Naweza kusema ushindi wa bao 4 kwa 0 dhidi ya CR Belouizdad na kuwafanya Yanga kufuzu hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya klabu yao na kuwafanya wananchi watambe usiku kucha na balaa la timu yao ni moja kati ya tukio kubwa sana litakalobaki katika historia kwa wananchi daima.
Yanga wameamua kutuonesha kuwa mpira ni uwekezaji na sio propaganda za mitandaoni jambo ambalo limewaziba midomo wengi na kuwafanya wao wajibu kwa vitendo zaidi uwanjani.
Wakati Yanga wanashiriki mpaka kufika hatua ya fainali ya kombe la shirikisho Afrika kulikua na propaganda za Yanga kushiriki kombe la looser (shirikisho), wakatoka hapo Yanga ikagonga mpaka fainali huku timu zikichapwa ipasavyo wakasema wamekutana na timu dhaifu, lakini wale wale waliowai kucheza hilo hilo kombe la looser wakaishia kuchoma uwanja wa watu na kutupwa nje ya michuano wakaishia robo fainali!
Wakatoka hapo wakahamia klabu bingwa wakabwata tena kwamba Yanga hatoboi kwenye hii ligi ya wanaume huku hakuna kina Malumo wala Rivers United, Haya wamepangiwa magiant wawili waarabu wagumu mabingwa wa Misri, mabingwa wa Algeria, na mabingwa wa Ghana, katika kundi ilo katoboa, katoa SARE mbili, kashinda 2, na kafungwa 1 mpaka Sasa kafuzu robo fainali akiwa na mechi moja mkononi!
Kafuzu kwa mpira mkubwa na wa kitabuni na sio wa kubahatisha na kushikilia roho, kaubonda mwingi sana!
Sasa siwezi Kuona ajabu wakitinga nusu fainali ya klabu bingwa na kuandika historia ya kipekee kwakuwa uwezo wanao, Nia wanayo na kikosi bora wanacho cha kufanya hivyo na sio unga unga mwana kama wazee wa propaganda!
Watu walikuwa wanajiandaa na mechi ya Belouizdad wengine walikuwa wamebaki kujadili bleach za wakina pacome, wakasahau walikuwa na mechi kule Ivory coast! Ubora wa kikosi cha Yanga utaendelea KUWAZIBA MIDOMO wengi hawaendi kwa kubahatisha bali kwa mipango madhubuti ya usajili bora na uongozi imara.
SOMA ZAIDI: Ningekua Gamondi Ningeanza Hivi Kwa CR Belouizdad
2 Comments
Pingback: Barua Nzito Ya Shabiki Wa Simba Kwenda Kwa Yanga - Kijiweni
Pingback: Hizi Ndio Pesa Za CAF Kwa Kila Hatua Ligi Ya Mabingwa - Kijiweni