Mchezo ulikuwa wa kimbinu zaidi kwa pande zote mbili yaani Yanga pamoja na Mamelodi kiasi ambacho hatukutarajia mchezo wa namna hii timu zote zikicheza taratibu hususani wakiwa kwenye nusu yao na wakati wakivuka kwenye nusu yao kasi iliongezeka.
Mamelod walianza na kumiliki mpira zaidi eneo Lao na muda mwingi walipiga pasi fupifupi kwa mabeki wao wawili wa kati wakipasiana na kipa wao Ronwen William kitu ambacho mabeki wa pembeni walikuwa juu kidogo na viungo wawili wakiwa mbele Ya mabeki wao.
Kwanini walicheza hivyo? Kumfanya Yanga SC kuja juu na kuweka presha kwenye mpira na hiyo ingempa nafasi kubwa ya kupata njia rahisi Ya kupiga pasi na kumshambulia Yanga SC ila mianya hiyo ilikosekana na hata ukiangalia nafasi chache walizopata kupenyeza mpira walifika golini kwa Yanga SC zaidi wakitumia pembeni.
Yanga SC waliwezaje kuwazuia? Kukaa nyuma kwa kuwa na mabeki 4 na viungo 4 huku Kennedy Musonda na Clement Mzize wakiwa juu na Mara nyingi walikuwa kwenye nusu Ya Mamelod Sundowns. Walifanikiwa kwa kuwanyima nafasi Mamelod ya kupita katikati mwa uwanja na ilo walifanikiwa kwa kukabia zaidi chini huku Kennedy akikimbia zaidi na mara nyingi alishuka na kupanda akitokea pembeni pamoja na Max Nzengeli na ilo iliwafanya kuwa wachezaji waliyokimbia zaidi wakitokea pembeni sana sana kwa Musonda.
Kipindi cha pili kilibadilika kidogo na timu zote zilifunguka na kufungua uwanja jambo ambalo lilitoa zaidi nafasi “space” Kwa timu zote kupiga pasi na hiyo ilisababisha timu zote mbili kufunguka na kupishana na hiyo ilitoa nafasi timu kufika golini kwa mwenzake kirahisi tofauti na kipindi cha pili.
Timu zote zilifanikiwa vipi ? Kutotoa mianya au nafasi ya kufunga na hiyo ilichangiwa zaidi kwa timu zote kuwa makini na kufanya ulinzi mzuri muda wote wachezaji walikuwa “Active” kwa pande zote mbili.
Kipi kilikosekana kwa timu zote. Kubwa ni kutumia nafasi chache walizopata kuna nyakati Clement Mzize alipata nafasi ambayo ilihitajika kwa yeye kufunga goli ila ilikuwa tofauti, upande wa Mamelod Sundowns walishindwa kuwa na pasi sahihi eneo la mwisho (ushambuliaji) na mara nyingi walipoteza pasi kirahisi.
Mchezo ulichezwa zaidi eneo la kati kama ambavyo awali kabla ya mchezo kuonyesha kuwa eneo la Kiungo ndiyo eneo mama kwa timu zote. Mudathiri Yahya alizunguka zaidi mbele ya Jonas Mkude akupanda juu kama tulivyomzoea na ilimpa nafasi Mkude kuzuia kwa urahisi na kuwafanya kuwa salama. Mamelod Sundowns wao kipindi cha pili waliamua kukabia juu na ilisababisha kwa nyakati tofauti Yanga SC kutengeneza shambulizi kupitia pembeni japo ufanisi kwenye kufunga ulikuwa mdogo sana.
NB: Nafasi chache za kufunga zilitengenzwa tofauti na matarajio ya wengi, Yanga SC wakikabia chini zaidi huku Mamelod wakikabia juu.
Max Nzengeli, Kennedy Musonda pamoja na Mudathiri Yahya walikimbia sana siku ya leo na mara nyingi mikimbio yao ilikuwa na faida kwa timu, Clement Mzize anahitaji kuongeza umakini na kuwa katili kwenye eneo la mwisho kufunga.
Ronwen William mtulivu sana anapiga pasi na kuelekeza pia sawa na Djigui Diara japo kwa leo hakukaa na mpira muda mwingi.
Huyu beki Khuliso Mudau anakimbia kuna nyakati Kennedy Musonda aliamua kupiga mipira mirefu alafu akimbizane naye ila alikuwa akishinda zaidi yeye na kushinda, ana uwezo mzuri wa kupiga “tackling” na kwenye Njoo na yeye aje ni mzuri sana inahitaji umakini sana kumpita.
Timu mbili tofauti ambazo zinalandana kwenye aina yao ya kiuchezaji na mechi ilikuwa katikati zaidi Ya uwanja.
SOMA ZAIDI: Yanga Dhidi Ya Mamelodi Uchambuzi Wa Mbinu Na Vikosi
1 Comment
Wakaongeze bidii kwenye eneo la ushambuliaji