Mchezo wa 25 kwa kila timu ukiwa ni mchezo wa ambao ni muhimu kwa timu zote mmoja akihitaji kushinda kujihakikishia ubingwa wa Ligi kuu ya NBC huku mmoja akitaka kujiweka kwenye nafasi nzuri Ya kuepuka kushuka au kucheza mtoano.
Timu hizi zimekutana mara moja kwenye mchezo wa Ligi kuu Ya NBC na klabu Ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa goli 2-1, na mchezo huu utakuwa mchezo wao wa pili wanakutana kwenye Ligi kuu ya NBC.
Takwimu zao kwenye michezo mitano Ya mwisho kwenye michuano yote waliyoshiriki klabu Ya Yanga SC imeibuka na ushindi kwenye michezo 4 na kutoa sare mchezo mmoja, kwa upande wa Mashujaa FC wao kwenye michezo 5 wamefanikiwa kufungwa michezo 2 na wakitoka sare michezo 3.
Upande wa magoli kikosi cha Yanga SC wamefanikiwa kufunga magoli 9 kwenye mechi 5 huku wakiwa wameruhusu goli moja tu, huku Mashujaa FC wakiwa wamefunga goli moja na wakiruhusu magoli 4.
Namna takwimu zinavyoonyesha ni dhahiri kuwa Yanga SC ana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kuliko kikosi cha Mashujaa FC huku pia wakiwa na wastani mzuri wa kutoruhusu magoli machache na hapo utofauti Upo kwa upande wa kuruhusu ambapo Mashujaa ameruhusu mengi kuliko Yanga SC.
Ubora na Uhodari wa Yanga SC Upo kwenye eneo la Kiungo wakiwa na uwezo mzuri wa kuzuia na kushambulia pia tofauti na Mashujaa FC ambao changamoto ipo kwenye kuzuia na kutumi nafasi wanazopata kwa uzuri kabisa. Yanga SC wana ubora idara nyingi kiwanjani kuanzia uzuiaji wao kwenye eneo la beki kuja kiungo mkabaji, eneo hatari zaidi ni ushambuliaji kwao wana wachezaji ambao wana uwezo wa kuamua namna Ya kucheza kwa kasi au taratibu jambo ambalo linawapa nafasi kubwa ya kushinda michezo mingi.
Changamoto ni pale wanapokutana na timu ambayo inaamua kukabia chini vizuri na kutumia mianya wanayoacha sehemu ambayo ni tatizo kwa vilabu vingi kushindwa kuziba mianya wanaposhambulia na kupoteza mpira na hiyo ipo kwenye upande wa timu zote mbili.
Mashujaa FC jambo kubwa ni kukubali kuwa chini ya Yanga SC na kushambulia kwa kushtukiza kwanini ? Uwezo wa Yanga SC kushambulia umakini na matumizi sahihi ya nafasi wanazotengeneza na zaidi na kuwa namba kubwa ya Wachezaji wenye uwezo wa kufunga magoli. Mchezo wao wa kwanza Mashujaa FC walifanikiwa kuwazuia kwa kukabia chini na kujaribu kuziba mianya kwa kiasi kikubwa japo hawakufanikiwa kwa asilimia zote.
SOMA ZAIDI: Viongozi Simba Wanajiroga Wenyewe Na Kujitega Mtego Mbaya
1 Comment
Ni mchezo mzuri itaamuliwa na mifumo ya makocha nategemea mchezo wenye magoli machache utaamuliwa na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja