Ilipoishia โSijapata kumwona Mwanadamu Mbishi na Mgumu kama huyuโ aliutupa mkono wakeย uliojaa damu kwa hasira sana kisha akarudi kuketi kitini akitafakari ni namna gani afanye iliย apate taarifa nyeti. Haraka akanyanyuka kutoka kitini kwa hasira akamfwata tena Elizabeth,ย akamwambia
โUkiendelea kuwa jeuri utamfuata Rais alipoโ alisema kisha akaondoka ndani ya chumbaย hicho, haraka Elizabeth akatambua fika kua Rais alikua ameshauawa na kilichokua kinaendaย kufanyika ni Uasi mkubwa wa kuitawala Nchi.ย
Elizabeth akiwa ananingโinia akaukumbuka Usiku wa Heka Heka. Endeleaย
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
MSATA. SAA TANO USIKUย
Elizabeth alifika Msata akiwa amebadilisha mwonekano wake kama Msichana mwenyeย mambo mengi mjini, aliweka kope Bandia, akaweka kucha, alivalia gauni fupi lenye mgโao,ย juu aliweka Wigi fupi ambalo lilimfanya aonekana kama siyo yeye, eneo ambalo alielekezwaย na Zagamba wakakabidhiane Nyaraka M21 lilikua ni Msituni.ย
Akaiweka gari kando ya Barabara kisha taratibu akaingia Msituni, Hapo aliambiwa kuaย atakutana na Mtu wa Zagamba aliyepewa kazi ya kupeleka Nyaraka kwa Zagamba, alipoanzaย kukaribia aliona tochi, akajua ndiye anayepaswa kuonana naye hapo. Akaiweka sawa Bastolaย yake ndogo aliyoitoa kutoka kwenye mkoba wakeย
Akatembea taratibu tena kwa tahadhari kubwa sana, hakutaka kumwamini yeyote. Mkononiย alivalia kifaa chenye GPS ambayo ilikuwa inamwezesha Muhonzi kuona mitembeo yaย Elizabeth na kujua yupo wapi. Alipofika hapo alikutana na mwanaume mmoja aliyevalia kotiย jeusi, ndani zaidi ya Msitu mzito wenye kiza kizito kisicho na nuru kabisaย
Chini ya Mti mmoja ndipo alipokuwepo Mtu huyo.ย
โUna mzigo?โ aliuliza Mwanaume huyo, Elizabeth akamjibu kwa umakini โSiwezi kukupa mzigo bila kuona namna utakavyonipa pesaโย ย
โBinti, Bilioni 30 ni ngumu sana kutembea nazo hata kama zipo kwemye mfumo wa Dola.ย Nimeziacha ndani ya gari, naomba nione hizo nyaraka kwanza ndipo nikupe pesa yakoโย Mazungumzo haya yalikua Mubashara kwa Muhonzi.ย
Elizabeth akatoa Flashi akampatia Mwanaume huyo asiye mfahamu, kisha Mwanaume yuleย akawasha kifaa chenye mfanano na Kompyuta Mpakato akaiingiza Flash na kuhakiki, akatoa tabasamu la kuchanua ambalo lilimpa ishara Elizabeth kua Mtu huyo hakua na lengo zuriย kwake, hakuishia hapo aliangusha kicheko.ย
Haraka Elizabeth akaichomoa Flash kutoka kwenye kompyta kisha akamnyooshea Bastolaย Mwanaume huyo.ย
โPesa nikupe Nyarakaโ alisema, mkononi alikua na tocho ndogo lakini alipommulika vizuriย alimwona Mwanaume huyo akiwa na mavazi ya Usalama wa Taifa, akajua wazi kua alikuaย ameingia Mtegoni.ย
โOooh taratibu Elizabeth, pesa yako ipo ndani ya gari. Ok, ongozana na Mimiโ alisemaย Mwanaume huyo, Elizabeth akaongeza umakini wa kutosha baada ya kugundua hapo Msituniย hapakua eneo salama kwake.
Akayaangaza macho yake kama Paka mwizi, kisha akamsukuma mbele yule Mwanaume iliย amtumie kama chambo cha yeye kutoka pale Msituni, akilini mwake alishaiuwa Biashara yaย Nyaraka zile za siri baada ya kuona dalili za uwepo wa hatari. Hatua za yule Mwanaumeย zilikua za mahesabu makali sana, Elizabeth alishaligundua hilo sababu alikua Jasusiย
Sauti ya Muhonzi ikasikika Masikioni mwa Elizabeth, ikamwambiaย
โNaona uwepo wa Watu zaidi ya Mmoja hapo Msituni, haraka Ondokaโ alisema kishaย Elizabeth akajibu kwa Ukimya huku sauti za Majani makavu yaliyokanywagwa zikiendeleaย kusikika. Moyo wa Elizabeth ukaanza Riadha ya haraka, nywele zikamsisimka vya kutoshaย huku vipele vidogo vidogo vya Tahadhali vikianza kumtoka.ย
Hatua ya sita ya yule Mwanaume ilimfanya Elizabeth ashuhudie teke kali likimuelekea,ย kwakua tayari alishaanza kuzihesabu hatua za yule Mwanaume na kujua hatua hizoย alilikwepa teke kwa haraka huku akiukunja mgongo wake kuelekea mbele, aliporudiย alikutana na kipande cha mti kilichotua eneo la tumbo na kumjeruhi.ย
โMshenzi unafanya nini?โ aliuliza Elizabeth, hapo akajua fika kua taarifa za yeye kua ndaniย ya Msitu zilishauzwa muda mrefu hivyo kituo kinachofwata ni kukamatwa na kuuawa kikatiliย na Wanaume hao wenye sare za Ikulu, kwa haraka akili yake haikuchekecha vyema na kujuaย ni Nani aliyeuza mpango huo, akajikaza ili atoke ndani ya Msitu.ย
Bastola ilikua imeshamtoka, kutokana na giza zito hakufanikiwa kuiyona mahali ilipoย dondokea, mkononi alikua na Flashi yenye nyaraka, akaisweka haraka ndani ya chupi naย kuifunga kwa zipu kisha akajiweka sawa kukabiliana na Mwanaume huyo aliyekua na tamboย za kutosha kua angemmaliza Elizabeth hapo Msituni.ย
Tochi ilikua pembeni, Elizabeth alipoutoa mkono tumboni alihisi uwepo wa damu Mbichiย yenye harufu, ikampa hasira, akamvaa Mwanaume yule mwenye ngumi nzito.ย
Akashusha mvua ya ngumi nyepesi alizolenga sehemu moja, kisha akaachia pigo zito kwaย kutumia skuna yake iliyomtoboa yule Mwanaume eneo la shavu. Akatema damu hukuย akigugumia kisha akapiga filimbi ya kuita Watu wengine walio pale Msituni, dakika moja tuย alishajua kupambana na Elizabeth isingelikua kazi rahisi kuifanya.ย ย
Tochi zikaanza kutapakaa pale Msituni, Elizabeth akamshushia na teke takatifu lililomlazaย yule Mwanaume kisha akaanza kukimbia ili kuokoa Maisha yake huku akivuja damu, eneoย ambalo alikatisha lilikua na Miiba ya kutosha iliyomkwangua kila eneo la mwili wake naย kumchania nguo.ย
Alikatiza ndani ya Msitu wenye giza nene huku akijua fika kua hapakua na Umbali mrefuย kutoka hapo kuelekea Barabarani alipoacha gari yake, lakini haikua rahisi kufika Barabarani,ย ilimtaka atumie nguvu zake zilizoanza kumsaliti. Alikimbia huku akifukuzwa na Wanaumeย kadhaa wenye tochiย
La haula!ย
Akafika Barabarani lakini hapakua na gari yoyote, eneo ambalo alitokea halikua lile eneoย aliloingilia, akaanza kuifukuza ile Barabara asijuwe anasonga mbele au anarudi nyuma, gizaย
lilikua la kutosha na hapakua na dalili ya kutokea kwa gari au Pikipiki, akamwambiaย Muhonziย
โSijui kama nitachomoka salama Muhonzi, hali yangu siyo nzuriโ akasema kisha akakitupaย kifaa chake cha Mawasiliano, Bahati nzuri akamulikwa na taa ya gari kutokea nyuma yake,ย akasimama na kupungia mkono gari isimame.ย ย
Ndani ya gari alikuwamo Benjamin Kingai, rubani wa Shirika la Air Tanzania aliyekuaย akitokea Arusha kwa Mpenzi wake, gari iliposimama akafungua mlango na kuingia harakaย kisha akamwambia yule dereva kuaย
โOndoa gari Harakaโ Benjamin akiwa mwenye taharuki akawaona wanaume wenye Silahaย wakitokea Msituni, haraka akaliondoa gari bila kuuliza swali lolote.ย
**ย
Ndani ya Ikulu. Saa 9 Alhasiri.ย
Waziri Mkuu Haji Babi, alielekea eneo la siri ambalo Rais alikua akitesa na kuuwa Watesiย wake, akaingia kwenye moja ya chumba ambacho alikuwamo Mke wa Rais Lucas Mbelewa,ย hakutaka kutangaza kifo cha Rais Bila kupatikana kwa Nyaraka za siri ambazo zilikuaย mikononi mwa Elizabeth.ย
Alipofika alimkuta Mke wa Rais akiwa ameketi sakafuni, Haji Babi akasogea naย kuchuchumaa mbele ya Mke wa Rais kisha akamwambiaย
โMasaa machache yajayo nitatangazwa kua Rais wa Nchi hii, hakuna Mtu wa karibu waย Lucas atakayebaki kua hai. Una nafasi moja ya kuishi, nieleze unafahamu nini kuhusuย Nyaraka M21?โ alihoji Haji Babi akiwa amekaza macho yake kuelekea alipo Mke wa Rais. Hofu ya Haji Babi ni kua Nyaraka hizo zina siri zake pia kwani viongozi wengi wa ngazi zaย juu walikua kwenye nyaraka hizo.ย
Mke wa Rais alikua kimya huku akilini akijiuliza ni jambo gani lililomfika Rais, akiwa katikaย tafakari akanyanyuliwa na kupelekwa kwenye chumba kingine ambacho kilikua na jokofu laย kuhifadhia Maiti, humo ndimo mwili wa Rais Lucas ulikuwa umehifadhiwa.ย
Mke wa Rais akawa anatetemeka, ujanja wote akautia mfukono, waziri Mkuu Haji Babiย alionesha wazi kua alikua siyo Mtu mzuri, japo Mke wa Rais alihitaji Rais atoke madarakaniย lakini hakutegemea kama angetolewa kwa njia hiyo ya Uwasi, jokofu lilipofunuliwa akaambiwaย
โNenda kaangalie kuna nini ndani yakeโ alisema Waziri Mkuu, kisha akatoa tabasamu panaย huku akisigina kiatu chake sakafuni, Mke wa Rais akasogea hadi kwenye jokofu, aliiyonaย maiti ya Rais. Mwili huo ulikua na matundu ya Risasi, alijikuta akiishiwa nguvu, Waziriย mkuu akamdakaย
โSasa unapaswa kua upande wangu Mke wa Rais, nitayafungulia Maisha yako yaliyokuaย yamefungwa na Lucas, nyota yako itawaka tena kwenye Siasaโ akasema Waziri Mkuu hukuย akiwa anamwonesha tabasamu pana sana, alionekana kujua siri nyingi za Maisha yaย Marehemu Rais Mbelwa na Mke wake.
Akaagiza Mke wa Rais awekwe kwenye chumba kingine kwa uangalizi mkubwa, akawekwaย kwenye chumba kizuri ambacho alipewa kila kitu isipokua simu, Mpango wa Waziri Mkuuย ukawa ni kutaka kuitawala Nchi, aliporudi ndani ya Ofisi ya Rais akampigia Simu Muuwajiย wake wa kuaminika, akamtaka awasili hapo Ikulu jioni hiyo ili ampe kazi ya kusafisha woteย anaowahisi watakua kikwazo kwenye Utawala wake.ย
**ย
Hatma!!ย
Baada ya kutoka Black Site akiwa amechoka sana Bi. Sandra alikua akiegesha gari lakeย kwenye jumba moja la ghorofa ambamo ndimo alimokua akiishi, Ulikua usiku umeshaingia,ย nywele zake alizozifunga kwa nyuma zilikua zikimfuata kila aendako.ย
Palikua kimya sana, kichwani alikua na mawazo tele, kwanza alihitaji hizo nyaraka za siriย ambazo Elizabeth alikua nazo na pia alifikiria sana kuhusu Mauwaji aliyoyafanya kwa Raisย Lucas Mbelwa. Kwa kiasi kikubwa alianza kujiona mwenye hatiaย
Akalisogeza gari hadi maegesho, alipomaliza alishuka ili aelekee juu ambako alikua akiishi,ย eneo la maegesho lilikua na magari mengi, pia palikua na giza la wastani lakini ambaloย haliwezi kuyashinda macho yake, akapiga hatua kadhaa lakini akahisi uwepo wa Mtu nyumaย yake, akasimama kisha haraka akageuka lakini hapakua na Mtu yeyote yule.ย
Akashusha pumzi nzito ya wasiwasi, palikua kimya kuliko kawaida. Alipogeuka mbeleย alimwona Mtu mmoja aliyevalia suruali ya Jinzi ya Bluu, shati jeupe alilolichomekea vizuri.ย Akapata ahueni, akatabasamu kisha akaendelea mbele.ย
Yule Mtu alikua Mwanaume aliyeenda hewani, mweusi mwenye mwili uliojengeka vizuri,ย alipokaribiana na Bi. Sandra alianza kutafuta kitu mfukoni mwake lakini kwa Bahati mbayaย aliangusha Karatasi alizokua amezibeba, akainama kuokota, Bi Sandra akajikuta tuย akimsaidia kuziokota maana zilikua zimetawanyika sana.ย
Namna ambayo Bi. Sandra alikua akiishi ni ngumu sana kugundua alikua Muuwaji waย kuaminika.ย
โOoh Ahsante sanaโ alisema Mwanaume huyo baada ya Bi Sandra kumpatia karatasiย alizokua ameziokota.ย
โSiku nyingine uwe makiniโ akasema Bi. Sandra akiwa anampa tabasamu Mwanaume huyoย aliyemzidi umri parefu sana. Alipotaka kuachana naye Mwanaume yule akamwambia Bi.ย Sandraย
โSamahani Naitwa Skandaโ alisema huku akitabasamu kama Mtu aliyehitaji ukaribu na Bi.ย Sandra, hakujua Mtu aliyekua akizungumza naye alikua Mtu wa namna gani, haraka Bi.ย Sandra akajua Mwanaume huyo alihitaji ukaribu, alizungumza akiwa amempatia mkono Bi.ย Sandra.ย
Bila Hiyana Bi. Sandra alirudisha tabasamu pamoja na Mkono, akampa Mwanaume huyo.ย Sekunde moja tu ikabadilisha kila kitu, yule Mwanaume akaubana mkono wa Bi. Sandra kwaย nguvu huku akitabasamu,kwa kutumia ujuzi wake Bi. Sandra akajitoa
Alipojiangalia aliona ana tundu dogo linalotoa damu, kisha ghafla nguvu zilianza kumwisha,ย akachomoa Bastola yake ili amshambulie Mwanaume huyo aliyekua amesimama mbele yake,ย cha ajabu Mwanaume yule hata hakujitingisha, pale pale Bi. Sandra alianguka na kuanzaย kutapa tapa, yule Mwanaume akaangalia huku na kule kisha akauvuta mwili wa Bi. Sandra naย kuuingiza chini ya gari yake, halafu akajikungโuka vumbiย
Akaitoa simu kutoka mfukoni kisha akapiga mahali.ย
โNani anafuata?โ akauliza Mwanaume huyo, Naaam!! Mpango wa Waziri Mkuu Haji Babiย ulianza kufanya kazi, tayari Muuwaji alikua kazini kufyeka wote anaowahofia kwenyeย Utawala wake. Maisha ya Bi. Sandra yakaondoka kizembe.ย
**ย
Waziri Mkuu Haji Babi, akaketi kwenye kiti cha Rais akiwa anagida mvinyo, muziki waย taratibu ukiwa unamburudisha huku Muuwaji wake akizidi kufanya Mauwaji Usiku huo,ย hakuishia kwa Bi. Sandra, akammaliza Balozi akiwa ndani ya gari kwa kutumia kitambaaย chenye Sumu.ย
Mauwaji haya yalifanyika kwa siri nzito na uharaka wa ajabu sana, kipaumbele sasa kikawaย ni kupata Nyaraka za siri zilizopewa jina la M21, akamtuma Muuwaji wake wa kuaminikaย kwenda Ilipo Black Site kumchukua Elizabeth Mlacha. Akampa ramani ya mahali ilipo Blackย Site, akaondoka Usiku huo huo na gari ndogo aina ya Carrina C4 kuelekea Black Site.ย
Kitu pekee kilichobakia kwa Waziri Mkuu ni kupata nyaraka ili kifo cha Rais kitangazwe,ย Upande wa pili ndani ya Godauniย
Muhonzi akafanikiwa kukata kamba alivyofungwa, giza lilikua nene ndani ya Chumbaย alichohifadhiwa, akajaribu kuchungulia dirishani kwa mtindo wa kuruka sababu dirishaย lilikua juu sana lakini hakuambulia kuona chochote kile, akajaribu kuitaย
โKuna nani hapo nahitaji Majiโ aliita kwa makusudi huku akifahamu fika kua eneo hilo linaย ulinzi mkali kuhakikisha yeye hachomoki, akaita tena, ndipo aliposikia hatua za kiatu zikijaย upande wake, akarudi haraka kuketi sakafuni alipokua ameketi.ย
Mara taa ikiwashwa, kisha akatupiwa maji aliyoyataka.
Nini kitaendelea?ย
Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
8 Comments
wakwanza kuisoma
Ni mimi
๐ฅ๐ฅ
๐๐๐
Msalaa ๐๐
Weeeee weee hatar na nusu
Jaman masala ni moto wa quotes mbali admin umeweza
Nzuri