Ni zaidi ya miongo mitatu sasa tangu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) kuanzishwa na kushuhudia mataifa mbalimbali yakipokezana taji hili hasa yale ambayo yana wastani mzuri wa wanasoka wanaosukuma kabumbu nje ya bara la Afrika.
Mwaka 2023, Taifa la Ivory Coast limebahatika kuandaa AFCON ya 34 huku Mataifa yenye Idadi kubwa ya wachezaji wanaokipiga kwenye Ligi za ndani ya bara hili wakionesha Mapinduzi makubwa na kutingisha vigogo kadhaa huku toleo hili la 34 la AFCON limekuwa tofauti wengi wa waafrika waliamini mataifa ambayo yana wachezaji wengi wanaocheza nje ya bara ili wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri ukilinganisha na mataifa ambayo vikosi vyao vimeundwa zaidi na wazawa wanaocheza Ligi za nyumbani kwao pamoja na ndani ya bara la Afrika.
Imekuwa tofauti sana kwani sehemu kubwa ya wachezaji waliyofanya vizuri wanacheza Ligi za ndani ya bara la Afrika kama Henock Inonga wa DR Congo, Percy Tau wa Afrika Kusini, Djigui Diara kutokea Mali, Aliou Dieng wa Mali, Ali Sangare wa Ivory coast na zaidi ni kuwa Afrika ya Kusini imeheshimisha Ligi za ndani ya bara la Afrika ikiwa klabu pekee yenye wachezaji wengi wanaokipiga Ligi za ndani ya bara hili.
Wanaturudisha nyuma na kutupa kumbukumbu ya Spain iliyokuwa na wachezaji wengi wanaokipiga ndani ya Spain huku robo tatu ya kikosi kikiwa ni cha FC Barcelona. Mpaka wanafika hatua hii ya nusu fainali robo tatu ya kikosi chao kinaundwa na wachezaji wanaocheza klabu ya Mamelodi Sundowns ya nyumbani Afrika kusini.
Shujaa wa hatua ya nusu fainali Ronwen Williams, mabeki Aubrey Modiba, Mothobi Mvala, Grant Kekana, Khuliso Mudau, viungo Teboho Mokoena, Themba Zwane pamoja na Thapelo Morena na hawa wachezaji huwa ndiyo waliocheza sana kwenye kikosi hicho cha Bafana Bafana.
Lakini kikubwa zaidi ni kuwa kikosi chote cha Afrika Kusini “Bafana Bafana” kinaundwa na wachezaji kutoka vilabu saba vya Afrika kusini na kimoja nje ya taifa ilo huku wachezaji wawili (2) tu kutokea nje ya bara la Afrika ambao ni kiungo Mihlali Mayambela kutokea Aris Limassol ya Cyprus pamoja na kiungo Sphephelo Sithole kutokea Tondela ya Ureno.
Vilabu ambavyo vimefanikiwa kutoa wachezaji ndani ya kikosi hicho kutokea PSL ni Pamoja na Mamelod Sundowns, Orlando Pirates, Amazulu, Cape town City, Polokwane city, Stellenbosch FC pamoja na Sekhukhune United. Kumbuka kuwa Afrika Kusini ndiyo taifa ambalo limefuzu hatua ya nusu fainali na wachezaji kutokea Bara la Afrika tofauti na Nigeria yenye wachezaji wengi kutokea nje, Ivory Coast na DR Congo pia. Huu ni wakati sasa kujiamini kuwa bara la Afrika tunaweza na vipaji tunavyo lakini pia ni fundisho kuwa siyo lazima kuwekeza kwa wachezaji wanaocheza nje ya bara la Afrika bali ni njia nzuri za kimpira kuanzia uwekezaji, imani, uvumilivu na kujitoa kwa wasimamizi wa mpira ndani ya nchi husika.
SOMA ZAIDI: Inonga Kuondoka SIMBA Baada ya AFCON?
3 Comments
Pingback: Ratiba Kamili Nusu Fainali AFCON - Kijiweni
Pingback: Ukiizungumzia Nusu Fainali AFCON Huwezi Yaacha Majina Haya - Kijiweni
Pingback: Wachezaji Watano Muhimu Wa Kuwapa Ubingwa Ivory Coast - Kijiweni