Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2023 (AFCON) ni moja kati ya tukio kubwa katika kalenda ya michezo ya bara la Afrika ambalo limekua na maajabu mengi makubwa lakini msimu huu kukiwa na maajabu zaidi ambayo hayajafikiriwa kutokea. Kunzia hatua ya mechi za makundi mpaka hatua ya 16 bora ambayo ndio inaenda kuanza tumeshuhudia matukio makubwa, ushindani wa hali ya juu, na maajabu mengi katika viwanja mbalimbali ambavyo mechi mbalimbali zimechezwa.
Katika michuano ya mwaka huu kumekua na timu kadhaa kutoka bara la Afrika ambazo zimefuzu zikiwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu na ubora mkubwa wa kisoka na ikumbukwe kuwa wapo wachezaji ambao wameshiriki wakitoka ligi kubwa barani Ulaya. Wachezaji wengi kama vile magolikipa , washambuliaji , na viungo wat imu wamekua wakionesha ubora mkubwa ingawa wapo wachache ambao wamekua wakichukua tuzo za mchezaji bora wa mechi.
Kuna baadhi ya timu ambazo hazikutarajiwa lakini zimeonesha uwezo mkubwa sana na wa kushangaza katika michuano hii.Kunzia katika makundi nchi kama Cape Verde ni moja kati ya nchi ambayo imewashangaza wengi katika michuano hii kwa kumfunga mwenyeji kwa idadi kubwa zaidi ya magoli lakini pia na kufuzu hatua inayofuata.
Kama inavyotokea mara nyingine katika mashindano makubwa, AFCON 2023 imeshuhudia matokeo ya kushangaza na maajabu. Timu zilizopigiwa chapuo kubwa zimekutana na changamoto kutoka kwa wapinzani wasiotarajiwa, na haya yamechangia kufanya mashindano kuwa ya kusisimua na kutotabirika.
Michezo hii imeonyesha namna ambavyo umoja wa bara la Afrika kupitia soka ulivyo kwani mashabiki, wachezaji na viongozi wa timu wameonesha hamasa na uzalendo wakiyafanya mashindano haya kuwa fursa ya kuimarisha umoja wa mataifa ya Afrika.
Hii ni michuano ambayo daima itaacha alama kubwa katika historia ya mpira wa miguu barani Afrika kwani michuano hii imetoa fursa kwa wachezaji kujitambulisha kimataifa, kwa timu kuonyesha ubora wao na kwa mashabiki kushuhudia maajabu ya soka la Kiafrika. Tuna matumaini kuwa mafanikio haya yatachochea ukuaji zaidi wa mchezo huu na kuleta heshima kubwa kwa bara letu.
SOMA ZAIDI: Balaa La Cape Verde Katika AFCON