Leo ni ile siku ambayo bila shaka waafrika kusini na wakongo watakua makini kabisa bila kusahau mashabiki wa soka barani Afrika kutazama mtanange wa kutafuta mshindi wa 3 wa michuano ya mataifa barani Afrika ambapo South Africa anakutana na DR Congo.
Ni mchezo ambao unawakutanisha wachezaji wenye vipaji vikubwa sana barani Afrika ambao wanacheza nje ya bara hili lakini pia wale ambao wanacheza soka ndani ya bara hili na hapa tutazame wachezaji ambao unapaswa kuwaangalia kwa jicho la tatu kabisa katika mchezo huu.
Taboho Mokoena
Huyu ni kiungo mshambuliaji wa South Africa ambaye amekuwa na mashindano bora ya AFCON na amekuwa mhimili mkubwa kwa taifa ilo kwenye michuano ya msimu huu.Amekuwa akitekeleza majukumu yake mama ya kushambulia ila amekuwa pia akisaidia kukaba, amecheza michezo yote ya AFCON mpaka sasa akiwa amefunga goli 2 na kutengeneza moja, ni moja ya mchezaji wa kuangaliwa kwenye mchezo wa mshindi wa tatu na anavaa jezi namba 4.
Aubrey Modiba
Ni kiungo mkabaji wa timu ya taifa ya Afrika Kusini amekuwa akifanya kazi kubwa sana ya kukaba anavaa jezi namba 6 mgongoni. Ni mhimili wa Afrika Kusini kwenye eneo la kiungo mkabaji anakaba kisawasawa na amecheza michezo yote 6 kuonyesha umuhimu wake kikosini, mpe jicho lako kwenye mchezo wa mshindi wa tatu.
Khuliso Mudau
Ana miaka 28 anacheza kama beki wa pembeni na wakati mwingine kama kiungo amekuwa akipanda na kushuka kusaidia mashambulizi pamoja na kukaba wakati wakiwa wanashambuliwa. Anavaa jezi namba 20 mgongoni akiwa na kikosi cha Bafana Bafana, mpe umakini wako kwenye mchezo wa leo dhidi ya DR Congo.
Meshack Elia
Mshambuliaji wa DR Congo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu hiyo kuanzia michezo ya awali, hatua ya makundi alikuwa akitumika zaidi kipindi cha pili ila kuanzia 16 bora amekuwa akianza kwenye kikosi cha kwanza. Mpaka sasa amechangia magoli 2 akitengeneza pasi ya goli 1 na amefunga goli 1 amekuwa wa kuchangia zaidi mashambulizi kuliko kuzuia ni hatari sana kuanzia eneo la katikati mwa uwanja kuelekea kwenye nusu ya mpinzani, ni moja ya mchezaji wa kuchungwa dhidi ya South Afrika anavaa jezi namba 13.
Yoanne Wissa
Ni kiungo mshambuliaji wa DR Congo anavaa jezi namba 20 mgongoni ana miaka 27 akiwa amehusika kwenye magoli 2 na mchango huo amefunga magoli 2. Ni moja ya winga wa kuchungwa na amekuwa winga ambaye anatokea pembeni kuingia ndani ya eneo la mpinzani.
Arthur Masuaku
Ni beki wa pembeni wa DR Congo ila ni wa kuchungwa sana kwani mpaka sasa amefunga goli 1 kwenye AFCON. Ni beki ambaye anapanda na kushuka akisaidia majukumu yote mawili kukaba kama jukumu lake mama la eneo analocheza pamoja na kupandisha mashambulizi, ana vaa jezi namba 26 mpe jicho lako kwenye mchezo wa mshindi wa tatu dhidi ya South Afrika “Bafana Bafana”.
SOMA ZAIDI: Ukiizungumzia Nusu Fainali AFCON Huwezi Yaacha Majina Haya