Wakiwa na kumbukumbu nao ya kuwatoa katika kombe la FA hii leo klabu ya Simba wako ugenini kukabiliana na Mashujaa katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma moja kati ya mechi kubwa kwa hii leo kutokana na umuhimu wa mchezo huu kwa timu zote mbili.
Ugumu wa mchezo wa leo kati Mashujaa dhidi ya Simba utakuwa kwenye maeneo mawili ambapo moja ni nafasi ya 15 aliyopo Mashujaa sio nzuri sana hivyo atahitaji kujinasua huko kwa kupata matokeo Chanya na kubwa zaidi ukizingatia yupo kwenye dimba lake la Lake Tanganyika ongeza na maingizo mapya kwenye kikosi chao hii itaongeza morali ya wachezaji kupambana zaidi kupata matokeo.
Lakin wanaenda kucheza dhidi ya Simba ambao pia wamekuwa hawana muendelezo mzuri wa kiwango na matokeo ya hivi karibuni ila kutokana na matokeo ya jana ya Mtani wao Yanga itaenda kuongeza hali ya kupambana zaidi kuweza kushinda ili kumsogelea lakini pia kurejea kwa wachezaji wao muhimu ambao walikua majeraha na wale ambao walikua katika michuano ya mataifa barani Afrika haswa Clatous Chama.
Yanga amecheza michezo 12 alama 31 huku Simba ataenda kucheza mchezo wa 11 akishinda atafikisha alama 26 na mchezo mkononi hapo unaona ni mechi ya lazima kwa klabu ya Simba kushinda hii leo kwani ataingia kama timu ya kwanza kwenye mchezo huu kutokana na ubora wa kikosi chake dhidi ya Mashujaa, hivyo Mashujaa ili wafanikiwe kupata alama kwanza kuwaheshimu Simba alaf kufanya mambo ya Msingi uwanjani.
Januari 31 Simba ilicheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Tembo katika mchezo wa Azam Sports Federation uliochezwa Uwanja wa Azam Complex huku februari Mosi Kikosi kilitua mkoani Kigoma kwa ajili ya kukabiliana na Mashujaa FC kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Februari 3, 2024 Uwanja wa Lake Tanganyika.
SOMA ZAIDI: Chama amedhihirisha kuwa viongozi wa simba ni wababaifu