Baada ya kuwatoa Vital’O ya Burundi kwa jumla ya mabao 10:0 klabu ya Yanga itakutana na mabingwa wa msimu uliopita 2023/2024 wa Ligi kuu ya Ethiopia inayofahamika kama Ethiopian Premier League klabu ya CBE SA au Ethiopian Nigd Bank.
CBE SA ni klabu ambayo inapatikana katika jiji la Addis Ababa ambapo ilianzishwa mwaka 1982 na jina lake kamili ni Commercial Bank of Ethiopia Sports Association yaani ni klabu ambayo inamilikiwa na benki pale nchini Ethiopia.
Mwaka 2010 klabu hii ilibadilishwa jina ambapo ilikua inaitwa Banks Sport Club na kwenda kuitwa Commercial Bank of Ethiopia Sports Association ambapo msimu wa mwaka 2020/2021 ilikua ikicheza Ligi daraja la kwanza na baada ya kufanya vizuri ikapanda ligi kuu ya Ethiopia.
Katika upande wa mataji ni mabingwa wa ligi kuu ya Ethiopia msimu wa 2023/2024 na hii ndio mara yao ya kwanza kuchukua ubingwa huu ambapo ikawapa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu , mwaka 2014 walichukua ubingwa wa Addis Ababa City Cup.
Kwenye michuano ya kimataifa kwa ngazi ya CAF klabu hii haijafanya makubwa sana ya kushtua kwani waliwahi kushiriki upande wa kombe la shirikisho barani Africa yaani CAF CONFEDERATION CUP mara mbili n azote waliishia hatua ya awali ambapo nim waka 2005 pamoja na mwaka 2010 huku katika ligi ya mabingwa Afrika yaani CAF CHAMPIONS LEAGUE hii ni mara yao ya kwanza kushiriki na ndio wameingia raundi ya pili ambayo wanakutana na mabingwa wa ligi kuu ya NBC klabu ya Yanga.
Kwa upande wa jezi wanazotumia wakiwa nyumbani wanavaa jezi nyekundu ambayo inakua na mistari ya bluu pamoja na bukta nyeusi na soksi ya bluu huku wakiwa ugenini wanavaa jezi ya bluu Bahari yenye mistari ya njano shingoni pamoja na bukta ya njano na soksi nyeusi.
Kumbuka kuwa ligi kuu ya Ethiopia ambayo inafahamika kama Betking Ethiopian Premier League inashirikisha timu 16 pekee na klabu ambayo inaongoza kwa kuchukua mataji mengi zaidi ni Saint Georgr ambayo imechukua makombe 31.
SOMA PIA: Yanga Wana Matatizo, Hawajitambui. Je Ni Lini Watajielewa?
8 Comments
Sasa jezi za nn
Hakikisha unachoandika kiwe kinaukweli aboubeker nesir ameondoka mwaka juzi kujiunga na sundown sasa amekuwaje mwaka jana mfungaji bora
Hata bila historia yao,, wanakula nyingi hawa
Kwa kweli CBE wapige Dua na sala za mwisho kabla ya kuwakuta makuu
Hahahahaha kabsaaa maan.kwa takwim zao hizoo watapigwa kama ngoma
Yanga wanakuja kujiokotea tuuuu mwendo wa kuterezaaaaa
Hao madogo wajiandae meng magor hawana rekod nzuri🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Pingback: Hii Ndio Sheria Tata Zaidi Kwenye Mpira Wa Miguu