilaumu kwanini nilikuja Dar, niliona ugumu ulio mbele yangu. Nilitoka ndani nikampigia Msonjo ili ikiwezekana nirudi Tabora mara moja, niliona ni bora kulala njaa kuliko Maisha yale
“Jojo tutapata wapi nauli ya wewe kurudi haraka hivyo? Vumilia kidogo mbona mapema hivi unakata tamaa jamani?” Ilikuwa ni sauti ya Msonjo
“Sikia Msonjo, yaani siwezi kuvumilia japo kwa sekunde moja, wewe haupo ila Maisha yanatisha hivi Watu wa Mjini ndio wanaishi hivi? Chumba kimoja Watu saba?”
“Jojo! Ngoja niongee na Bosi tuone inakuwaje!” Alisema Msonjo
“Jitahidi nakuomba Msonjo nipo katika nyakati ngumu sana” Nilisema kisha salio liliisha kwenye simu yangu, nilipogeuka nyuma nilimuona Shonaa akitikisa kichwa chake, alikuwa akisikitika.
Shonaa alirudi ndani bila kusema chochote ila alikuwa amesikia mazungumzo yangu, nilipofika ndani aliniambia
“Jiandae tuondoke” basi nilielekea chumbani, yaani nilikuta mazingira ya hovyo sana, jinsi walivyolala wamewekeana Miguu,
mwingine alikuwa ametapika karibu na begi langu, kichefuchefu kilinizonga. Nilijikaza tu hivyo hivyo nilibadilisha nguo, kisha nilitoka.
“Ndio unavaa hivyo?” Aliniuliza Shonaa
“Ndiyo kwni kuna tatizo?” Nilimuuliza
“Mmh! Haya twende” Alisema Shonaa kama vile kuna jambo alitaka kusema. Tulipanda daladala hadi Sinza kwa Remi, kulikuwa na kumbi kubwa mpya ya Starehe iliyoitwa Dar City ndiyo ilikuwa ikimilikiwa na huyo Bosi aliyeitwa Muntaza.
Tulienda hapo kwenye huo ukumbi, palikuwa pameshachangamka asubuhi asubuhi, Watu walikuwa wakipiga mitungi kama hawana akili nzuri, tena ilionesha walikuwa wamekesha hapo hapo, ilikuwa ni siku ya Jumamosi.
“Shonaa upo na mrembo” Alisema mmoja wa walevi kisha alimshika shonaa titi, alafu Shonaa hakuonesha kuchukia ndio kwanza alikuwa akicheka, nguvu ziliniisha
“Kama kawaida si unanijuwa Mimi” Alisema Shonaa kisha tuliingia kwenye chemba moja
“Shonaa haya Maisha sitoyaweza” Nilisema
“Jojo bado hujayaona Maisha tayari unasema hutoweza, sasa unaweza kurudi kwenu Tabora na huna pesa hata ya kula? Acha ujinga, fanya kazi hata mwezi mmoja kisha ndio uondoke…..unakata tamaa mapema, inabidi upambane kuhakikisha unapata pesa, hapa Mjini kila kitu ni pesa” Alisema Shonaa akiwa amenikazia jicho, kisha aliongoza mbele nami nilimfuata. Nilikuwa sijala ila Maisha niliyoyaona yalinifanya nishibe, hebu fikiria Mtu anashikwa Titi mbele za Watu alafu anacheka wakati Tabora Mtu umshike bega tu bila ridhaa yake anakupiga kofi, nilitikisa kichwa changu
Tuliingia kwenye chumba kimoja ambacho alikuwemo huyo Muntaza, kilikuwa ni chumba kinachonuka sigara na pombe, alikuwa na wasichana wawili makamo yangu. Aliwaondoa baada ya sisi kuwa tumeshaingia na kuketi kwenye sofa jirani na alipoketi yeye, nilijikuta naanza kukohoa kutokana na ule moshi. Muntaza alikuwa ni pande la Mtu, alikuwa na cheni nyingi na pete, alafu alikuwa na kitambi, umri wake ulionesha alikuwa zaidi ya miaka 50
Basi Shonaa alimsogelea na kumpiga busu huyo Muntaza, nilitazama pembeni nikiwa ninakohoa.
“Wow!” Alisema Muntaza
“Bosi huyu ni Jojo uliyeniagiza kumpokea” Alisema Shonaa, nilijichekesha kidogo ila kiukweli moyo ulikuwa ukinienda mbio sana.
“Hukumuelekeza mavazi ya kuyavaa?” Alihoji Muntaza “Ndio Mwanzo Bosi nitaongea naye vizuri”
“Ok! Muelekeze majukumu yake” Alisema Muntaza kisha aliondoka hata bila ya kunisemesha chochote.
Alpoondoka Muntaza nilizidi kukohoa, nilikuwa nimevaa gauni na mtandio kichwani.
“Jojo ukitaka kuishi hapa vziri kubali hali halisi ila ukileta misimamo isiyo na maana utajikuta Mji unakushinda huu. Hapa ndiyo ofisini kwako, kwangu na kwa wale wadada wengine tuliowaacha kule nyumbani, mavazi ya hapa ni kama yangu” Alivyosema hivyo nilimtazama alivyovaa, yaani alivaa kikomdomu tu na vest, chini raba
“Ukizubaa unapotea, kuwa mjanja”
“Lakini kusema ule ukweli Shonaa haya Maisha sina uhakika wa kuyaweza kabisa, najilaumu sana kuja huku Dar ila aliyenitafutia kazi nimemuomba anisaidie kuongea na Bosi ili anipe nauli nirudi kwetu” Nilisema.
“Usijidanganye kuhusu kupewa nauli, hata Mimi nilikuja kama wewe miaka miwili iliyopita, nilikuwa muoga nilikuwa nikilia nirudi nyumbani lakini ilishindikana”
“Lakini Shonaa mimi nimefiwa na Mama yangu mwezi uliopita, nahisi nitakuwa namkosea sana kufanya kazi ya hivi, alinilea katika mazingira bora sana” nilisema
“Sawa alikulea katika mazingira bora ila hakuacha msingi wowote, laiti kama angelikuachia msingi basi usingekuja huku kutafuta Maisha, hata Mimi Mama yangu nimemzika miezi michache iliyopita huko Kilimanjaro, nimerudi sababu hii ni kazi inayoendesha Maisha yangu”
Maneno ya Shonaa yalinikata sana kauli, niliona napaswa kukubaliana na hali halisi japo bado tumaini langu lilikuwa kwa Msonjo aliyenileta Dar. Kulikuwa na nguo zikizokuwa mle kwenye chumba alinipatia nizivae, nilijitahidi kukataa lakini aliniambia hakukuwa na sababu ya kutoka Tabora kuja Dar ni bora ningebaki Tabora. Basi nilizichukua nikabadilisha, sikujiangalia mara mbili, yaani chupi ilikuwa ikionekana, nguo zilibana na kushika mwili wangu, kila kiungo kilijichonga. Kibaya zaidi aliniambia nisivae sidiria
“Shonaa hivi siwezi kusema ukweli nitaweza vipi kutembea jamani mbona unanipa wakati mgumu hivi” nilisema, Shonaa alicheka sana. Kabla hata hajaongea chochote aliingia Muntaza
“Yupo tayari?” Aliuliza
“Ndiyo Bosi”
“Haya akaanze kazi” Alisema kisha alijitupa kwenye Sofa akiwa anakohoa. Ningefanyaje unafikiri? Nilitoka na Shonaa bila ubishi wowote ila nilikuwa navuta vuta nguo zangu ili zisinichonge hapa mbele kwa Bibi.
Siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza katika Maisha yangu kufanya kazi ya Ubaamedi, nilikutana na vikwazo vingi ikiwemo kushikwa shikwa lakini nilijitahidi kukwepa kadili nilivyoweza. Saa 12 walikuja wengine, Mimi na Shonaa tulirudi nyumbani kupumzika. Nilipewa elfu 10 kama pesa ya siku ya kazi, niliiweka pembeni ili ikitimia pesa ya Nauli niondoke zangu.
“Umeionaje siku yako ya kwanza kazini?” Aliniuliza Shonaa
“Nzuri tu” Nilisema kisha nilitoa tabasamu feki, sikutaka tena kujionesha kuwa kazi hiyo nilikuwa siitaki, kwakuwa niliona naweza pewa kila siku elfu 10 hivyo ningeweza kurudi Tabora haraka sana.
“Najuwa unaumia Jojo ila utazoea tu sababu hata Mimi nilikuwa kama wewe siku ya kwanza naanza kazi, nilikuwa mnyonge, sikuzoea kuvaa hivi ila ilinibidi nikubali hali halisi”
Alisema Shonaa akiwa ananiangalia vizuri kama vile alikuwa akinikagua, nilionesha lile tabasamu feki
“Kuna nini?” Nilimuuliza, alinishika nywele zangu akazibana kwa kutumia mpira aliokuwa ameushika mkononi
“Wewe ni mzuri sana Jojo” Alisema kisha aliachia tabasamu lililotoka moyoni mwake kabisa, hata mimi niliachia tabasamu lililotoka moyoni
“Asante!” Nilimshukuru, tulikuwa wawili tu sababu wengine walienda zamu ya Jioni hiyo kurudi hadi asubuhi.
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU ya MUNGU AMENISAHAU bila kuacha comments hapo chini
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx Mungu Amenisahau xx
9 Comments
Fupi sana admin ila tamu ✌
Asantee admini
Duh Jamani jojo
Maisha hayo jamani
Jamani
Nzuri sanaaa
Daah Jojo jaman
Mbona sehemu ya Tatu ina chelewa? Au ni mimi sijaona
sehemu ya tatu admin