Stade de Marrakech ni uwanja wa michezo uliopo katika mji wa Marrakech, Morocco. Uwanja huu una uwezo wa kuchukua takribani watazamaji 45,240 na unatumika hasa kwa michezo ya mpira wa miguu.
Ujenzi wa uwanja huu ulikamilika mwaka 2011 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la FIFA. Uwanja huu ulikuwa moja ya viwanja vilivyotumika kama uwanja wa michezo wakati wa Kombe la Dunia la FIFA kwa Vilabu mwaka 2013 na ni moja ya viwanja vya kisasa zaidi nchini Morocco. Ina viti vyote vya kisasa kwa watazamaji lakini pia nae neo zuri kwa vyombo vya habari , ikitoa uzoefu mzuri kwa watazamaji na waandishi wa habari.
Licha ya kutumika na vilabu lakini pia timu ya taifa ya Morocco imekua mwenyeji wa mechi za kimataifa katika dimba hili ambapo wameweza kucheza mechi za kimataifa mbalimbali.
Mbali na mpira wa miguu, uwanja huu pia hutumiwa kwa matukio mengine ya michezo kama mechi za rugby na tamasha la muziki ambapo pia ndani ya uwanja huu kuna vituo vya chakula na vinywaji, pamoja na maduka ya kuuza bidhaa za michezo.
Hii leo klabu ya Simba watautumia uwanja huu kucheza na Wydad Casablanca mchezo wa klabu bingwa barani Afrika hatua ya makundi. Mchezo ambao mashabiki wengi wa soka Tanzania wanasubiri kuona utakua mchezo wa aina gani na mulekeo wa kundi utakuwaje kufuzu robo fainali ambapo mpaka sasa Wydad hana alama yoyote huku klabu ya Simba wakiwa na alama 2 anayeongoza kundi ni ASEC uakiwa na alama 4 akifuatiwa na Jwaneng mwenye alama 4 naye katika kundi hilo.
Wydad Casablanca ni klabu ya mpira wa miguu iliyopo Casablanca, Morocco. Ilianzishwa mnamo mwaka 1937 na imechukua jukumu kubwa katika soka nchini Morocco ikiwa ni moja wapo ya vilabu maarufu nchini humo na pia katika bara la Afrika.
Kwa habari zaidi za michezo ya ligi ya mabingwa barani Afrika pamoja na ulaya unaweza kusoma hapa.