Yule Msichana wala hakua na hofu, alirudi nyuma ili kumpa nafasi Marcus atoke kwenye kile choo, Bastola ilidondokea kwenye choo kingine kwa chini hivyo hakuna hata Mmoja kati yao ambaye angeweza kuiokota.
Marcus akaikumbuka Bastola yake akahitaji kujipapasa, alishangaa Bastola kuiyona kwa yule Msichana mzuri mwenye asili ya Kilimanjaro kwa namna meno yake yalivyobadilika rangi, hata lafudhi yake ilifanana sana na Watu wa huko lakini yule Msichana hakutaka kuitumia Bastola, akazitoa risasi zote kisha akaitupa chini.
“Umeniona, umenijua. Nataka nikupeleke kuzimu” alisema, kisha akajiweka sawa kupambana na Mpelelezi Marcus ambaye alikua ameiva kwa mapigano kisha akasema
“Karibu Malcom” alilitaja jina ambalo Alilibadilisha ili kuficha uhusika wake, alishangaa kuona bado Kuna Mtu aliyeweza kumtambua.
“Umelijuaje hilo jina la Malcom?”
“Najua vingi kuhusu wewe lakini muda hautoshi Malcom sababu kifo chako kimeshafika” alisema Msichana huyo kisha alitupa ngumi moja iliyokwepwa na Marcus, akapanga tena shambulizi huku Marcus akimsoma Msichana huyo.
Msichana huyo akatupa tena ngumi iliyoambata na teke kali la Mguu wa kulia, Marcus akakumbana na teke hadi akajibamiza kwenye mlango wa choo kisha akamwona Msichana akidanki danki kama Mtu aliye ulingoni.
Alipojiokotanisha alikutana na teke la bega ambalo Marcus alilidaka lakini kwa ufundi Msichana huyo alijivuta na kutua shingoni kwa Marcus kisha akaanza kumpa makonde ya shingo Marcus akalazimika kumwachilia lakini makonde hayo yalimwingia na kumsababishia Maumivu,
Marcus hakupewa nafasi ya kujiandaa na kurusha pigo, alikutana na mvua ya mateke ya tumbo
yaliyopigwa kwa kasi sana. Kila pigo lilikua na aina yake ya upigaji ambayo ilimchanganya Marcus, kwa dakika hizo Marcus hakufanikiwa kutupa pigo lolote kwa Msichana huyo.
Damu ilikua ikimtoka puani na mdomoni, kila alivyojaribu kumsoma alishindwa kwani alikua akitumia aina tofauti tofauti za mapigano yaliyomchanganya Marcus, akiwa anatafakari akakutana na teke la kichwa lililompeleka hadi chini, akawa anaona nyota nyota tu. Yule Msichana akasogea alipolala Marcus akamwambia
“Nawe unastahili kufa kama wao” Msichana huyo alikua na Bisi Bisi ambayo kwa hakika ndiyo
anayoitumia kutobolea Macho Watu anaowauwa. Marcus akaona kama atazidi kuzubaa anaweza
akauawa hapo, alichofanya ni kumpiga changa la macho kwa kujifanya kazidiwa sana na mapigo
yake.
Kisha haraka akamvaa Msichana huyo na kuanza kumpokonya kwa nguvu Bisi bisi hiyo, katika
purukushani akafanikiwa kumchoma nayo eneo la tumbo kwa chini yule Msichana.
“Oooooh Shit” alisema Msichana huyo kisha akaonekana kutaka kukimbia hapo lakini Marcus
alimzuia kisha akambana ukutani kwa nguvu na kuanza kumchapa makonde ya shingo hadi
alipohakikisha amemlegeza.
Akanyanyua simu na kuwapigia polisi wafike hapo haraka, yule Msichana akacheka tu huku akitema damu akamwambia Marcus
“Wewe ni Mtu pekee mwenye Bahati Malcom, unapenda sana kuonekana shujaa si ndiyo. Umekua hivyo mara zote lakini hutonishinda” alisema akiwa ameishiwa nguvu, maumivu ya Bisibisi iliyozama tumboni yalizidi kuongezeka huku Damu ikimtoka.
“Sitokuacha ufe kama ulivyofanya kwa Watu uliowaua, nitakuacha ukiwa hai ili Dunia ijue kwanini unauwa” alisema Marcus, muda huo huo polisi walifika hapo na kumkamata Msichana huyo.
Malcom naye akachukuliwa ili kupatiwa msaada wa matibabu
IG mpenda sifa Saimon Kuga akaita waandishi wa habari na kwa Mbwembwe kabisa akasema Polisi wamefanikiwa kumnasa Muuwaji, taarifa hii hata Mpelelezi Daudi Mbaga aliiyona kwenye Tv na kusikia Tambo za IGP Saimon Kuga.
Akapata sifa kubwa huku uhamisho wa Daudi Mbaga ukitajwa kua ndiyo uliosababisha kesi kwenda haraka na Muuwaji kunaswa.
Baada ya wiki kadhaa alianza kuhojiwa akiwa amepona kabisa, kitengo cha Polisi kilimfikisha
Mtuhumiwa huyo kwenye idara ya Mahojiano, Marcus alikua ni miongoni mwa waliokua nje
wakisikiliza mahojiano hayo.
Jina la Muuwaji huyo alijitambulisha kama Sakina Kahaya, umri wake ni Miaka 28, umri ambao Daudi Mbaga aliamini kua Muuwaji alikua chini ya Miaka 30. Alikubali Makosa yote kuanzia kifo cha Mzee Yusuf na wengine wote aliwaua yeye, akaulizwa ni kwanini alikua akiwauwa, hapo kila mmoja alisubiria kusikia sababu atakayoitoa Sakina.
“Mzee Yusuf aliitenda unyama familia yangu kwa kupora ardhi ambayo ilikua na umuhimu sana
kwetu, dhulma ile ilisababisha Baba yangu kufariki kwa presha. Niliapa kuwa nitamuuwa siku moja, tena nitauwa wote wanaomzunguka ili kulipa kisasi”
Jibu hili halikuingia kichwani kwa mpelelezi Marcus kwani aliona maelezo yaliyotolewa hayakushiba kabisa
Sakina alipoulizwa kuhusu Michael Jomo alikiri kumuuwa sababu alikua rafiki yake aliyekua
akimweleza kila kitu anachokifanya, akasema baada ya kumuuwa Mzee Yusuf alimpiga picha na
kumtumia Michael Jomo ili aione sanaa yake ya mauwaji.
Akazidi kueleza kua alimuuwa sababu Michael aliamua kuichora picha hiyo ambayo ingekuja kumfanya agundulike ndipo akamuuwa Michael Jomo.
Kwa Maelezo haya, Sakika akatajwa moja kwa moja kuwa ndiye Muuwaji, akafikishwa Mahakama ya Kisutu na kuhukumiwa kifungo cha Miaka 45 jela. Vyombo vyote vya habari vikahitimisha maandiko yao kua Muuwaji amepatikana .
xxx
Familia ya Mzee Yusuf ikiongozwa na Kaka Mkubwa Hamza ilitoa shukurani za dhati kwa jeshi la polisi kwa kumnasa Muuaji, furaha na amani vilirejea kwenye Maisha yao, hata Adela sasa alionekana kukaa sawa baada ya taarifa hiyo.
Familia ilimwita Mpelelezi Marcus na kumpongeza kwa kumnasa Muuwaji, Sofia akatoa zawadi ya gari aina ya Range Rover mpya kabisa, Marcus alipotaka kukataa zawadi walimlazimisha kuichukua kwani wameitoa kama Shukurani kwake, wakiamini hata Baba yao anafuraha huko aliko.
Baada ya wiki moja kupita, kila kitu kilionekana kwenda sawa, kesi ilionekana kufika mwisho kirahisi sana tofauti na ilivyotegemewa. Sakina alipelekwa Segerea kutumikia adhabu yake ya Mauwaji yaliyoitikisa Tanzania,
Usiku mmoja Jasusi Marcus akiwa amelala, mishale ya saa 9 Usiku alishtushwa na mlio wa simu yake ndogo aliyopendelea zaidi kuitumia. Alipoamka kitu cha kwanza kilikua ni kuangalia saa yake, haikumshtua sana kupata simu mishale hiyo kutokana na Majukumu yake.
Akaivuta na kubofya kitufe cha kupokelea, kisha akaiweka sikioni huku akijipangusa uso wake wenye mafuta mengi
“Hallo” alisema, hakumfahamu Mpigaji sababu namba iliyopigwa haikua miongoni mwa alizozihifadhi kwenye simu yake.
“Hello Marcus, habari yako na pole kwa kukushtua Usiku huu mwingi” ilisikika sauti iliyopoa sana, sauti iliyoashiria ilikua na jambo zito la kusema. Haraka Marcus aligundua sauti hiyo ilikua ya Mtu makini sana, ilikua sauti ya kiume nzito iliyorarua Masikio ya Marcus
“Sijui naongea na Nani wakati huu?”
“Naitwa Mpelelezi Daudi Mbaga” alijitambulisha mpigaji, haraka Marcus akamtambua sababu faili la kesi ya Mzee Yusuf iliandikwa jina la Mpelelezi huyo.
“Nakupata”
“Marcus hivi ni rahisi kumnasa Muuwaji niliyehangaika naye kwa miezi?” ilisikika sauti ya Daudi Mbaga ikihoji
“Unataka kusema Nini?”
“Huyo uliyemnasa hawezi kuwa Muuwaji halisi, nenda mbali zaidi Marcus, Muuwaji amekulamba kisogo”
“Lakini yule Binti ni Mtu pekee niliyemkuta akiwa amefanya Mauwaji, pili ni Mtu pekee aliyekiri na kuijua stori yote hata yale ambayo Wapelelezi waliyaficha. Anaonesha wazi kua ni yeye”
“Hapana, akili yangu inaniambia kuwa Muuwaji yupo pembeni anautazama huu Mchezo Marcus tena ni Mtu anayejificha sana akikwepa mkono wa Serikali. Nahisi bado hajamaliza, atauwa wengine” alisema Daudi Mbaga.
Maneno haya yalimfikirisha sana Marcus kisha akamsikia tena Daudi akisema
“Lisome vizuri faili la kesi, Muuwaji ni Mtu aliye karibu na hiyo familia ya Bilionea Yusuf, ni kati ya hao Watoto wa Mzee. Kuna picha nimeambatanisha, kwenye hiyo picha ndipo alipo Muuwaji” alisema Daudi
Haraka Marcus akasimama na kulifuata faili juu ya meza, aliiona picha hiyo
“Hebu ngoja nipitie vizuri nitarudi Kwako” alisema Marcus kisha aliiweka simu juu ya meza, Usingizi ilishamwisha. Akaanza kulisoma faili upya kama Daudi Mbaga alivyotaka.
Macho ya Kijasusi yakawa yanapitia kurasa moja hadi nyingine, kila alichoona kilikua na umuhimu alikiandika pembeni, hadi anafika saa 12 Asubuhi alikua ameandika zaidi ya Mambo ishirini kutoka katika lile faili.
Kwanza alihitaji kuthibitisha kuwa Sakina alikua Mwanachuo pale UDSM ili ajuwe mahali anapoweza kuanza napo.Safari ya kwanza asubuhi hiyo baada ya kujiandaa alielekea Chuo Kikuu cha UDSM, Moja kwa moja hadi kwa Mkuu wa Chuo
“Karibu” alikaribishwa ofisini na Mkuu wa Chuo, akajitambulisha kuwa ni Mpelelezi wa Mauwaji yaliyotokea hapo Chuo kisha akaanza kumuuliza Mkuu huyo.
“Nataka kujua kama Sakina Kahaya ni Mwanachuo wa hapa” Yule Mkuu wa Chuo akafunga mikono yake kisha akamtazama Mpelelezi Marcus akamjibu
“Sijui hata ilikuaje akaonekana ni Mwanachuo wa Chuo hiki, hakuna mahala ambapo panaonesha kuwa yule alikua akisoma hapa. Sakina Kahaya si Mtu wa hapa kabisa” alisema Mkuu wa chuo
“Kwanini hamkulisema hili alipokua Mahakamani?”
“Ndiyo maana nasema sijui nini kilitokea hadi akaonekana wa hapa, hatuna rekodi ya Mwanachuo Muuwaji katika Chuo hiki, tukio lile limekitia doa chuo” akasema tena kwa msisitizo, hapa akili ya Marcus ikaanza kumwelewa Daudi Mbaga, sasa kama si Mwanachuo kwanini alitoa maelezo kua alikua akisoma hapo?
“Kwa vyovyote yule itakua ni Kopi ya Muuwaji” alijisemea moyoni Marcus.
“Asante”
“Karibu tena” Marcus aliagana na Mkuu wa Chuo, mara moja akaelekea kwenye gari, akiwa hapo akampigia simu Mpelelezi Daudi Mbaga
“Nasadiki maneno yako Daudi, nimetoka chuo kuonana na Mkuu wa Chuo. Sakina si Mwanachuo wakati kwemye maelezo alithibitisha kuwa ni Mwanachuo, nafikiri nahitaji kwenda Segerea Magereza” alisema Marcus
“Nilikwambia Marcus, kuna jambo la siri sana kuhusu Muuwaji.
Wapo wawili tofauti na hapana shaka hawajuani kama uliisoma ripoti yangu”
“Nimeyajua yote hayo, wacha nifike Magereza nikaonane na Sakina” akasema Marcus kisha
akawasha gari na kuanza safari ya kufika Gereza la segerea.
Safari yake ilimchukua Masaa mawili kufika Gereza la Segerea, akaomba kuonana na mfungwa
namba T33-09. Akasubiria eneo la kuzungumza na Mfungwa, ilikua rahisi kwake kukubaliwa haraka sababu ndiye mpelelezi aliyeishikilia kesi hiyo.
Dakika tano baadaye, Sakina aliletwa mbele ya macho ya Mpelelezi Marcus, walipo gongana macho tu haraka Marcus aligundua kuwa Sakina alikua na hofu sana kama si yeye ambaye alikua akijitapa kwa kusababisha Mauwaji ya kikatili ya miezi kadhaa iliyopita. Hakuonekana kama shujaa kwa wiki chache alizokua hapo.
Sakina akatabasamu akiwa anamtazama Marcus, aliiondoa ile hali ya woga kisha akasogea mbele zaidi na kuketi kitini akiwa amefungwa pingu mikononi
“Mfungue tu” alisema Marcus akiwa anamtazama Mlinzi aliyekua nyuma ya Sakina, pale magereza
Sakina alitazamwa kama Mtu hatari zaidi kutokana na kesi iliyompeleka hapo.
“Unaweza ukatuacha kwa dakika tano tu” akasema tena Marcus, yule Mlinzi akatii amri hiyo,
akaondoka eneo hilo akawaacha Marcus na Sakina wakianza mazungumzo.
Marcus kutokana na ile simu ya Daudi Mbaga aliweka zaidi umakini kugundua dalili moja baada ya nyingine kuwa Sakina siyo Muuwaji anayekusudiwa, njia pekee ilikua katika Mazungumzo. Marcus akamwuliza Sakina swali la mtego sana
“Wewe ni Muuwaji wa kwanza au wa pili?” swali hili lilionekana kumshangaza Sakina, hapo haraka Marcus akapata ishara ya kwanza kuwa Sakina alipandikizwa na Muuwaji ili aendelee kujificha Mafichoni atekeleze Mauwaji bila vikwazo vyovyote vile.
“Nini kimekuleta hapa Malcom, nafikiri kesi ilishaisha. Natumikia adhabu yangu” alisema Sakina, sura yake na maneno havikulingana kabisa, alisema tu kutoka mdomoni na si Moyoni kwa maana maneno yake yalijaa hofu ndani yake
“Unafikiri ukimlinda Muuwaji sitompata, Sakina najua wewe si Muuwaji. Sijui ni nini kimekuingiza huku lakini naamini Muuwaji atakuuwa hapa Magereza, amua kushirikiana na Mimi ili nimnase Muuwaji halisi” akasema Marcus,
Sakina akacheka kwa kicheko cha dhihaka
“Malcom, nimethibitisha Mbele ya Mahakama kwa hakika kuwa nimetenda yote. Ule ndiyo ukweli na hakuna ukweli mwingine. Hakuna Muuwaji zaidi yangu” alisema Sakina kisha akasema kwa nguvu
“Askari njoo unitoe hapa” mara moja yule askari magereza alifika na kumwambia Marcus
“Wakati mwingine” aliondoka na Sakina.
Marcus hakufanikiwa kwa hakika kuthibitisha juu ya wasiwasi wake, aliamua kuondoka Segerea kisha akaelekea kwa Mkuu wake wa kazi na kumweleza kuwa anahitaji kuifufua tena ile kesi ya Mauwaji, Mkuu wake akamwambia
“Tayari ameshahukumiwa, kila kitu kimeisha. Kwanini unataka kufufua yaliyozikwa na Mahakama tena wiki chache tu?”
“Nimegundua kuwa yule si Muuwaji halisi, amepandikizwa na Muuwaji”
“Marcus, ni wewe ndiye uliyesimama Mahakamani na kueleza kua yule Binti ndiye Muuwaji, leo unataka kupangua maneno yako mwenyewe?”
“Mkuu naomba ruksa niichunguze tena hii kesi, Sakina ana mengi ya kunieleza…..Nataka
kumdhihirisha Muuwaji wa kweli” alisema Marcus.
Mkuu wake akakaa kimya kwa sekunde zisizodi thelathini kisha akalikubali ombi la Marcus, Sasa Kesi inaanza Upya. Nini kitaendelea, je Marcus atafanikiwa kumnasa Muuwaji? USIKOSE SEHEMU YA 09
Jiunge WhatsApp Channel Ya KIJIWENI Ili Kuwa Wa Kwanza Kupata Updates Za RIWAYA Hii Kwa Kubonyeza Hapa
SOMA Uchambuzi Na Makala Mbalimbali Kwa Kubonyeza Hapa
19 Comments
Dah mpaka tumpate mwenye koti Jeusi Shughuli ipo🙄🙄
Riwaya tamu sana hii unga tu imalizike unakata patamu sasa aisee
Bonge la Movie 🍿
Daaaaah🥲 uchoyo tu kwan ungeweka na sehemu inayofuata ungekosa nn sasa😂
🤣🤣
Ilete no.9 fasta mpaka tumdake mwenye koti jeusi ha ha haaa nipo na wewe mpaka kieleweke
Fupi jaman jion ongeza nyngine ya kulalia tutapoa sana jaman please
Mwandishi tuma laini pesa tukuwekee ya maji bonge moja la hadith big up brooo
🤝
Daudi Mbaga ni mwamba
chumaa aisee huyo Martha atakiona cha moto
Ni hatar sana tupe sehemu inayofata bas
Hii ingekuwa asubuhi na JIONI wakuu
Sema hii story inabidi kama vipi muitolee ata Movie🤣
🤝
🤝
Picha limeanza
🤝🏿
Ata module hazna faid kwa hii stry , kiukwel nafirce time ya kusom stry cjawah som module zang,😉😉😉