Mnyama simba yupo zake ugenini leo hii nchini ivory coast akiwinda alama tatu dhidi ya Asec Mimosas na ni Simba na Asec wanakua ni moja kati ya vilabu vya kwanza kabisa kutoka barani Afrika kutumia dimba la Felix Boigny baada ya Afcon kumalizika nchini humo hivyo hakuna kisingizo chochote leo katika eneo la kuchezea na miundombinu yote kwa ujumla.
Kwenye mchezo wa leo ni muhimu sana kocha kuanza na Saido Ntibazonkiza licha ya kuwa na pandashuka za kiwango msimu huu lakini uzoefu wake hakuna asiyeifahamu ukiongeza na uzoefu bado utambeba Saido kuanza leo hii.
Kocha wa Asec amezungumzia suala la kumkosa mshambuliaji Sankara Karamoko ambaye ametimkia nchini Austria lakini simba wana Saido ambaye kacheza ligi kuu Ufaransa na nahodha wa timu ya taifa ya Burundi KWANINI asianze kikosi cha kumi na moja bora?? Ndio maana naona kuwa sina shaka na hofu yoyote akianza muhimu ni awe sahihi tu kwenye matendo yake.
Ukiachana na Godfather wa Bujumbura mtu hatari zaidi kwa Asec leo hii ni mwamba wa lusaka Chama yuko kwenye fomu nzuri ya kutafuta mkataba mpya sasa hivo hazuiliki kabisa na goli alilowafunga JKT Tanzania katika ligi kuu linazungumza vyote na ni wazi jamaa anaugwadu kweli kweli kwa sasa, anapenda mechi kubwa na anaweza kuzicheza na kwa chama unapata tafsiri halisi ya big names can make big stories.
Kila la kheri mnyama kazi kwenu kuwatoa wenge la ubingwa wa Ivory Coast leo hii.
SOMA ZAIDI: Naamini Kuwa Medeama Ndio Msaada Mkubwa Kwa Yanga