Habari Mhariri,
Nikiwa na afya njema kabisa na amani ya moyo, Napenda barua hii iwafikie viongozi wa klabu ya Simba maana kinachoendelea ndani ya uongozi matokeo yake ndio haya yanaonekana kwa kipindi cha misimu hii mitatu,
Ikumbukwe Simba kipindi cha Barbara Gonzalez, tuliiona simba yenye ushindani na yenye mafanikio makubwa kana kwamba kumfunga mtu kama Al Ahly pale kwa Mkapa ikawa ni jambo la kawaida, mpaka hatua ya kuongoza kundi mbele ya bingwa wa kihistoria wa michuano ya mabingwa Afrika na kipekee ndio simba iliopofikia hatua za kutaka kufika mpaka nusu fainali kwa kumpiga Kaizer Chief ilihali mechi iliisha kwa idadi ya magoli isiokua rafiki kwa simba.
Unadhani kumfukuza Kocha Robertinho ilikuwa suluhisho? mbona amekuja bingwa wa shirikisho bado mambo ni yale yale? Hii dhahiri huonyesha udhaifu katika uongozi wa Simba. Katika ukweli pasemwe ukweli kama Yanga wataendelea hivi misimu miwili au mitatu basi ni dhahiri nusu fainali na mpaka fainali wanaingia katika ligi ya mabingwa Afrika maana wamethubutu.
Yanga ni timu yanye uongozi thabiti kupitia kwa Hersi Saidi na nikiri wazi kuwa anatakiwa kuigwa kwani timu ya soka ni uongozi na sio wachezaji
Mfano mzuri klabu ya Simba ilikua na mtu kama Augustine okrah, Jonas Mkude, Baleke Jean pamoja na Phiri Moses, hawa wote walikua wachezaji ambao kabla ya uongozi kupinda pinda wanafanya vizuri, ila sasa baada yake wakaonekana wabovu na kutemwa na ajabu walipo wanakiwasha vibaya mnooo.
Wekundu wa msimbazi wana watu ambao kama wakienda timu kama Azam au hata Yanga lazima tutashangaa, lakini viongozi wamebaki kaa na kumpangia kocha wale vijana ambao damu bado changa wapo jukwaani,
Mwisho niseme ikiendelea hivi hivi hata aje Messi au Ronaldo simba haiwezi kua imara kwani timu ni uongozi ndio wachezaji wafuate,
Katika Utekelezaji wa majukumu
Mohamedi Abdala Mohamedi
Mwanafunzi UDSM
SOMA ZAIDI BARUA NYINGINE HAPA
10 Comments
Mi naona viongozi wajiuzuru wote mana hawajui kuleta maendeleo ya kimpira zaidi ya kujinufaisha wamekalia majungu tu na propaganda
Hakuna viongozi Simba na ndio sababu hata muwekezaji wetu anakata tamaa, viongozi wengi wa Simba wapo kimipigo na wapo kwa maslahi yao binafsi! Tunaomba liangaliwe hili.
Ukweli ni kwamba tatizo la Simba halijawahi kuwa kocha hata kidogo bali viongozi. Kwa vikosi vinavyoyoka katika kila mechi ni wazi kuwa kocha ana shinikizo la nani achezee na nani asicheze, sio bure kila kukicha kikosi ni kile kile huku vijana wadogo wanaosajiliwa wanaendelea kukaa bench na wengine jukwaani. Uongozi uwajibike
Hap Simba wamtoe matora ndo anaharbu timu mtakuja kunikumbuk
Viongozi waachie ngazi kwakweli inatuumiza sanakuona wachezaji wazuri wanaondika watuletea siasa kwenye Moira wakati mambo yapo hadharani nitoshe kusema viongozi hatuwataki
Nakama Simba Kuna sehemu walimkosea mgunda wakamuombe msamaha kama timu aliifundisha akiwa Hana sub natimu ikafanya vizuri harafu hao viongozi wakaona hafai wakaanza kutafuta kocho ambae anasaini Hela ndefu kumbe yake kidogo hii inafikirisha sana ndo maana walimtoa baleke na kumleta Fred wakamtoa phili na kumleta jobe kifupi ipo siku watatukuta pale ofisini tumewasubili tuone wataingiaje ofisini
N wazi kabisaa viongoz wapo kimaslah Nd màan hata hawaonyesh kushtushwa na MATOKEO màan washaeka Chao mfukon tunaoumia n Sisi…..Viongoz hatuwatak tang mmeingia hamn maendleo yyte nmefanya sio kusajil Wala nn ishort hakun mlichofanya n zerooo sas tumechooka token hapo waje watu weny uchungu wa kuipeleka team mbal na sio siasa
Pingback: Itawachukua Muda Mrefu Sana Yanga Kumpata Golikipa Mwingine - Kijiweni
yani wanatuumiza sana mbona kama timu hela inayo alafu wanafanya sajili za bei rahisi mana ukitaka kizurii lazima ugharamikie jaman uongozi wa simba mnatuumiza sana mashabiki
Siwezi sema kama kuna upigaji kwa kuwa sina uthibitisho wa ilo ila naweza sema kuna jambo ambalo si jema linaendelea ndani ya uongozi na si kosa lao kuwa nalo ndani ya uongozi nasi kulitoa nje kwani ndiyo uongozi ulivyo si kila jambo litatoka nje, kuna changamoto zingine zinatafutia suluhu ndani kwa ndani na changamoto kwenye jambo lolote ni kawaida sana ila mnaliondoa vipi ilo ndiyo jambo la msingi.
Kwa upande wangu nawaombea nguvu na busara viongozi wa SIMBA katika utendaji wao wa kazi na kuwa watulivu kwa kutokata tamaa au kusongwa na lawama zinazoendelea.
Kocha la Mpira,
Mwl. Ally Mussa
Ruangwa-Lindi