Ilipoishia “James, ni wazi bado unampenda Matilda, ni wazi kua ipo siku utakuja kunitelekeza na Mimba yangu kitu ambacho sipo tayari kitokee” akasema Neema akiwa anamsogelea James
“Neema sikutegemea kama ungekua katili kiasi hiki, hukupaswa kumtesa Matilda kiasi hiki hata kama lengo lilikua aondoke..”
“Ishia hapo hapo, James ulinipa ruksa ya kufanya kila jambo, inaonekana kua moyo wako umerudi nyuma, umerudisha mapenzi kwa Matilda si ndiyo?” akauliza Neema lakini James hakujibu chochote huku macho yake akiwa ameyapeleka kwa Matilda ambaye alikua njia panda sababu aligundua kua James alikua na nia njema kwake na wala hakushiriki kumtesa kiasi kile.
“Vizuri James, niliyajua yote haya pale niliposikia kua ulienda polisi kumwona Matilda, Sasa James inabidi uchague kitu kimoja, ilipofikia siko tayari kupoteza chochote” James akasimama baada ya kusikia Hivyo
“Unamaanisha nini?”
“Nitamwacha Matilda endapo utakubali kufunga ndoa nami” Akasema Neema
“Najua hilo lazima likupe wakati Mgumu sana sababu tukiachana tutalazimika kugawana Utajiri ulio nao, kama hilo ni ngumu kwako basi Nitamuuwa Matilda” James hakua na jibu lolote la kumpa Neema.
Hadi kufikia Usiku hakukua na taarifa yoyote kuhusu Matilda ni wapi alipo, Mtu pekee aliyefanikiwa kujua alikua ni James, hilo lilimpa mawazo sana, alikunywa pombe huku akitafakari yale aliyoambiwa na Neema, achague moja, kumwoa Neema au kukubali Matilda afe, kingine kilichompa mawazo ni kwamba Neema ni Mjamzito, kiu yake kubwa ilikua ni kupata Mtoto japo alikua na Mtoto na Matilda lakini Mtoto huyo alimkataa sababu alikua ni Mlemavu, Usiku huo hakutaka kuzungumza na Mtu yeyote zaidi ya kunywa pombe akiwa nyumbani kwake. Akajikuta akichanganikiwa kabisa, alikua na pesa nyingi lakini hakua mwenye furaha, sababu kubwa iliyopelekea kutokua na furaha ni maamuzi yake ya kumkataa Mtoto wake.
Siku iliyofuata, bado Matilda aliendelea kutafutwa bila mafanikio yoyote yale huku Mtoto wa Matilda akipatiwa matibabu Muhimbili kwa hisani ya Mama yake James, wakahangaika kila kona kumsaka Matilda, polisi bado wakaendelea kushikilia msimamo kua Matilda aliachiwa huru
Upande wa James aliamua kuelekea Hospitali ili amwone Patra kabla hajafanya maamuzi yoyote yale, akaambiwa kua Mtoto alisha hamishwa hapo siku tatu zilizopita, akapewa anuani ya Muhimbili, haraka akaelekea huko hadi kwa Daktari ambaye alikua na jukumu hilo la kumtibia Patra
Akapelekwa hadi kwenye Wodi ambayo alikuwepo Patra, moyo wangu ukaingiwa na uchungu sana, akalia ndani ya moyo wake, ni kweli Patra ni Mtoto wake lakini kilichomfanya amkatae ni ile aibu kua Mtoto huyo ni mlemavu, Bilionea kama Yeye awe na Mtoto mlemavu hakutaka kabisa kukubali ndiyo maana akaweka nguvu kwa Neema kuhakikisha anamzalia Mtoto, mambo yakaanza kwenda kombo huku tumaini la furaha likiingia huzuni
“Mbona unalia, una uhusiano gani naye?” akauliza Daktari, maana James alijitanbulisha kama Mfadhili, chozi likiwa linamtoka akimtazama Binti yake ambaye alikua ameshafanyiwa upasuaji, kilichomliza zaidi James ni kuhusu Matilda ambaye alikua akipewa mateso na Neema.
“Nimeguswa tu na Maisha yake, pengine anastahili kilicho bora zaidi” Akasema James huku akiwa anafuta chozi lake, kwa mara ya kwanza alijisikia vibaya sana kuhusu Patra.
“Usijali hali yake itaanza kuimarika kadili siku zitakavyokua zinasonga, tatizo lililokua likimsumbua tayari tumeshaliondoa” Akasema Daktari huyo.
Wakati huo Mama yake James na Mama Naomi wakiwa wanakuja hapo Hospitalini, Baada ya kushuka kwenye gari Mama James akamwambia Mama Naomi
“Sikulala usiku wa jana, japo sijamwona huyo Binti aliyezaa na James lakini nimejikuta nikimuwazia sana, sijui anafananaje” Alisema akiwa anafunga mlango wa gari
“Mama hata Mimi sipati usingizi tokea alipokua polisi, wakati mwingine nachoka lakini nikifikiria kuhusu yule Mtoto najikuta napata nguvu ya kuja hospitalini” Akasema Mama Naomi wakiwa wanaanza kutembea kuelekea wodini
“Hongera hakika wewe ni miongoni mwa wanadamu wachache ambao wana mioyo bora sana hapa Duniani”
“Mama Usijali sana namchukulia Matilda kama Mdogo wangu hivyo chochote chake ni changu pia” Maongezi yaliendelea wakiwa wanasogea wodini wakati huo James akiwa anamwambia Daktari
“Nitasimamia matibabu kuanzia sasa, kadi yangu ya Mawasiliano ni hii hapa, kwa chochote nijulishe” Akampatia kadi Daktari
“Mungu akuongoze ukaguse Maisha ya wengine wenye uhitaji Mr. James” Akasema Daktari bila kujua kua aliyekua mbele yake ndiye Baba wa Mtoto, Basi James akamuaga Daktari kisha akatoka wodini wakati huo Mama yake akiwa anafika hapo, wakapishana kidogo tu, James anageuza kisogo Mama naye ndiyo anaingia akamkuta Daktari Daktari akiwa ameshikilia kadi
“Karibu Mama, karibuni sana” Akasema Daktari huyo kisha akaitia kadi mfukoni
“Hali ya Mtoto inasemaje?” akauliza Mama James huku Mama Naomi akiwa anatabasamu kwa namna mashine zilivyokua zikionesha hali ya Patra
“Hali yake Mungu anasaidia sana tena ashukuliwe zaidi na zaidi sababu pasi na yeye hakuna Uhai wa Binadamu yeyote” Wote wakatabasamu kwa maneno ya Busara ya Daktari
Mchungaji George akawatangazia waumini wa kanisa lake juu ya Mwenendo mzima wa Matilda na Binti yake sababu baada ya mchango ule hakusimama Madhabauni na kuzungumza, akawaambia hali halisi ya kinachoendelea huku akiwataka waumini kutoa taarifa endapo watasikia au kumwona Matilda, kila mmoja alisikitika sana, ikawa gumzo kanisani hapo
“Ikibidi tufunge na kusali ili Mungu atuoneshe ni wapi alipo Matilda” Akasema Mchungaji
“Ameen” Waumini wakaitikia
Mchungaji George akaanza maombi pamoja na waumini wote ili Matilda apatikane popote alipo, pia hali ya Mtoto wa Matilda iimarike zaidi na zaidi.
“Mama, ilipofikia naona kama naenda kushindwa” Akasema Neema mbele ya Mama yake, macho ya Mama Neema yakagongana na ya Binti yake kisha akamtazama Masudi
“Kwanini unasema hivyo?”
“James amerudi kwa Matilda. Nimefanya kama ulivyoniagiza lakini inaonekana wazi kua ameanza kurejea upande wa Matilda” Akasema Neema huku akiketi kwenye sofa
“Kwa dawa ambazo ulikua ukimpa kwa kipindi chote sidhani kama anaeza akathubutu kufanya hivyo, maisha yetu yamebadilika Neema, hii ni ishara kua dawa zinafanya kazi. Cha Msingi ni kuvuta subra ili aamue jambo letu”
“lakini Mama anachosema Neema kina ukweli sababu jamaa haeleweki sasa hivi, si kama zamani…” Akadakia Masudi
“James hawezi kubadilika isipokua ni hofu zenu tu, tulishamtengeneza vya kutosha, kala limbwata za kutosha inawezekana vipi ndani ya muda mfupi mseme amebadilika? kumbukeni huu ni mpango wa kufanikisha kupata pesa kwake, kama ni hivyo basi Ujauzito hauna maana tena” Akasema Mama yake Neema
“Bado namshikilia kwanza Matilda ili nione msimamo wa James utakua vipi, alafu pili nataka nijue Hospitali aliyolazwa Mtoto wa Matilda, hiyo inaweza kua karata nyingine sababu Hospitali ya Mwanzo hayupo” akasema Neema huku akiangalia Ujauzito wake ambao ulianza kukua
“Neema nafikili ulifanya makosa pale mwanzo, ulipaswa kumuuwa Mtoto akiwa tumboni na siyo kumfanya azaliwe kilema, haya yote yasingejitokeza sasa hivi, huu mvutano unatokana na yule Mtoto, sasa inabidi tumuuwe tu hakuna njia nyingine” Akasema Mama yake Neema
“Mama, Kwasasa nakusikiliza wewe tu. Chochote ambacho utakiamua nitakifwata sababu naona mambo yanataka kuniendea kombo”
“Basi mpigie simu Babu yako, Mwambie amuuwe Mtoto usiku wa leo ili asubuhi kuwe na habari nyingine, kama ulivyosema karata pekee inayoweza kutufanya tukatimiza adhma yetu ni kumuuwa yule Mtoto kwanza” Akasema Mama Neema kisha akaketi pia huku Masudi akifuatia kuketi
Mpango mpya mbele yao ukawa kwanza kujua Mtoto amelazwa Hospitali gani, kama alivyosema Mama yake, Neema akampigia simu Babu yake ambaye alikua Mchawi haswa na ndiye aliyesababisha Matilda akazaa Mtoto mlemavu. Babu yake alikua haishi mbali sana na Jiji la Dar, alivyopata simu ya Neema, haraka akaingia Dar akitokea Kiluvya – Kibaha.
Babu yake Neema aliyeitwa Mzee Mapinduzi, akajaribu kuangalia namna ya kufanya lakini ikawa ngumu kujua Mtoto mahali gani alipo, Maombi ya Mchungaji George yalionekana kuzuia jambo hilo kufanyika, akawaambia
“Simwoni Mtoto, Mna hakika yupo hai?” akauliza Mzee Mapinduzi wakiwa sebleni
“Babu, Mtoto yupo hai, Hospitali ya mwanzo alihamishwa” Akasema Neema
“Simwoni ndiyo maana nauliza, kuna kitu gani kinachozuia hapa?…”
“Basi Babu, nitafanya jitihada za kujua yupo Hospitali gani, kesho tutajua Hospitali ambayo Mtoto amelazwa” Akasema Neema
Wakati Neema na familia yake wakipanga namna gani wafanye, Usiku huo Mama yake James akamwita James nyumbani kwake, Haikumpa Mshituko James sababu alijua Mama yake hafahamu chochote kile kinachoendelea, Mama yake James hakutaka kumwonesha chochote kijana wake kua anajua kinachoendelea, akamuuliza
“Hivi Neema anaendeleaje, Maana tokea ile siku umemleta hadi hivi leo sijamtia machoni, nawe husemi chochote kile” Sura ya James ikapoteza Uchangamfu kidogo baada ya kusikia swali la Mama yake, akamjibu
“Neema anaendelea vizuri tu Mama, ni majukumu ya hapa na pale ndiyo maana unaona kimya, hata hivyo nilipanga kuja naye ila nikaona ni usiku nikamwacha apumzike”
“Hivi James, katika pitapita zako hauna hata Mtoto wa kusingiziwa kweli Mwanangu?” akauliza Mama yake kwa utani hivi huku akitabasamu, James naye akatabasamu kidogo lakini moyoni swali hilo lilimpa pigo takatifu
“hapana Mama, sitaki litokee hilo, unajua ukishakua na hela basi kila Mwanamke atataka kusema hivyo, siwapi nafasi kabisa, Mjukuu pekee yupo kwa Neema, tarajia mazuri” Akasema na kujichekesha,
“Haya Mwanangu, Nami Mama yako natarajia mazuri kutoka kwako na Neema, natamani sana kuitwa Bibi..”
“Usijali Mama yangu, muda siyo mrefu utapata Mjukuu wako…” Wakazungumza kwa dakika kadhaa kabla ya James kuondoka.
Maisha ya James yalibadilika hasa kutokana na kile kilichokua kikiendelea, akahisi labda ni Mkosi wa kumkana Mtoto ndiyo umepelekea kuingia katika nyakati ngumu ambayo kuingia kwake ilikua rahisi lakini kutoka ikawa ngumu sana, alipewa siku tatu na Neema ili atoe jibu kama yupo tayari kwa ndoa, akilini mwake alishajua Mwanamke huyo alikua na tamaa ya kuupata Utajiri wake lakini hakua na njia ya kumkwepa sababu aliamini ana Mtoto wake tumboni, aliendesha gari kwa spidi sana hadi nyumbani kwa rafiki yake Chilo
Mara nyingi alipokwama alipewa ushauri na Chilo lakini siku hiyo ilikua tofauti sana, Chilo alikua na Mke wake, aliziona simu za James zikiingia lakini Mke wake akamwambia
“Mwache Dunia imfunze, hiyo ni laana ya kumkataa Mtoto, usiku huu akusumbue Mume wangu Akhaaa” Alisema akiwa anamkumbatia Chilo ambaye aliyakubali maneno ya Mke wake, James alipiga sana honi bila mafanikio yoyote yale kitu ambacho hakikua kawaida, akashuka na kugonga geti kwa nguvu lakini hakuna aliyefungua geti, akajaribu kumwita Chilo lakini hakupokea jibu lolote lile, akazidi kuchanganikiwa, akarudi kwenye gari, akaketi kumsubiria Chilo akiamini huwenda hajarudi Usiku huo, akajikuta amepitiwa na Usingizi Mzito sana.
Alipokuja kushtuka palikua tayari pamepambazuka, alishtuka, hakuamini Bilionea kama yeye alale ndani ya gari, Mara Mke wa Chilo akafungua geti wakati James akiendelea kujikagua, haraka akashuka kwenye gari huku akipiga mihayo ya Uchovu
“Habari Shem, mbona asubuhi mapema hivi kuna tatizo?” aliuliza Mke wa Chilo kama vile siyo yeye aliyesababisha James akalala kwenye gari, James alipoona Mke wa Chilo hajui kama yeye alilala hapo akajifanya kuzuga
“Nilikua na Mihadi na Chilo, ndiyo nimekuja lakini kama hajaamka, basi kuna mambo naenda kuweka sawa kisha nitawasiliana naye” akasema James kisha akarudi kwenye gari, akaondoa gari hapo huku Mke wa Chilo akitabasamu tu
“Na bado. wanaume wa namna hii wanaishia kuishi Maisha ya Kimasikini sababu ya laana za kujitakia” Akasema huku akilisindikiza kwa macho gari la James
Mahali ambapo Matilda alihifadhiwa alihamishwa na kupelekwa sehemu nyingine sababu James alikua ameshapajua, mpango ulio mbele ni kumuuwa Mtoto wa Matilda ili James akose nguvu.
Akatumwa Masudi kupeleleza ni wapi ambapo Mtoto amepelekwa, Akaelekea Magomeni Hospitali, akaambiwa kua Mtoto yupo Muhimbili, haraka akampigia simu Neeema na kumpa taarifa,
Taarifa hiyo hiyo ikamfikia pia Mzee Mapinduzi, akamwambia Neema
“Chukua hii, katupe Muhimbili, katikati ya Hospitali, inaonekana kuna nguvu inayonizidi ndiyo maana simwoni Mtoto” Akasema Mzee Mapinduzi, akampatia Neema kitu mfano wa pipi tena akamsistiza
“Hakikisha mahali hapo Mtu hawezi kuokota wala kuigusa, ikae hapo ili nimshughulikie” Haraka Neema, akaingia kwenye gari akawaacha Mama yake na Babu yake wakiendelea kuzungumza huku wakisubiria Neema akafanye tukio hilo.
Ndani ya Hospitali, mambo yalikua shwari kabisa sababu hali ya Patra ilianza kukaa sawa, maombi ya Mchungaji na Matibabu ambayo Mama James aligharamia yaliimarisha afya ya Mjukuu wake japo alifanya kwa siri James asijuwe, Patra alikua akitabasamu huku akitazama walio mzunguka, alionekana kuhitaji kuuliza ni wapi alipo Mama yake lakini Mtoto huyo alizaliwa akiwa hajui kuzungumza kutokana na Uchawi ambao familia ya Neema ilimfanyia, Mbele ya Patra alikua amesimama Mama James ambaye ni Bibi yake, Mama Naomi, na Mchungaji George
“Hakika Mungu aliye hai ametenda miujiza” Alisema Mchungaji George kwa Furaha kubwa kutokana na hali ya Patra ilivyokua ikiimarika
“Asante sana Mchungaji, maombi yako yamesaidia sana, mara ya kwanza nilivyomwona Mtoto huyu roho yangu iliumia sana, Malaika asiyejua chochote alikua akiteseka sana, hadi kua hivi leo ni Miujiza tu” Alisema Mama Yake James
“Itakua siyo busara kama tutasahau kumshukuru Mama Naomi, ni ngumu Dunia ya sasa kupata Jirani kama Mama Naomi hasa katika Jiji hili ambalo kila Mtu yupo bize” Akasema Mchungaji
“Ni kweli kabisa, Asante Mama Naomi, Mjukuu anaendelea vizuri. Sasa kilicho mbele yangu ni kuhakikisha tunampata Matilda ili ashuhudie Muujiza huu” Akasema Mama yake James
Muda huo Magari mawili yalikua yakiingia Hospitalini hapo kwa kupishana dakika tano, aliyekua wa kwanza kuingia alikua ni James, alipotoka tu kwa Chilo aliona ni bora alekee Hospitali kumwona Patra sababu nafsi ilikua ikimsuta sana. Akaketi
kwenye gari iliyo Paking kwa dakika kadhaa akitafakari namna mambo yalivyokua yakiendelea, Gari ya pili ilikua ni gari ya Neema, kila mmoja aliegesha gari kwa upande wake lakini James alikua na nafasi ya kumwona Neena sababu alikua amepaki sehemu yenye magari mengi, akaliona gari la Neema likiingia akajiuliza Neema amefuata nini pale Hospitalini. Endelea
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
14 Comments
Waooooo
Story nzuri sana, hongera sana, inafundisha, inasisimua na inatupa burudani
Moto unawaka lazima Mungu ajitambulishe kawaida kila mashauri ya Shetani na Mawakala wake lazzima ya simame
Nikizeeka nitawasimulia wajukuu iih story nitawaambia ilimkuta mjamaa mmoja anaitwa adimini aaahaa
Next please 🙏 yaan Ni🔥
Ujawahi kukosea admini
Jaman si utoe asubihi na jion Admin maana hii ki2 ni 🔥🔥
Alaniwe nakila mwenye mipango yakudhuru kwa mwenzake
Inazidi kunoga
daaah! Neema anakwenda kuumbuka
Mambo ni moto inazid kuwa fire
NOMAAA🔥🔥🔥🔥🔥
ahsante admin nasubir sehem ya nane
Glory to God