Mpaka sasa yale majina makubwa ambayo yalikua yanategemewa kuwa yataibuka kuwa wafungaji bora wa michuano ya mataifa barani Afrika(AFCON) wamezidiwa kwa idadi kubwa kabisa ya magoli na mchezaji ambaye hakutegemewa kabisa kama atakua na mabao mengi kiasi hiki mpaka sasa.
Anaitwa Emilio Nsue ambaye akiwa katika klabu yake ya CF Intercity ambayo inashiriki ligi daraja la tatu anacheza kama kama beki wa kulia lakini katika timu yake ya taifa ya Guinea ya Ikweta anacheza kama mshambuliaji huku nafasi hiyo ikimlipa zaidi katika michuano hii kwani mpaka sasa anaongoza orodha ya wafungaji bora akiwa na mabao 5 huku anayemfuatia akiwa na mabao 2.
Katika maajabu ambayo yametokea katika michuano hii, Nsue ndie mchezaji pekee ambaye amefunga mabao matatu katika mchezo mmoja huku akiwafunga mabao 2 wenyeji wa michuano ya msimu huu timu ya Ivory Coast.
Katika hatua ya makundi ambayo mpaka sasa inaelekea kutamatika huku baadhi ya timu za taifa zikiwa tayari zimefuzu katika hatua inayofata ya 16 bora mchezaji pekee ambaye alifunga zaidi ya mabao 5 katika hatua ya makundi ni Laurent Pokou kutoka nchini Ivory Coast ambaye alishinda mabao 7.
Kuna wakati unajiuliza kwanini yale majina makubwa kutoka ligi kubwa mbalimbali ulaya hawajafanikiwa kufikia idadi kubwa kama hii aliyonayo Nsue lakini unaamua kukaa kimya na kuendelea kuamini maneno ya Rais wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe aliposema michuano hii itakua michuano bora zaidi kutazama barani Afrika.
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mara nyingi huleta pamoja wachezaji wanaotoka katika ligi tofauti duniani, na ni wazi kuwa wachezaji wanaotamba katika ligi kubwa ulaya hawatilii sana maanani katika AFCON. Hali hii inaweza kueleweka kwa kuchambua mambo kadhaa yanayoweza kuchangia utendaji duni wa wachezaji hawa wakati wa michuano hiyo.
Wachezaji wanaotoka katika ligi kubwa ulaya mara nyingi hupata changamoto kubwa kutokana na tofauti za utamaduni na mifumo ya timu wanazojiunga nazo katika AFCON. Wanaweza kuwa hawajazoea mifumo mipya au njia tofauti za kucheza, na hivyo kuchukua muda Kwenda saw ana mazingira ya timu husika.
Wachezaji wa ligi kubwa ulaya mara nyingi hushiriki katika msimu mrefu na unaoshughulika na mashindano mengi kama vile Ligi Kuu ya England, La Liga, Serie A, na Bundesliga. Kabla ya kushiriki katika AFCON, wengi wao wanaweza kuwa wamechoka kimwili na kiakili kutokana na majukumu mengi ya michezo wanayoshiriki.
SOMA ZAIDI: Tanzania Dhidi Ya DR Congo Ni Vita Ya Kujuana
1 Comment
Pingback: Taifa Stars Ilikosa Kujiamini Hakukua Na Mipango Sahihi - Kijiweni