Soka la bara la Afrika limeanza kupiga hatua limeanza kukuwa sana kuanzia ndani ya uwanja mpaka nje ya uwanja, kwa sasa vilabu vingi vilivyoonekana vya kati na hata vya chini navyo vimeanza kujipambanua na kuweka juhudi za kufanya vizuri wanaposhiriki michuano mikubwa kama Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
Moja ya eneo ambalo limebadilisha sana michuano hiyo na kufikia hatua baadhi ya vigogo kushindwa kupata matokeo mazuri kwa vilabu vya kati au chini kabisa. Mpaka sasa Shirilisho la Soka Afrika CAF limethibitisha ubora wa Ligi mbalimbali ndani ya bara ili, na hiyo imekuwa tofauti sana na namna timu zao za taifa zilipo kwenye nafasi ya FIFA kwani Ligi nyingine zimekuwa chini sana Licha ya timu zao za taifa ziko juu sana.
Changamoto kubwa ambayo imekuwa ikikumba baadhi ya nchini ni ratiba za Ligi zao kwenda tofauti na malengo japo siyo kwa nchi zote ila vilabu vingi vinavyofanikiwa kufika hatua za mbali za michuano hiyo imekuwa na changamoto kubwa sana ya kuwa na viporo vya michezo mbalimmbali ya Ligi zao.
Bila ubishi Morocco imekuwa ni moja ya Ligi bora Afrika nchini Misri ndiyo Ligi ambayo imekuwa na changamoto kubwa sana ya kuwa na viporo vingi na kupelekea Ligi hiyo kuchelewa kutamatika.
Jambo ilo limenifanya kukumbuka kipindi cha nyuma ambapo vilabu vyetu vilikuwa vikifika mbali na hususa kipindi kile Simba SC alipokuwa akishiriki CAF CHAMPIONS LEAGUE na kufika hatua ya Makundi, ilikuwa ndiyo klabu ambayo inaongoza kwa kuwa na michezo mingi mkononi ukilinganisha na vilabu vingine shiriki vya Ligi ya Tanzania.
Jambo ilo lilikuwa kero kubwa sana kwa wapenzi, mashabiki, wanachama na watu wengi wa kimpira nchini wakiaminia ndiyo nchi rahisi kwa timu kuwa bingwa. Lakini jambo ilo kwa sasa ni yofauti kwa sasa kwenye Ligi yetu ni msimu wa tatu sasa kadri muda unaenda ndivyo ambavyo changamoto ya ratiba inapungua kama siyo kuisha kabisa.
Pongezi kubwa sana ziwaendee Bodi ya Ligi kuu Tanzania TPLB chini ya kiongozi mkuu Almasi Kasongo mmejitahidi sana kuboresha ratiba ya Ligi hii kwa kuipanga kwenye njia ambayo inaepusha mrundikano wa mechi nyingi kwa timu moja na wakati mwingine kuondoa dhana ya kuwa na upangaji wa kimatokeo.
Almasi Kasongo na jopo lenu lote kongole kwenu kwa sasa siyo Simba SC wala Yanga SC wote kwa pamoja wanakuwa sawa kimichezo Licha ya ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa ila mmejitahidi sana hususa kwa msimu uliyopita kupunguza changamoto hiyo, hapo hapo mliposhikilia mpini ndipo hapo hapo inapaswa kukazia.
Kama kutashindwa kuwa na maboresho zaidi basi tubaki kwenye njia hiyo hiyo, naamini ipo siku tutakuwa daraja kwa wengine kujifunza kutoka kwetu kwa kushiriki moja kwa moja au kwa namna yoyote ile, kongole sana naamini itakuwa hivi hivi mpaka mwisho wa msimu ratiba kufuatwa kwa usahihi bila kumminya hata mmoja.
1 Comment
Hongera kubwa mno wanastahili kwakweli, waendelee kuboresha zaidi na zaidi naamini ipo siku tutakuwa mfano wa kuigwa kwa timu zingine za afrika