Lazima tuzungumze na hatuwezi kunyamaza katika hili, kwenye uwanja zipo sheria ambazo zinaamuliwa na mwenye kuzisimamia ni mwamuzi sasa tukianza kuziamua sisi maana yake tumekosa imani na wasimamizi wa mpira wetu.
Kuanza kumwandama mchezaji mmoja kila kukicha ni kampeni za waziwazi ambazo kwa namna moja au nyingine zinaonesha namna gani tumekua na roho mbaya juu yake, Khalid Aucho ni mchezaji ambaye amekuja kutafuta ugali wake na wote tunafahamu ukicheza eneo la kiungo namba Sita jukumu lako mama ni kukaba, sasa namna unavyoelezewa Aucho ni kama anawauwa wachezaji wenzake,
Wakati mwingine tukubali kuuzungumza mpira tusiongelee vitu vingine ikaonekana kama kuna chuki juu ya kitu fulani, huwezi kucheza namba Sita halafu ukawa lelemama hakuna mpira wa hivyo duniani, Kiungo mkabaji lazima uwe na roho ya kikatili, lazima ukabe kwelikweli ila usivunje sheria, anachokifanya Aucho ni utekelezaji wa namba yake na wala hana hayo yanayozungumzwa.
Siyo mara moja kwake kuchezewa madhambi na hakuna kiongozi yoyote wa Yanga aliwahi kutoka na panga kuhusu hilo, si yeye mchezaji kuwahi kulalama kwani anafahamu huu ni mpira siyo drafti kwamba hakuna kugusana, kitendo cha kuanza kuwaelekeza Waamuzi nini wafanye kwa Khalid Aucho au Bodi ya Ligi na watu wake siyo sawa, yaani tunaanza kuhama kwenye mpira tunaenda kwenye maelekezo ya chuki.
Tunafahamu umuhimu wa Aucho na Yanga yake hii isitumike kwa wapinzani kutaka mchezaji huyu afungiwe ili wengine waanze kunufaika na pengo lake, kama timu zote zimesajili zicheze mpira ziache mbinu chafu kwa mchezaji anayetimiza majukumu yake. Ningewaona wa maana sana kama wangekumbushia zile rafu mbaya ambazo hadi leo hii hakuna adhabu yoyote juu ya wachezaji wale.Tumuache mchezaji acheze mpira kwani hii ndio ajira yake kama ilivyo ya kwako.
SOMA ZAIDI: Kiburi Cha Chama Kinalindwa Na Mashabiki Wa Simba
1 Comment
Pingback: Kama Una Tabia Hizi Hupaswi Kuitwa Shabiki Wa Yanga - Kijiweni