Ni Simba dhidi ya Al Ahly moja kati ya mchezo mkubwa na wenye matokeo ya kufurahisha kwa timu zote mbili, kwa sasa hakuna timu isiyomjua mwenzake wamekutana zaidi ya mara ya tatu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mara mbili pekee wakikutana kwenye mchezo wa African Football League.
Michuano ya Ligi ya Mabingwa mpaka sasa baina yao wawili wamekutana mara 4 huku mara mbili wakikutana kwenye African Football League AFL na kufanya kuwa michezo sita (6), katika michezo hiyo 4 ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Simba SC akiibuka na ushindi mara 2 na Al Ahly naye akishinda mara 2 huku yakifungwa jumla ya magoli 8 huku Simba SC akifunga magoli mawili pekee na Al Ahly akifunga magoli sita. Uzuri ni kuwa michezo hiyo 4 ilikuwa ya Makundi ambapo msimu wa 2018/2019 walikutana kwenye kundi D Simba akiibuka na ushindi 1-0 nyumbani na akipoteza 5-0 ugenini pia msimu wa 2020/2021 walikutana tena na kila mmoja akiibuka na ushindi wa 1-0 nyumbani kwake.
Nje ya michuano ya CAF Champions League Simba SC na Al Ahly SC wamekutana tena kwenye michuano ya African Football League kwenye hatua ya mtoano ambapo mchezo wa kwanza Simba SC walitoka Sare ya 2-2 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa na kutoa tena sare ya 1-1 nchini Misri Nyumbani kwa Al Ahly na kutolewa kwa goli la ugenini.
Wachezaji wanaongoza mpaka sasa kufunga magoli baina yao walipokutana mara zote sita, nne za CAFCL na mbili za AFL ni kiungo wa Simba SC Sadio Kanoute pamoja na KMahmoud Kahraba ambao wote wamefanikiwa kufunga magoli mawili na yote wamefunga kwenye michuano ya AFL huku Karim Nedved naye akifunga mawili kwenye CAFCL Pia kwenye CAFCL wapo wengine wakiwa wamefunga magoli mojamoja kwa wachezaji mbalimbali akiwemo Medie Kagere, Luis Miquissone kwa upande wa Simba SC na Mohamed Sherif, Amr Al Sulaya, Ali Maaloul, Junior Ajayi pamoja na Karim Nedved kwa upande wa Al Ahly.
Michezo yao mitano ya mwisho msimu huu kwenye mashindano yote Al Ahly wamefanikiwa kufunga magoli jumla ya magoli 12 na wakiruhusu magoli matano na kwa upande wa Simba SC wamefunga magoli 14 na wakiruhusu magoli matatu.
Timu zote mbili ni waumini wakubwa wa kuweka mpira chini kwa pasi fupi fupi wakitokea chini, Simba SC wamekuwa wakitumia zaidi mfumo wa 4-2-3-1 ambapo wamekuwa wakitumia zaidi viungo watatu kushambulia na wawili wakikaba huku wakisimama na mshambuliaji mmoja pia kwa upande wa Al Ahly wamekuwa wakitumia zaidi mfumo wa 4-3-3 ambapo Reda Slim, Antony Modeste na Karim Fouad wakisimama eneo la ushambuliaji huku Emam Ashour, Marwan Attia na Mohamed Kashfa wakiwa eneo la kati (kiungo) kusaidia mashambulizi na kukaba pia huku Mohamed Kashfa na Marwan Atti wakitumika zaidi kukaba na kushambulia na Emam Ashour akiwa zaidi eneo la kushambulia.
Uzuri ni kuwa kila timu ina nafasi ya kuweza kufunga goli na hiyo inachagizwa na matokeo ya michezo mitano ya mwisho ya michuano yote wakiwa wamefunga magoli huku wakiwa na wastani mdogo wa kufungwa magoli, pia pale timu hizi zinapokutana daima panakuwa na upatikanaji wa goli hivyo kiufupi kuna asilimia kubwa mchezo huo usimalizike bila kupatikana goli kwa timu zote mbili.
Namna timu zote mbili zikicheza inachagiza kushuhudia mchezo mzuri ambao timu zote hazina mchezo wa kubaki nyuma tofauti kubwa kwao ni kuwa Al Ahly wakivuka kwenye nusu yao wamekuwa wakiongeza kasi ya kushambulia zaidi tofauti na Simba SC ambao wao wamekuwa wakicheza taratibu na wakati mwingine wakitumia mipira mirefu na “Press” ndogo kwa mpinzani wao wakiwa na mpira.
Kipi Simba SC wafanye ili waweze kuibuka na Ushindi ? Kikubwa ni wao kutumia zaidi nafasi chache watakazopata kufunga magoli na kuepuka kupoteza ovyo nafasi hizo. Upi udhaifu wa Al Ahly ni kuwa na mchezo wa kutoka zaidi hususa maeneo yao ya pembeni ambapo Percy Tau na wakati mwingine Emam Ashour wakishambulia zaidi upande huo, huko ndiyo maeneo ambayo Simba SC wakiyatumia vizuri wanaweza kupata nafasi kivipi ? Uchezaji wao mara nyingi wanajaa eneo la kati kuanzia wakianzisha mashambulizi. Upi ni ubora wa Al Ahly? Kubwa zaidi ni eneo Lao la kiungo wamekuwa bora sana eneo ilo uwepo wa viungo wao Aliou Dieng na Marwan Attia pamoja na Kashfa.
Ubora upi wa Simba SC ? Ni eneo Lao la nyuma wamekuwa bora sana na wakitekeleza majukumu yao vizuri pamoja na eneo Lao la ushambuliaji wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi japokuwa matumizi Ya nafasi yamekuwa kidogo tofauti na wapinzani wao ambao wamekuwa na uwiano mkubwa zaidi wa kupiga mashuti yanayolenga lango zaidi japoku nao wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi.
Tutashuhudia mchezo mzuri wenye mbinu na ubora kwa wachezaji wa timu zote mbili, Simba SC wanapaswa kutumia zaidi nafasi zao kwa usahihi.
SOMA ZAIDI: Yanga Akimfunga Mamelodi Kwa Mkapa Anafuzu Nusu Fainali
1 Comment
Pingback: Kuhusu Simba Nilitegemea Baada Ya Kumuona Mchezaji Huyu - Kijiweni