Ilipoishia ” Mkuu wake akakaa kimya kwa sekunde zisizodi thelathini kisha akalikubali ombi la Marcus, Sasa Kesi inaanza Upya ”
Tuendelee
SEHEMU YA 09
Ulikua Usiku mwingi, Adela akiwa Chumbani kwake alianza kumwona Babu yake Bilionea Yusuf akimnyooshea Kidole Mjukuu wake huyo huku akimwita kuwa ni Msaliti, Adela alianza kuogopa hakuamini alichokiona kuwa ni kitu halisi, Babu yake alishafariki.
“Hapana Babu, Hapana Babuuu” alijikuta akianza kutapatapa pale kitandani huku akitupa Miguu
yake iliyo ndani ya Soksi, punde taswira ya Babu yake ikatoweka kisha zikatokea taswira Mbili, moja ikiwa imefunika uso wote kwa kitambaa Cheusi, nyingine ikiwa haijafunika Uso, hii moja hakuijua lakini hii ya pili aliijua na ndiyo iliyomtia hofu zaidi.
Taswira anayoijua ikawa inamwambia
“Ukifungua kinywa chako nitakuuwa kama nilivyomuuwa Babu yako, kaa kimyaaaa” ilisema kwa Mamlaka, muda huo huo ile nyingine ikasema
“Nani Muuwaji Adela, Nani alimchoma kisu Babu yako?” Mtoto Adela hakuweza kuvumilia akajikuta akipiga yowe kali, muda huo huo mlango ukafunguliwa. Akamwona Mama yake na Mjomba yake Hamza wakiwa wameingia hapo wakifuatiwa na Bi Choro.
Haraka Sofia alimfuata Mtoto wake na kumweka kifuani, wote waligundua kua ilikua ni ndoto Mbaya aliyoiota Binti huyo. Namna alivyokua akivuja jasho na kuweweseka wakashauriana kumpeleka kwa Daktari Usiku huo huo, haraka Hamza akatayarisha gari, Adela alikua hawezi kusema Chochote kile, alikua na kwikwi.
Akafikishwa Hospitali Usiku huo huo, kutokana na Uwezo wao kifedha akawekwa daraja la kwanza
‘First Class’
“Ukifungua kinywa chako nitakuuwa kama nilivyomuuwa Babu yako, kaa kimyaaaa” Sauti ya Kutisha ya yule Mwanamke aliyemjua iliendelea kujirudia na kusababisha hali yake izidi kua mbaya hadi akahamishwa na kupelekwa Wodi ya Wagonjwa Mahututi.
“Sijui amekutwa na Nini?” aliuliza Sofia akiwa analia, Kaka yake Hamza akamtaka kutulia.
***
Ilikua ni Saa 1:30 Asubuhi ya siku iliyofuata, Mpelelezi Marcus alitembelea nyumbani alipokua
anaishi Marehemu Michael Jomo, yule Mchoraji ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDSM.
Alianza upya kupeleleza kesi hiyo baada ya kupata Baraka zote kutoka kwa Mkuu wake wa kazi
Alipofika alikuta nyumba hiyo ikiwa imepigwa kufuli, mazingira yake yalionesha hapakua na Mkaaji eneo hilo. Akakutana na jirani Mmoja Kibibi kizee kilichokua kinaota jua nyumba jirani
“Samahani Bibi, hivi wenyeji kwenye nyumba ile wapo kweli?” alionesha nyumba aliyoikusudia, yule Bibi asiye na meno akamjibu
“Baada ya Msiba yule Mama aliondoka na kurudi Kijijini, hata hivyo nyumba imeshauzwa”
“Oooh! Basi asante Bibi” alisema Marcus kisha akaondoka hapo, alipofika mahali ambapo aliona yule Bibi hawezi kumwona, aliparamia ukuta kisha akachumpa hadi ndani ya uzio wa Ukuta, halafu akauelekea mlango wa kuingilia ndani kabisa ambao ulikua umefungwa. Akatafuta namna ya kuingia humo, akafanikiwa kupitia dirisha la choo.
Namna palivyo ni wazi hapakua panaishi Binadamu kwa siku kadhaa, akaufuauta ule Mlango
ulioandikwa J ambao ndiyo Michael alikua akiishi ndani yake. Akaingia humo taratibu huku
akiusukuma Mlango uliokua ukipiga kelele.
Alipofika alikutana na michoro mingi ndani ya chumba hicho, hiyo pekee ikasadiki maneno ya Mkuu wa chuo kuwa alikua mchoraji mzuri, alichora picha za viongozi, wasanii na picha za marafiki zake.
Picha moja ikamvutia kuitazama zaidi, ilikua ni picha ya kuchora ya rangi ikimwonesha yeye Michael na rafiki yake mmoja wa kike, rafiki huyo ndani ya Mchoro hakua na kichwa.
Akajaribu kuzitazama picha zingine aliona hivyo hivyo, yaani kichwa cha rafiki huyo hakikuwepo kwenye mchoro, alikua Mtu wa kuvalia mavazi yenye kuachia maungo yake kwenye picha kadhaa, akiwa anakagua akapata kuiyona picha moja iliyopigwa kwa Kamera, picha hiyo ilikua na Watu watatu tu.
Mmoja alimtambua kua ni Michael mwenyewe, mwingine hakumtambua, huyu mwingine wa kike sura yake ilifutwa kwa makusudi, hapa akaweka walakini inawezekanaje Mtu huyo afute kichwa chake kwenye picha, zile za kuchorwa kichwa chake hakikuwepo kabisa? Akazichukua picha kadhaa ambazo Mwanamke huyo alikuwepo.
Akaondoka nazo hadi kwa Mkuu wa chuo Kikuu cha UDSM
Akampatia ile picha ya rangi, Mkuu akaiangalia kisha akamuuliza Marcus
“Leo unataka msaada gani Mpelelezi?”
“Nataka kuwajua marafiki wa Marehemu Michael Jomo”
“Sawa” Muda huo huo Mkuu akapiga simu, akazungumza kisha akamwambia Marcus
“Wanakuja”
***
Miaka kadhaa iliyopita, Shambani Dodoma.
Ni jioni moja, Bwana mmoja akiwa amesimama mbele ya shamba moja la Zabibu alijikuta
akitabasamu, purukushani za Wafanyakazi wa shamba hilo zilikua zikiendelea. Magari yalikua
yakisomba Zabibu kutoka katika Shamba hilo Kubwa lenye Ukubwa wa Hekari 700, Bwana huyo alikua akiitwa George Bona.
Akiwa katika hali ya kushangaa akaguswa begani na Bilionea Yusuf aliyevalia kofia aina ya Beleti.
“Hakika leo nimeona jambo kubwa lenye kustaajabisha. Katika Maisha yangu sikuwahi kuona
shamba kubwa kiasi hiki, nimelizunguka kwa Masaa na sijamaliza hadi nimechoka” alisema Bwana George
“Ha!ha!ha!” akacheka Bilionea Yusuf, ilikua ni mwezi mmoja baada ya wawili hawa kufahamiana Hospitalini, huyu George ndiye Baba yake Martha. Pale pale akaja Mwanamke mmoja mzuri mwenye asili ya kipemba akamsemesha Bwana George
“Mimi naelekea Dar, nimepigiwa simu kuwa Martha hataki kula wala kufanya chochote zaidi ya kulia. Tokea Alfajiri hadi sasa analia tu”
“OOOH JAMANI ITAKUWAJE NA NDIYO TUMEFIKA HUKU?” akasema Bwana George, Bilionea Yusuf alikubaliana na Bwana George kuwa atampa usimamizi wa shamba hilo la zabibu na ndiyo sababu ya wao kutoka Dar hadi Dodoma.
Walikubaliana Martha akakae kwa Bilionea Yusuf sababu Hamza alikua akimpenda sana Binti huyo.
Hadi hapo ilipofikia Bwana George akawa anaogopa kufanya maamuzi, Bilionea Yusuf akagundua.
“Usijali tutarudi pamoja”
“OOOH!! Kushukuru sana Baba, maana hapa nilikua najiuliza itakuaje”
“usiwe na hofu George, wewe utabakia huku wakati Mkeo anaandaa mazingira ya kurudi tena
Dodoma.
Mke wa George na Bilionea Yusuf walianza Safari ya kurudi Dar kwa kutumia gari Binafsi aina ya Nissan Safari. Waliketi siti ya nyuma wakizungumza wakati dereva akiichapa fimbo Nissan hiyo.
Wakiwa Barabarani wanakaribia Gairo yule dereva alianza kujisikia vibaya ikabidi apaki gari pembeni. Akaelekea kando ya Barabara na kuanza kutapika, alitumia zaidi ya dakika thelathini akiugulia kisha akarudi kwenye gari na kumwambia Bilionea Yusuf kua hatoweza kuendelea na Safari, anapaswa kutafuta dawa ya kumsaidia kuzuia kutapika.
Akasimamisha pikipiki na kutafuta duka la dawa, kilomita kadhaa akafanikiwa kupata kisha akarudi kwenye gari, lakini alipoangalia vizuri mazingira aliyoyaacha siyo aliyoyakuta. Bilionea Yusuf alikua upande wa kulia na Mke wa George kushoto wakati aliwaacha wakiwa tofauti ya hivyo.
“Umerudi Eeh, tumekusubiria sana” alisema, mara moja dereva aliwasha gari na safari iliendelea.
Akilini mwa yule dereva alihisi Bilionea Yusuf na Mke wa Bwana George wametenda dhambi ya
ngono ndani ya gari lakini alichagua kukaa kimya.
Tukirudi UDSM Sasa
Marafiki wa Michael Jomo wamefikishwa mbele ya Jasusi wa kuaminika Marcus, walikua watatu tu na kweli walikua wanachuo wa UDSM wakichukua masomo tofauti tofauti tena kwa miaka tofauti kabisa. Wote walikiri mbele ya Jasusi Marcus kuwa ni kweli wao ni marafiki wakubwa, wote walijuana kupitia kwa Michael Jomo.
“Mnaweza mkamtambua huyu Mwanamke kwenye hizi picha?” Marcus akawapa picha alizozichukua nyumbani alikokua anaishi Michael Jomo, walitumia dakika kadhaa kutazama mwisho wakajikuta wakitazamana
“Nawauliza tena Mnamfahamu huyo?” alihoji tena Marcus huku akigonga meza kwa kitisho, wote kwa pamoja walikana kutomjua Mwanamke huyo.
“Ni ajabu eti hamumjui huyo na Mlipiga naye picha?” Marcus akapiga simu polisi, gari ikaja na
kuwasomba vijana hao wa kiume watatu, wakapelekwa hadi Mahabusu, lango likafunguliwa
wakatupwa humo kama mizigo.
Walijikuta wale vijana ndani ya chumba kimoja chenye giza, harufu za vinyesi na mikojo, mmoja wao akawa anatapika sana kisha nguvu zikamwisha akawaambia wenzake
“Mimi naenda kusema Ukweli” alisema akiwa ameshikilia nondo za mlango wa Mahabusu, mmoja akamfuata kwa jazba na kumwambia
“Utakuja kufa kama wengine, ni bora tuteseke lakini tusiseme chochote. Naamini muda ukifika
watatuacha huru, ukifungua mdomo utatuponza sote” alisema akiwa amemkwida shati.
Saa 11:00 jioni, Marcus aliagiza vijana hao wapelekwe chumba cha mateso ili wamtaje yule Msichana aliyekua akijificha kwenye zile picha, hisia za Marcus zilimwambia kuwa Msichana huyo kwa hakika ndiye Muuwaji halisi, alipata hisia hizo kutokana na tabia yake ya kupenda kuficha uhalisia wake kwenye zile picha.
Ikampa taswira kua alikuja akificha jambo Vijana wale watatu wakavuliwa nguo zao kisha wakaingizwa ndani ya chumba kimoja chenye wadudu aina ya siafu wakali waliokua wakifugwa humo, walipiga kelele za kuomba lango lifunguliwe kwani sauti za siafu zilisikika.
Waling’atwa na siafu hao kila kona ya miili yao huku polisi wakiwatazama kupitia lango kuu la
chumba hicho chenye Siafu wakali.
“Aaaaaaaahhhh!!! Nasema ukweli namjuaaaaaaa” alisema yule Mwoga ambaye alikua ametapika
sana kule Mahabusu, Marcus akaagiza vijana watolewe.
Dakika saba pekee zilitosha kwa Marcus kupata mahali pa kuanza Uchunguzi wake, walitolewa vijana hao wakiwa wamevimba sehemu mbalimbali za Miili yao.
JE, Muuwaji anaenda kujulikana? Usikose Sehemu Ya 10
Jiunge WhatsApp Channel Ya KIJIWENI Ili Kuwa Wa Kwanza Kupata Updates Za RIWAYA Hii Kwa Kubonyeza Hapa
SOMA Uchambuzi Na Makala Mbalimbali Kwa Kubonyeza Hapa
19 Comments
Awww mabo yamefika opatamu
Martha jamani Martha
😂😂✌️👊🏻
daaah hii noma
Jamani mmiliki wa hii story naomba hii series niitafutie script mim😢
Huyo Martha kabisaaaa😅😅
Mbona ndogo
Uyo muuaj anasumbua San wapelelz🙌
Shusha nyingineeee
Nzuri sana tupia kitu
Apa anaitajika pia daudi washirikiane kumtafuta huyu kuuaji au ni Sofia😄😄😄
Jamani koti jeusi iruke mara tatu kwa siku ombi kwa admin 🤔🤔😅😅
Kabisa yan
Je ni Martha au Sofia? Ahahahaha hatari
Uyo Martha😅
Kusema ukweli hata ukitoa kumi kwa siku hazitoshi ndugu admin daaah😁
Sema admin nicheck nina jambo muhim tuongee 0626 152 175 ni muhimu kweli kama hutojali
Marthaa 😂😂
Shida nn admin? Kama ni bando si tutachangia utupe vitu?
Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tano) KOTI JEUSI – 15 - Kijiweni