Nikiwa kama mdau wa michezo hasa Mpira wa Miguu, nashauri Serikali kufanya haya ili kuboresha kiwango cha mpira nchini, na hata ushiriki wetu kwenye mashindano yajayo ya AFCON,2027 yatakayo fanyika nchini kwa kushirikiana na wenzetu wa Kenya na Uganda.
- Tutafute Kocha wa daraja la juu wa soka ambaye analifahamu soka la Africa na dunia kwa ujumla. Yule ambaye rekodi yake haina shaka yoyote.Nampendekeza kocha wa zamani wa Zambia na Ivory Coast ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Ufaransa , Herve Renard ,tukishindwa huyo twende na kocha wa zamani wa Aly Ahly ya Egypt/Mamelody Pitso Mosimane au Mkongo Florent Ibenge, bila kusahau suala la timu kukaa kambini muda mrefu,miezi 6 itapendeza zaidi.
- Kwa maendeleo ya muda mrefu tuchukue makocha hata 10 vijana na wale wa makamo wapelekwe nchi za Ulaya hasa Ujerumani, kwa mafunzo ya soka {Burundi walishafanya hili)..napendekeza makocha wafuatao wapate hiyo fursa, Zuberi Katwila, Selemani Matola, Minziro, Mecky Mexime, Mbwana Makata, Edward Augustino, Pawasa, huyo kocha wa sasa Prison yaani Ahmad Ally, Julio, na wengine kadiri Serikali itakavyoona inafaa ila kwa kuanzia tunaweza tupeleke Makocha 10, na wakirudi wapewe timu za taifa na hata vilabu kwa malengo maalumu. Kuhusu gharama tunaweza OMBA ufadhili kwa wenzetu wa Ujerumani kama ambavyo nchi nyingi zimekua zikifanya
3.Tuboreshe chuo cha Michezo cha Malya Mwanza,na hawa watakaopelekwa Ujerumani wanaweza kuwa Wakufunzi hata wa muda kule chuo cha Michezo Malya,
SOMA ZAIDI: Ni Wakati Wa Simba Kumuamini Kocha Mzawa?
5 Comments
1. Tumuajiri nasredene nabi atutengenezee project ya taifa
2. Apo kwenye accademi pamuhimu zaidi mana sisi tunafungwa siyo tu kwa sababu hatuna vipaji ila tunashindwa kujua ni muda upi tucheze mpira, muda gani tumuachie mpinzani n’a muda gani tupoteze muda mana hapo ndo warabu wanapotuzidi
3. Mwisho tumpe uraia isak wa new castle mana dogo asili yake ni Masai atatuongezea kitu na uzoefu wake ๐๐ ni mawazo tu ๐ญ๐ญ
Ni ushauri mzuri mzuri mnoooo.
Ila AFCON ni 2027 kuhusu makocha kwasasa tunahitaji kocha ambaye 1. Mzuri katika kutengeneza saikolojia ya wachezaji, 2. Mzuri katika kuweka kutumia ule uwezo wa wachezaji wetu kwa wakati uliopo. (((Kwann nasem hii, Simba ilimfukuza Robertihno ikamleta Adelhak kocha mwenye class kubwa, ila Benchikha ni kocha anayehitaji wachezaji walio teyari, sio wachezaji wakuja kupewa mda/wachezaji wa kuunga unga)))
1…. tumtafute kocha mapema aanze kuangalia wachezaji watakaofaa kwenye project yake
2… tuhakikishe kila barabara uwanja na hoter zinakuwa na matangazo ya vivutio vyetu vya watalii
Nb: tumpee eng Hers nafasi ya kuunda mpangonmkakati mtakuja kunishukuru
#nguvumoja
Shida Siyo Hayo Yote Bali Je Mikakati Na Mipango Katika Kufanya Tanzania Iwe Hapo Ipo? Na viongozi Je?
Pingback: Fredy Ni Mchezaji Mzuri Akitumiwa Vizuri Ataisaidia SIMBA - Kijiweni