Kama kawaida yangu Mhariri nimepitapita pita katika mitandao ya kijamii na kukutana na chapisho ambalo ameandika mchambuzi wa soka kutoka hapa nchini Tanzania anayefahamika kama Presenter Noah kuhusu klabu ya Simba.
Katika chapisho lake ambalo nimeona niwashirikishe wadau wa Kijiweni na kupata maoni yao ni kuhusiana na mabadiliko ndni ya klabu ya Simba na kichwa cha chapisho lake ameandika SIMBA WANATAKIWA KUFANYA HAYA, ILI KUREJEA KWENYE USHINDANI WA UBORA nisiandike sana na mimi lakini tusome kile ambacho amekiandika kisha acha maoni yako hapo chini
- Badili viongozi- Wanaweza wakawa wamefanya mengi makubwa ila muda umefika wapishe sura mpya, zenye Maono mapya na vision mpya, kiongozi anayeleta mchezaji wa Timu nyingine kama maonesho ili kupooza mashabiki na kuamini kama kutengeneza whatsapp channel ni mafanikio kwa karne hii ni mambo ya aibu
- Watu wakae kwenye nafasi zao ofisini kutokana na majukumu yake kitaaluma(positions based on their merits)- Hakuna mambo ya kujuana au fulani katoka na timu mbali, na ndiomaana unaona kuna mashabiki wa Mnyama wanafanya kazi Yanga na wanafanya kwa ufasaha, so mtu bora apewe nafasi na afanye kazi
- Vunja Kikosi- wachezaji wanaotakiwa kubaki na wanapaswa kua kwenye first eleven ya Simba hawafiki sita, kikosi kifumuliwe na waje wachezaji wa maana kama ambavyo hua tunaambiwa thamani ya kikosi Ila wachezaji masalu wote watolewe na tuwashukuru kwa utendaji wao wakati wakiwa Simba
- Benchikha apewe Muda- sidhani kama panahitaji maelezo hapa, kocha ni bora na analijua soka la Africa, sasa chukueni report yake mpeni mahitaji yake achape kazi.
- Simba inatakiwa kua moja, slogan yetu ni Nguvu moja ila kwa sasa kila mtu anaimba wimbo wake, Simba hakuna kabisa unity na hii ni sababu ya uwepo wa watu wengi wenye ego na kutopenda sikiliza ushauri au kukosolewa, hii inafanya idara nyingi kuzorota na kutokua na ufanisi
Mwisho Tajiri Mo tunajua unaumia ila mashabiki wanaumia zaidi, tunaomba muwahurumie, uzuri kwenye moja ya interview zako ulisema Unawajua viongozi wanaoikwamisha Simba na ipo siku utawataja, sasa tunaomba usiwataje ila WATOKE ndani ya klabu. Ijengwe Simba mpya kuanzia kwenye uongozi mpaka kikosi.
Nawasilisha
Wewe maoni yako ni yapi? Tuambie kwenye comments hapa chini sasa
SOMA ZAIDI: Yanga Inabebwa Na Uimara Wa Eneo Hili Mbele Ya Simba
13 Comments
Ili kurejea katika ubora inahitajika afumue kikosi chote na akisuke upya hapo atarudi kwenye ubora tofauti na hapo,? Yuko hatarini kushuka daraja kabisaaaaa
By tajiri ABAS
Kwenye uongozi hapo upo Sahihi asilimia zote ni muda Sasa wa kupata watu wapya na kubadilisha ufanisi kwenye kuendesha klabu wakati mwingine mambo ya kujuana yanatukwamisha Wanasimba
Toa viongozi wote Tyr again Mangungu boy Kajula hawa wote tupa kule hawana msaada kwa simba kwa sasa
Mazao yakisua sua ng’olea mbali yapandwe mengine,,
Inabidi tupate uongoz mpya wenye views za kuifikisha Simba mbele. Pia wachezaj wanabidi wajitume Kwa mechi zilizobaki Ili walau tuambulie nafasi ya pili kabla Panga halijapita mwisho wa msimu.
Magugu,Try again na Kijola waondoke…hatuwezi Kaa na watu wa hovyo kiasi hiki kwa sasa
Mambo yasiwe mengi….
Kikubwa ni kitendo waache brabraaaaaa….
Msimu umeshawaacha wajipamge upya wasikate tamaa Hali wakijua ni suala la mda tu
Tajiri Abaaas
Benchikha siyo kocha mbaya lakn kila kocha anahitaj uongoz bora na Scouting ya maana ili kupata wachezaj aoneshe ubora wake haya mambo yafanyiwe kazi kuelekea next Season tunaitaka Simba tuliyozoea kuiona na siyo ya sasa hv
Labda mbadilishe timu iitwe simba wa yuda ila ivi ivi never 🤐🤐
Mimi nichoona na ninachopenda kuongea saahz si muda wa kubezana na wala kulaumiana yalipita ndio yashapita japo hatuwezi kuyafuta kwa muda huu kilichobaki sasa ni kumuachia kocha Benchikha timu apange kikosi atuletee wachezaji wa viwango kwa ajili ya msimo ujao sasa hapo tutamjua mchawi wetu
Wakubaki ni
1.ayoub
2.Israel
3.chama
4.kibu
5.(chasambi,duchu,barua ni hazing)
6.benchi zima la ufundi
Wachezaj Wakigen wakubaki ni Chama, ayoub, Malone baaaas hao wengine wapewe kiinua mgongo wajikatae na viongoz wao