Golikipa bora kwa sasa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara yaani NBC Premier League Djigui Diarra ambaye anakipiga katika klabu ya Yanga ameendelea kumuaminisha kocha mkuu na kocha wa magolikipa wa timu ya taifa ya Mali kuwa yuko vyema langoni na anaweza kudaka katika mechi za timu yao ya Taifa katika michuano ya mataifa barani Afrika yaani AFCON inayofanyika nchini Ivory Coast.
Katika michezo yote miwili ya AFCON hatua ya makundi golikipa huyu wa klabu ya Yanga ameanza katika milingoni mitatu huku katika dakika 180 za michezo hiyo miwili akiruhusu bao 1 pekee katika mchezo dhidi ya Tunisia ambao uliisha kwa sare ya bao 1:1.
Kuanza golini kwa Djigui Diarra katika lango la Mali ni faida kwake kwa sababu anazidi kujiongezea thamani na umri wake wa miaka 28 unamruhusu Kwenda kucheza barani Ulaya kumbuka michuano ya AFCON 2023 inayoendelea pale nchini Ivory Coast ina mawakala wengi hivyo haitakuwa jambo la kushangaza kama Diarra akapata dili ya kwenda Ulaya.
Kama ulikua hufahamu tu ni kuwa Diara hayupo kimakosa katika timu ya taifa ya Mali kwani amecheza michuano ya kombe la Dunia Under (20) hadi nusu fainali akilitumikia taifa lake huku akidaka penati mbili kwenye robo fainali dhidi ya Germany na kuifanikisha timu yake ya taifa kutinga nusu fainali.
Amecheza fainali za (AFCON) under 23 akiwa golikipa namba moja. Kwenye tuzo za (CAF) 2015, Djigui Diarra aliorodheshwa kwenye tano (5) bora ya magolikipa bora chipukizi barani Afrika.
Diarra amecheza fainali za (CHAN) mara mbili kwenye Senior team akiwa golikipa namba moja wa Mali Katika fainali hizo za (CHAN) mwaka (2016).
Aliisaidia timu yake ya Mali kutinga fainali,, Walipoteza dhidi ya timu ya taifa ya DR Congo kwenye fainali hiyo. Diarra aliorodheshwa kuwa golikipa bora namba (2) Afrika mwaka (2016). Ambapo alidaka penati (3) katika mechi (6) kwenye michuano hiyo ya CHAN.
Mwaka 2020 Djigui Diarra allisaidia tena timu yake ya taifa ya Mali kutinga tena fainali ya CHAN,, Katika michuano hiyo aliweka rekodi ya kucheza dakika (365′) bila kuruhusu goli kwenye nyavu zake, ikiwemo kudaka penati muhimu hatua ya nusu fainali dhidi ya Guinea.
Diarra alifika hatua ya (16) bora kwenye michuano ya AFCON mwaka 2019, alicheza mechi zote kwa dakika (90′) Alifungwa goli (1) na timu ya taifa ya Ivory Coast goli la Wilfred Zaha.
Mwaka 2016)Diarra alichaguliwa kwenye kikosi bora cha (CAF) Huyo ndiye Djigui Diarra, sio kwamba ubora alionao ameanzia Yanga kuuonesha, ni golikipa bora hata kwenye michuano mikubwa ya kimataifa tangu zamani.
Kutokana na rekodi zake lakini pia na namna anavyoendelea kuonesha kuwa yuko vyema katika kikosi ha timu ya taifa ya Mali ni wazi kwamba bado anayo nafasi ya Kwenda kukipiga Ulaya.
SOMA ZAIDI: Mauritania Mmejitahidi Bahati Sio Yenu