BAADA ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, uliochezwa Desemba 20, Medeama ya Ghana imemfuta kazi kocha wake mkuu, Evans Adotey kutokana na matokeo hayo mabaya.
Evans amekiongoza kikosi cha medeama katika michezo minne ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na kuvuna alama nne na kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi D, linaloongozwa na Al Ahly mechi tatu pointi tano, nafasi ya pili Yanga mechi nne pointi tano na ya tatu ni CR Belouizdad mechi tatu pointi nne.
Hata hivyo, baada ya kufutwa kazi kama kocha mkuu, timu hiyo imempa majukumu mengine ya ukurugenzi wa fundi wa klabu hiyo cheo alichokuwa nacho awali katika timu hiyo kabla ya kuwa kocha mkuu.
Katika Ligi Kuu Ghana kocha huyo amekiongoza kikosi hicho katika mechi 11, nakuvuna pointi 16, akishika nafasi ya 12 katika timu 18 na ameshinda mechi tano, amepoteza tano na sare moja.
Katika hatua ya makundi Medeama bado ina michezo miwili dhidi ya Al Ahly na CR Belouizdad.
Endelea kufuatilia taarifa za bara la Afrika kuelekea AFCON kwa kusoma hapa.